Tetesi: Malalamiko dhidi ya afisa utumishi wa wilaya ya Hai juu ya upendeleo kwa watumishi

Tetesi: Malalamiko dhidi ya afisa utumishi wa wilaya ya Hai juu ya upendeleo kwa watumishi

prosmote

New Member
Joined
Apr 3, 2020
Posts
1
Reaction score
0
MALALAMIKO DHIDI YA AFISA UTUMISHI WA WILAYA YA HAI JUU YA UPENDELEO KWA WATUMISHI

Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Hai dhidi ya afisa utumishi wao. Mwana mama huyu amekuwa na kiburi na ubaguzi mkubwa/UBABE/upokeaji wa rushwa/fitna/kejeli/masimango kwenye kutoa haki kwa baadhi ya watumishi wa halmashauri ya wilaya ya hai. Anatoa upendeleo kwa marafiki zake na watu ambao wanao uwezo wa kumpa rushwa ili aweze kutekeleza au kutekelezewa Suala Lake;(usipotoa chochote Hai utakwama tu)

Kwa leo nitazungumzia idara mbili tu na watumishi 2 tu ;

1; IDARA YA AFYA

MTUMISHI WA IDARA YA AFYA ANYWA SUMU KUJIUA WILAYA YA HAI


Tarehe 1/4/2020 mtumishi mmoja ambaye inasadikika ni nurse hospitali ya wilaya ya Hai alimemeza vidonde kutaka kujiua kwa kile kinachosadikiwa ni manyanyaso na mateso ya kuonewa na kunyanyaswa na afisa utumishi wa wilaya ya Hai kwa kutokumsikiliza matatizo yake. Mtumishi huyu alisikika (jina tunalihifADHI) Alisikika akiwa anapiga yowe kwenye ofisi za afisa utumishi kwa kile anachodai amechoka kuonewa kazini;

Swali; hadi mtumishi anafikia kujiua kweli ketengo cha rasilimali watu hamuoni kuna matatizoooo; na matatizo yanaanzia hapo hapo kwenu?; ni dhahiri pasipo na shaka kuwa idara hii imekuwa inawatesa watumishi kwa vitendo; kuna wengine hawajafikia kunywa sumu au kujiua lakini wanaumia na wanateseka mmno;je nani wa kuwasikiliza kama idara yenyewe ipo hivyo?

2; KITENGO CHA TEHAMA

IDARA YA ITs (TEHAMA) HAI


Katika hali ya kushangaza afisa utumishi wa wilaya ya Hai amemwamisha shosti wake wa karibu (Jina limehifadhiwa) kutoka Moshi Vijijini akiwa kama mwalimu na kumhamishia wilaya ya Hai (uhamisho ulipangwa kwa makusudi); Baada ya kumhamishia huyo shosti wake afisa utumishi huyu alifanya lobbing na kuazimwa idara ya Tehama ya wilaya na mpango uliopo kwa sasa ni wa kumfanyia recategorization shosti huyo;

Kinachoshangaza; ni kuwa katika wilaya ya Hai wapo walimu na watumishi wa kada nyingine waliosomea ITs ambao wana sifa KULIKO SHOSTI HUYO za kufanya kazi hiyo ya tehama ;

swali; ni kwanini ahamishe mtu kutoka moshi vijijini aje afanyiwe recategorization wilaya ya Hai angali hapahapa Hai wapo watumishi wenye sifa hiyo?

Cha kushangaza zaidi kwenye idara hiyohiyo yupo mtumishi ambaye ni mwalimu(Jina limehifadhiwa) ameazimwa na anafanya kazi kama IT na hadi leo hii hajafanyiwa recategorization kwa kuwa hajatoa chochote kwa afisa utumishi huyo; Huu ni uonevu mkuwa sana,wapo wengi wenye matatizo HAI ambao wakisema hawasikilizwi kwa kuwa hawajatoa rushwa ili mambo yao yafanikiwe ( ) Kuna shida wilaya ya HAI;

HATA HIVYO; KWA KUWEKA KUMBUKUMBU SAWA AFISA UTUMISHI WA WILAYA YA HAI ALIHAMISHWA KUTOKA MOSHI VIJIJINI AKALETWA WILAYA YA HAI .HIVYO AMERUDISHA FADHILA KWA SHOSTI WAKE;

Viongozi wapo na hawajui matatizo ya watumishi wake; mkurugenzi yupo ila hajui matatizo ya watumishi wake?


Nitaedelea kutoa wengine toleo lijalo kwa watu wengine na idara nyingine ambazo watumishi wake wananyanyasika na kuteswa kazini ….stay tune THIS WEEK////NITACHAMBUA IDARA MOJA BAADA YA NYINGINE

MZALENDO

HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI
 
Kabla hatua zozote hazijachukuliwa vyema na huyo mama asikilizwe, ni rahisi sana kuja hapa kwa fake ID kwasababu hata kama ukiandika uongo hakuna atakayekufahamu, hivyo ni rahisi kumuonea mwingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu unacho sema NI kweli naye aje hapa akanushe.

Hawa ma HR ni wanyanyasaji usipime na mkimpata HR mwadilifu hamudumu naye sijui kwanini

Kuna Afisa utumishi mmoja kwa Sasa Yuko Halmashauri mojawapo mkoani kagera kwa kweli alikuwa mtu wa watu kule Mbinga DC

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UNAFAHAMU KAZI YA TUME YA UTUMISHI WA UMMA??

1. KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO
2. KUSHUGHULIKIA RUFAA

Nenda kwao utasaidiwa
 
HR wengi hasa private sector wanajiona miungu watu ukizinguana nae ukicheza kesho huna kazi. Sometime ofisini Huwa nawaonea huruma sana wafanyakazi wanawake ni victim wakubwa wa hawa ma HR. Asipotoa mzigo kibarua kinaweza ota mbaya
 
Kabla hatua zozote hazijachukuliwa vyema na huyo mama asikilizwe, ni rahisi sana kuja hapa kwa fake ID kwasababu hata kama ukiandika uongo hakuna atakayekufahamu, hivyo ni rahisi kumuonea mwingine.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ishu ya fake ID haina maana, muhimu ni taarifa imetolewa.

Ndiyo maana kuna MASUNDUKU YA MAONI karibu kila ofisi/taasisi ya umma. Na mtu atoae maoni yake, halazimiki kuandika jina lake halisi. Lengo ni kuwalinda watoa taarifa dhidi ya wanaotolewa taarifa.....

Ipo idara ya habari na mawasiliano ya wilaya, wanapaswa kukanusha au kukubali na kuomba radhi na kisha kujirekebisha.

Na la muhimu zaidi ni kwa vyombo vya uchunguzi (PCCP, TISS nk ) kupokea taarifa hii, waichunguze na kuifanyia kazi.

Mfano iko kesi mahakamani dhidi ya JF vs CRDB vs GSM. Jamii Forum wakilazimishwa kutoa taarifa za WHISTLEBLOWER juu ya tuhuma dhidi ya benki ya CRDB na kampuni ya GSM.

Sasa hebu jaribu kufikiri kama mtoa taarifa huyu angekuwa anajulikana, unadhani nini kingetokea?

Nakuhakikishia wangemalizana naye mitaani tu bila kufuata taratibu za kisheria kama alivyotaka kumalizwa Tundu Lissu....!!
 
Ndo ume comment hapo unajua kwa nini jf ina kesi mahakaman ni kwa ajili ya kulinda watoa taarifa kama hawa ni jukumu letu kuanika na kusambaza uovu either tukiwa tumejificha ama tukiwa tunaonekana
Wazalendo siyo waoga bwashee!

Unamkumbuks Zitto wa Buzwagi au Kafulila aka Tumbiri wa Escrow?.....ule ndio uzalendo!
 
Hivi hapo si ndo pana Mkuu wa Wilaya anajifanyaga anasikiliza sana shida za wadau ofisini kwake pale kwenye kona huku amezungukwa na walinzi wenye mitutu au ni geresha. Kama ameshindwa tu kusikiliza kero za ofisi ya nne kutoka kwake ataweza kweli kusikiliza kero za kule Lawate, Kule Federici

Sent using Jamii Forums mobile app
Mleta mada hajasema ameshapeleka malalamiko kwa DC akashindwa! Vile vile inaweza ikawa wivu tu! Ndiyo maana tumemshauri aripoti kwenye mamlaka ili walishughulikie ili pande zote zipate muda wa kusikilizwa.
 
Back
Top Bottom