Malaika mikaeli alifanikiwa kuchukua mwili wa Musa shetani alipougombea, ukifa mwili wako utachukuliwa na nani? Amua sasa!!

Malaika mikaeli alifanikiwa kuchukua mwili wa Musa shetani alipougombea, ukifa mwili wako utachukuliwa na nani? Amua sasa!!

No,

Mwili ulionao wa Damu na nyama ni photocopy ya MWILI halisi wa Roho.

Mtu ni ROHO mwenye mwili wa Roho wenye viungo kama tu wa mwili.

Unaogombewa uende kuzimu au Mbinguni ni mwili wa Roho ambao ndio mtu halisi.

N B: Mtu ni ROHO anayo NAFSI na anaishi ndani ya MWILI wa nyama.
Haya bhana.
 
Alafu Munuu amabaye hadi Mungu alikuwa anaongea nae ana kwa ana then shetani aje kutaka mwili kweli..? Mmh
Ukifa tu,

Lazima Shetani au Malaika wa Nuru waje.

Hiyo ni kanuni na Utaratibu. Lazima uende unakostahili.
 
Kristo akubariki ktk huduma yako.
Ubarikiwe pia 🙏

Usiache kuomba Ili Mungu aongeze watendakazi shambani mwake maana mavuno ni mengi ila watendakazi ni Wachache.
 
Salaam, shalom!!

MADA hii ni fundisho Kwa wale wasioamini kwamba mtu afapo, mwili wake hupelekwa either Kuzimu au Mbinguni.

Na mwili unaopelekwa kuzimu ni mwili upi? Ni huu wa Damu na nyama?

Jibu ni Rahisi tu,

Mtu ni ROHO, anayo NAFSI, anaishi ndani ya MWILI.

Na ikiwa mtu ni ROHO, uwe na HAKIKA kuwa, mwili wa nyama ni vazi la Roho, hivyo shetani Huwa Hana habari sana na mwili/ vazi, Hilo vazi Huwa ni nyama ya wachawi, funza nk nk.

Anakufa Musa, shetani anakuja kuchukua mwili wa Musa aupekeke gerezani la kuzimu, hapo hapo Malaika mkuu naye anatokea kuchukua mwili wa Musa aupekeke Mbinguni.

Utaniuliza, Musa alikuwa na utashi wakati mwili wake ukigombaniwa na Malaika Mikael na shetani? Jibu ni ndio, afapo mtu, huona Kila kitu Kwa macho Yale halisi ya ndani, mfano mzuri ni macho ya ndotoni wakati ya MWILI yanapofumba unaonaje!!

Malaika mkuu Mikaeli anafanikiwa kuutwaa mwili wa Musa na kupeleka Mbinguni.

Na kuthibitisha kuwa Musa Yuko Mbinguni, Musa alimtokea Yesu pale mlimani na kuongea naye akimtia moyo, ndipo ujue kuwa Mbinguni hata sasa, WATAKATIFU wapo waliokufa ( Roho iliyo hai ilipotengana na miili ya kuharibika) Kisha wakaingia Mbinguni. Na wapo walioingia kuzimu na wanateswa gereza la muda chini kuzimu.

SOURCE: YUDA (1:9)

Ikiwa ungependa Malaika mkuu Mikaeli apate kibali Cha kukupeleka Mbinguni baada ya MWILI huu kufikia mwisho wa uhai, pumzi itapokata, yaani ukitaka Malaika mkuu Mikaeli auchukue mwili wako Kwa kumshinda shetani ambaye pia anautaka, fuatisha Sala hii.

EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, ULEVI USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. AMEN

KARIBUNI 🙏
Mwili wa Musa ulichukuliwa ili waisrael wasijue alipozikwa wakapaabudu badala ya Mungu chief si zaidi. Jifunze biblia tena.
 
Musa na Elia ni very unique examples kwenye bible. Hawakuwa na 'vifo' vya kawaida kama watu wengine.

Kuwatolea mfano kama ushahidi wa wafu kuwa mbinguni au jehanamu ni kulazimisha mambo.
Yn 11:25-26 SUV
[25] Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; [26] naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?
 
Maisha yangu Mimi.........

Nani atayathamini......

Usipomruhusu huyu Yesu....

Yeye kufanya marekebisho.....

Ukiiifa Leo wewe!! Naniii atakuthamini....

Usipomruhusu huyu Yesu...

Yeye kufanya marekebisho....

secretarybird
Kumbe Kuna maisha baada ya kufukiwa huu mwili wa Damu na nyama.

Na maisha hayo ni ya milele Mbinguni au jehannum!

Sasa miaka 100 ya duniani, kamwe sitokubali yanikoseshe mbingu ya milele.

Ubarikiwe 🙏
 
Mwili wa Musa ulichukuliwa ili waisrael wasijue alipozikwa wakapaabudu badala ya Mungu chief si zaidi. Jifunze biblia tena.
Rudia kusoma,

Yuda 1:9

Maandiko yasema Malaika mkuu Mikaeli na Shetani waliugombea mwili wa Musa, na Mikaeli akashinda.

Hayo uliyoandika umeyatoa source ipi?
 
Kumbe Kuna maisha baada ya kufukiwa huu mwili wa Damu na nyama.

Na maisha hayo ni ya milele Mbinguni au jehannum!

Sasa miaka 100 ya duniani, kamwe sitokubali yanikoseshe mbingu ya milele.

Ubarikiwe 🙏
Amen amen niombee
 
Ila izi stori za wazungu na waarabu zimetuweza sana wafrka
NENO la Mungu Si story,

Kama ambavyo pumzi uvutayo Bure hutoka Kwa Mungu, kadhalika Neno lake ni halisi Kweli na HAKIKA.

Acha hicho kibri Cha Uzima, siku za mwanadamu duniani ni chache sana, tena zimejaa taabu.
 
Amen amen niombee
Ni maombi yangu Mungu aongoze hatua zako,

Ukakue zaidi Kila siku katika nyanja zote maishani mwako.

Ukawe na siku nyingi zilizojaa furaha na baraka. Ukatumike shambani mwa BWANA ukimzalia matunda mema yaufukiao Uzima WA milele.

Aaaamen.
 
Back
Top Bottom