Nashauri kama bro, msomi, mchamungu, tajiri na kiongozi.
1. Huwa siafiki mwalimu wa msingi au sekondari kufanywa IT kwenye Halmashauri kwakuwa anajua kuformat flash na kuinstall window, big NO. Kwasababu hicho kitengo kina posho na marupurupu mengi, wakinogewa wanaiba chapuchapu ili siku akiondolewa asijilaumu. So kama huyo shosti yake hana Degree ya TEHAMA hafai kuwa kwenye hicho kitengo. Mkurugenzi anapaswa kupeleka maombi yake Utumishi aletewe wataalamu ikiwa ikama haijatimia. Wakati mkisubiri hao wataalamu waletwe yeyote mwenye ABC ya TEHAMA anaweza kuwekwa kitengoni kusaidia shughuli ziende kwa sharti kuwa mtaalamu akifika basi akubali kurudishwa kwenye nafasi yake ya zamani, kama ni mtendaji kijiji, nurse haya.
2. Hakuna utaratibu wa kumbadilishia mtu muundo wa utumishi kwakuwa amekaa kwenye kitengo kwa muda mrefu, LAWSON itakataa tu, so kama wewe ni mwalimu, huna degree ya TEHAMA, ila umewekwa kwenye kitengo cha TEHAMA kwa muda mrefu na haujajiongeza kupiga degree ya TEHAMA, unajichelewesha kupanda daraja lako la ualimu, watu wa TSC wanajua vizuri, waulize watakwambia
3. Kama kuna mwalimu amesomea TEHAMA, asisubiri huruma ya HR kupitia orodha ya watumishi ili kubaini uwepo wake, huyo mwalimu aandike barua kwenda kwa mkurugenzi kupitia kwa Mkuu wa shule na Afisa Elimu akiomba kubadilishiwa muundo, akikubaliwa ataondolewa ubaoni na kuletwa mezani kisha atapangiwa majukumu mapya ya AFISA TEHAMA.
4. Mtumishi huna sababu ya kujitoa uhai kisa kukerwa na HR wako, nchi hii ina Halmashauri zaidi ya 100, kama unaona hamuendani na HR wako, kuna haya mawili unaweza kufanya, kabiliana nae au muepuke.
Vipi utakabiliana nae?
(a) Ikiwa malalamiko yako ni ya msingi, sio mambo ya kuchukuliana wachumba, mripoti kwa mkurugenzi, ukiona Mkurugenzi analegalega, peleka malalamiko yako kwa RAS, mkurugenzi mpe nakala. Ukiona bado tatizo lako halijashughulikiwa na unaamini linapaswa kushugulikiwa, funga safari kamuone RC ukiwa na nakala ya barua zako zote ulizotoa malalamiko yako. Ukiona bado huko nako hakueleweki, ingia TAMISEMI Dodoma kamuone Katibu Mkuu, ila kwa utawala huu mpaka hapo kwa RC tatizo lako litakuwa solved. Unaweza kufikiria kwenda kushitaki, lakini hiyo iwe very last decision to make.
(b)Ikiwa ni jinai, kama hivyo ulivyodai kuwa anaomba rushwa, kama wewe ni mzoefu wa hapo hai utakuwa unajua takukuru ya hao kama wanafanya kazi kwa weledi au ni wababaishaji.
Wababaishaji kivipi? Iko hivi, wakimkamata mnyonge mnyonge fasta mahakamani, ila wakimkamata kibosile uchunguzi wanafanya miaka 100, basi ujue hao watakugeuka na kumtonya HR juu ya mpango wako, wanapigwa hela na wewe unakomolewa. Ila kama unaamini weledi wao, washirikishe na wataweka mtego wakumkamata.
Vipi umuepuke?
Ongea na DMO au Katibu wa afya, mueleze changamoto zako, kama ataweza kukusaidia kuongea nae huyo HR au kuongea na Mkurugenzi yakaisha salama kheri, ikishindikana waombe wakusaidie uhamisho uende kwenye halmashauri nyingine, maisha popote ndugu yangu.
5. Unaposema Viongozi hawajui, inamaana ofisi ya Mkurugenzi haiingiliki, hiyo ni hatari kwa afya ya watumishi wake, hususani wa ngazi za chini. Kila halmashauri ina madiwani watatu watata, ongea nao kwa nyakati tofauti, waombe wakusaidie kumhoji Mkurugenzi, usihofu hawatakutaja, ila hakikisha unawafeed taarifa sahihi na sio majungu, Mkurugenzi hatopenda kuona anafatwa fatwa kwa uzembe wa HR, trust me atafanya kitu kumshepu huyo mtu.
6. Kukomaa kuna tabu zake, ndio kama hizo, manyanyaso nk. Usijali yatapita.