Makunyanzi na mvi vinatishia uzuri wangu

Makunyanzi na mvi vinatishia uzuri wangu

kwi kwi kwi kwi kwi ni PM nikupe dawa za kupunguza uzee anatumia mzee wangu zimetoka marekani ni mbogamboga ziko kwenye mfumo wa vidoge hazina side effect hutazeeka kamwe hata rais bush anatumia
 
Do not worry always be happy; hautapata makunyanzi maisha yako yote!!!

Katika hii ardhi ya JK kuishi happy always ni sawa na kuwaza uwezekano wa kuwa happy dak 2 tu kule jehanam....which is just an illusion
 
Katika hii ardhi ya JK kuishi happy always ni sawa na kuwaza uwezekano wa kuwa happy dak 2 tu kule jehanam....which is just an illusion

Do not give up; there seems to be light at the end of the tunnel!!! Mandela angekata tamaa leo hii South afrika ingekuwa wapi? Kaza buti kamanda.
 
Najionea huruma sana nikifikiria kuwa miaka mitano ijayo nitakuwa na mvi na makunyanzi.Ngozi yangu haitakuwa kama leo, ntakuwa na miaka 35.Miaka 35 inabakiza miaka 15 tu niwe na miaka 50.Ndoto yangu ni kuendelea kuwa mrembo hata ntakapofika miaka 75.Najua kwa umri huo hata nikiwa na makunyanzi na mvi, umbo langu litakuwa kama nilivyo sasa. Hips za ukweli, kiuno kudogo na mzigo wa kichokozi nyuma.Nikifikiria uzee najihisi kuchanganyikiwa.CC: Madame B unayetaka watu8 aje kukupa huduma za massage nyumbani kwako
i recommend plastic surgery
 
Last edited by a moderator:
Najionea huruma sana nikifikiria kuwa miaka mitano ijayo nitakuwa na mvi na makunyanzi.
Ngozi yangu haitakuwa kama leo, ntakuwa na miaka 35.
Miaka 35 inabakiza miaka 15 tu niwe na miaka 50.
Ndoto yangu ni kuendelea kuwa mrembo hata ntakapofika miaka 75.
Najua kwa umri huo hata nikiwa na makunyanzi na mvi, umbo langu litakuwa kama nilivyo sasa. Hips za ukweli, kiuno kudogo na mzigo wa kichokozi nyuma.
Nikifikiria uzee najihisi kuchanganyikiwa.
CC: Madame B unayetaka watu8 aje kukupa huduma za massage nyumbani kwako

Pata ushauri wa Tina Turnner
 
Umenitega hapo nilipo bold. Na umenipata. Kile kiwanja changu cha Mbezi Beach niuze nikupe hela, au nikupe hicho kiwanja? Chagua moja!
 
Kula vizuri healthy diet, mazoezi, lala vizuri na usitumie vipodozi vyenye kemikali try uwe natural as possible
 
Akina Latoya,janet,madona, oprah,Marry, Naomi,wanatumia nini hawa wanawake! Mbona hawazeeki! Hata mrs Obama ni wa mwaka 196...... Lakini bado mrembo
 
Najionea huruma sana nikifikiria kuwa miaka mitano ijayo nitakuwa na mvi na makunyanzi.
Ngozi yangu haitakuwa kama leo, ntakuwa na miaka 35.
Miaka 35 inabakiza miaka 15 tu niwe na miaka 50.
Ndoto yangu ni kuendelea kuwa mrembo hata ntakapofika miaka 75.
Najua kwa umri huo hata nikiwa na makunyanzi na mvi, umbo langu litakuwa kama nilivyo sasa. Hips za ukweli, kiuno kudogo na mzigo wa kichokozi nyuma.
Nikifikiria uzee najihisi kuchanganyikiwa.
CC: Madame B unayetaka watu8 aje kukupa huduma za massage nyumbani kwako

Hizo ni hatua tu za makuzi,.Mbona huzungumzii hali uliyokua nayo kipindi una miaka 18-20-22? Dada wa umri wa miaka 30 halingani na wa miaka 20 kwa urembo na mvuto..Usiwe na hofu,Hiyo hali jamii inaikubali sema wewe binafsi unataka kushindana na NATURE.
 
Najionea huruma sana nikifikiria kuwa miaka mitano ijayo nitakuwa na mvi na makunyanzi.
Ngozi yangu haitakuwa kama leo, ntakuwa na miaka 35.
Miaka 35 inabakiza miaka 15 tu niwe na miaka 50.
Ndoto yangu ni kuendelea kuwa mrembo hata ntakapofika miaka 75.
Najua kwa umri huo hata nikiwa na makunyanzi na mvi, umbo langu litakuwa kama nilivyo sasa. Hips za ukweli, kiuno kudogo na mzigo wa kichokozi nyuma.
Nikifikiria uzee najihisi kuchanganyikiwa.
CC: Madame B unayetaka watu8 aje kukupa huduma za massage nyumbani kwako

Wakati ukuta ukishindana nao utaumia mwenyewe. Kubali matokeo. Saa nyingine kukataa umri nako kunaweza kukuingiza kwenye majanga
 
[TABLE="align: left"]
[TR]
[TD="align: left"] [h=2]AHAAAAAAAAAAA UMENIKUMBUSHA HILI SHAIRI, HEMBU TIRIRIKA
UJANA
[/h]
  1. Ujana kitu kitamu, tena ni azizi sana
    Maungoni mwangu humu, nilikuwa nao jana
    Kwa wingi katika damu, tahamaki leo sina!
    Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana.
  2. Kichwa kimejaa mvi, kinywani meno hamna
    Nikenda kama mlevi, miguu nguvu haina
    Kumbe ujana ni hivi, ukenda hauji tena!
    Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana.
  3. Jua langu limekuchwa, na nyota nilizoona
    Ukinitizama kichwa, nywele nyeusi hakina
    Kama zilizofikichwa,zikang'olewa mashina
    Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana.
  4. Natatizika kauli, midomo najitafuna
    Nimekusanya adili, walakini hali sina
    Dunia kitu bahili, hiki una kile huna!
    Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana.
  5. Nilikuwa ni waridi, furaha ya wasichana
    Neno hawakunirudi, wakati wa kukutana
    Sasa nanuka baridi, wanionapo waguna
    Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana.
  6. Walio wakinibusu, walikuwa wengi sana
    Wanawake wenye busu, uzuri na usichana
    Sasa sina hata nusu, ya wanitajao jina
    Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana.
  7. Wazuri wenye uturi, na mikono yenye hina
    Kila mtu mashuhuri, alipenda kuniona
    Nilifaa kwa shauri, na sasa sauti sina
    Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana.
  8. Dunia bibi arusi, kwa watu kila namna
    Inapendeza nafsi, wakati wa kuiona
    Na leo sina nafasi, kwa uzee kunibana
    Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana.
  9. Kilichokuwa gizani, niliweza kukionap
    Nikakijua thamani, sura yake hata jina
    Sasa sijui ni nini, hata ikiwa mchana
    Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana.
  10. Kilichotaka fikira, niliweza kukinena
    Kwa mfano na kwa sura, mpaka kikafanana
    Leo tazama hasara, nguvu hiyo sina tena
    Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana.
  11. Kilichotaka mapimo, sikifahamu mapana
    Marefu yake na kimo, siifahamu bayana
    Nusu nimo nusu simo, duniani najionap
    Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana.
  12. Hadumu nasikitika, rafiki yangu ujana
    Machozi yamiminika, na la kutenda hapana
    Ni wakati umefika, uzee dawa hauna
    Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana.
  13. Hauna dawa uzee, mabega yamepetana
    Anionaye ni"wee!, ondoka hapa laana"
    Wanaposema na miye, niliyekuwa na jina!
    Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana.
  14. Wakatabahu shairi, uchungu wanitafuna
    Walakini nafikiri, twafuata Subuhana
    Katika ile amri, ya"kuwa"na "kutengana"
    Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Najionea huruma sana nikifikiria kuwa miaka mitano ijayo nitakuwa na mvi na makunyanzi.
Ngozi yangu haitakuwa kama leo, ntakuwa na miaka 35.
Miaka 35 inabakiza miaka 15 tu niwe na miaka 50.
Ndoto yangu ni kuendelea kuwa mrembo hata ntakapofika miaka 75.
Najua kwa umri huo hata nikiwa na makunyanzi na mvi, umbo langu litakuwa kama nilivyo sasa. Hips za ukweli, kiuno kudogo na mzigo wa kichokozi nyuma.
Nikifikiria uzee najihisi kuchanganyikiwa.
CC: Madame B unayetaka watu8 aje kukupa huduma za massage nyumbani kwako
kula mbogamboga na matunda kama huna akili nzuri,pamoja na mazoezi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom