Malaika mikaeli alifanikiwa kuchukua mwili wa Musa shetani alipougombea, ukifa mwili wako utachukuliwa na nani? Amua sasa!!

Malaika mikaeli alifanikiwa kuchukua mwili wa Musa shetani alipougombea, ukifa mwili wako utachukuliwa na nani? Amua sasa!!

Ngoja kwanza. Kunakugombania maiti Tena?
FB_IMG_1734918834606.jpg
 
Mhubiri kajaribu kuzungumza sana kuhusu habari za kifo Cha mwanadamu lakini bado hakuna majibu sahihi kuwa mtu akifa anaenda kupumzika au anaenda kuzimu
Aliyeandikwa kitabu Cha muhubiri ni Nabii Suleiman,

Hakujua wapi ataenda akifa,ndomana aliuliza swali, nani ajuaye Roho huenda juu au chini!! lakini Yesu ameliweka wazi kabisa wapi mtu akifa ataenda,

Rejea majibu ya Yesu Kwa yule jambazi pale msalabani,

Pia jiulize Musa na Elia walikuwa wamekufa zamani, iweje wamtokee Yesu mlimani na wanafunzi wakiona Ili kumtia moyo.

Ndipo ujue Mbinguni watu wanaingia miili ikifa,

Na kuzimu daily wanaingia.

Sasa the choice is yours.
 
Source:

(Mathew 17:1-13) Ukisoma mistari hiyo juu, utakuwa kuwa,

Musa alimtokea Yesu mlimani akiwa na Elia na wakamtia Moyo.

Ndipo ujue mtu ni ROHO,

Hadi ni WA milele,

Mwili ni wa muda tu, usikudanganye, ni vazi la Roho, Roho ndiye mtu halisi mwenyewe.

Ubarikiwe🙏
Musa na Elia ni very unique examples kwenye bible. Hawakuwa na 'vifo' vya kawaida kama watu wengine.

Kuwatolea mfano kama ushahidi wa wafu kuwa mbinguni au jehanamu ni kulazimisha mambo.
 
Mhubiri kajaribu kuzungumza sana kuhusu habari za kifo Cha mwanadamu lakini bado hakuna majibu sahihi kuwa mtu akifa anaenda kupumzika au anaenda kuzimu
Pia ukiweza kujua mtu ni nani,

Utakuwa position nzuri ya kuelewa maandiko.

Mtu ni ROHO, anayo NAFSI na anaishi ndani ya MWILI.

Mwili utazikwa, Roho haizikwi.

Mwili utaoza, Roho haiozi.
 
Musa na Elia ni very unique examples kwenye bible. Hawakuwa na 'vifo' vya kawaida kama watu wengine.

Kuwatolea mfano kama ushahidi wa wafu kuwa mbinguni au jehanamu ni kulazimisha mambo.
Kifo Cha kawaida ni kipi na kifo kisicho Cha kawaida ni kipi?

Na BIBLIA Iko wazi kuwa Musa na Elia walitokea Mbinguni kuja kumtia moyo Yesu, na walionekana kama tu Malaika.

Rejea majibu ya Yesu Kwa mafarisayo,

Aliwambia, Mbinguni hakuna Kutoa Wala kutolewa, watu wakuwa na miili kama ya Malaika, na miili hiyo ya utisho ndiyo ilimtisha Petro akiamini Musa na Elia ni miungu sababu ya kungaa kwao.

Mimi na pambana nirudi Mbinguni nilikotoka kabla ya kuingia ndani ya tumbo la manangu na Kuzaliwa.
 
Wakisha gombania??? Kumbe wanagombanaga sikujua hili ajabu.
Hilo tendo la kugombea miili ni endelevu.

Ukiona tu mtu kakata kwamba, jua Malaika wa Giza na WA Nuru wako vitani kugombea miili.
 
Source:

(Mathew 17:1-13) Ukisoma mistari hiyo juu, utakuwa kuwa,

Musa alimtokea Yesu mlimani akiwa na Elia na wakamtia Moyo.

Ndipo ujue mtu ni ROHO,

Hadi ni WA milele,

Mwili ni wa muda tu, usikudanganye, ni vazi la Roho, Roho ndiye mtu halisi mwenyewe.

Ubarikiwe🙏
Nani alithibitisha kama aliyemtokea ndio mussa mwenyewe?
 
Salaam, shalom!!

MADA hii ni fundisho Kwa wale wasioamini kwamba mtu afapo, mwili wake hupelekwa either Kuzimu au Mbinguni.

Na mwili unaopelekwa kuzimu ni mwili upi? Ni huu wa Damu na nyama?

Jibu ni Rahisi tu,

Mtu ni ROHO, anayo NAFSI, anaishi ndani ya MWILI.

Na ikiwa mtu ni ROHO, uwe na HAKIKA kuwa, mwili wa nyama ni vazi la Roho, hivyo shetani Huwa Hana habari sana na mwili/ vazi, Hilo vazi Huwa ni nyama ya wachawi, funza nk nk.

Anakufa Musa, shetani anakuja kuchukua mwili wa Musa aupekeke gerezani la kuzimu, hapo hapo Malaika mkuu naye anatokea kuchukua mwili wa Musa aupekeke Mbinguni.

Utaniuliza, Musa alikuwa na utashi wakati mwili wake ukigombaniwa na Malaika Mikael na shetani? Jibu ni ndio, afapo mtu, huona Kila kitu Kwa macho Yale halisi ya ndani, mfano mzuri ni macho ya ndotoni wakati ya MWILI yanapofumba unaonaje!!

Malaika mkuu Mikaeli anafanikiwa kuutwaa mwili wa Musa na kupeleka Mbinguni.

Na kuthibitisha kuwa Musa Yuko Mbinguni, Musa alimtokea Yesu pale mlimani na kuongea naye akimtia moyo, ndipo ujue kuwa Mbinguni hata sasa, WATAKATIFU wapo waliokufa ( Roho iliyo hai ilipotengana na miili ya kuharibika) Kisha wakaingia Mbinguni. Na wapo walioingia kuzimu na wanateswa gereza la muda chini kuzimu.

SOURCE: YUDA (1:9)

Ikiwa ungependa Malaika mkuu Mikaeli apate kibali Cha kukupeleka Mbinguni baada ya MWILI huu kufikia mwisho wa uhai, pumzi itapokata, yaani ukitaka Malaika mkuu Mikaeli auchukue mwili wako Kwa kumshinda shetani ambaye pia anautaka, fuatisha Sala hii.

EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, ULEVI USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. AMEN

KARIBUNI 🙏
Alafu Munuu amabaye hadi Mungu alikuwa anaongea nae ana kwa ana then shetani aje kutaka mwili kweli..? Mmh
 
Ndio ile mke na wanandugu kugombea mwili???
No,

Mwili ulionao wa Damu na nyama ni photocopy ya MWILI halisi wa Roho.

Mtu ni ROHO mwenye mwili wa Roho wenye viungo kama tu wa mwili.

Unaogombewa uende kuzimu au Mbinguni ni mwili wa Roho ambao ndio mtu halisi.

N B: Mtu ni ROHO anayo NAFSI na anaishi ndani ya MWILI wa nyama.
 
Nani alithibitisha kama aliyemtokea ndio mussa mwenyewe?
Petro na Yohana waliona na kuthibitisha kuwa wale ni Musa na Elia.

Yesu akikutokea Leo, Hana haja ya kujitambulisha, utamjua huyu ni Yesu,

Macho ya Roho hayana limit kujua mambo, ikiwa mchawi akikujia unamwona, na ungeweza kuona sura yake asingenuiza kujificha Kwa mwonekano wa paka au nyoka au mbwa, ndipo ujue unatakiwa ujue wewe u nani.
 
Back
Top Bottom