A
Anonymous
Guest
Mimi ni mdau wa elimu na ninaomba utambulisho wangu ubaki kuwa siri kwa sababu za usalama.
Naomba mamlaka husika zifanye uchunguzi wa kina kuhusu mwenendo wa Mkuu wa shule huyu kutokana na tuhuma zifuatazo:
Aidha, ningeshauri mamlaka zinazohusika na uteuzi wa viongozi wa shule kuimarisha mchakato wa uhakiki wa historia ya utendaji na uwezo wa viongozi kabla ya kuwateua kusimamia taasisi za elimu. Hatua hiyo itasaidia kuhakikisha shule zinaongozwa na viongozi wenye weledi, uadilifu na uwezo wa kusimamia rasilimali za umma kwa kuzingatia sheria na maslahi ya wanafunzi.
Naomba mamlaka husika zifanye uchunguzi wa kina kuhusu mwenendo wa Mkuu wa shule huyu kutokana na tuhuma zifuatazo:
- Matumizi mabaya ya fedha za umma: Inadaiwa hutumia fedha za shule bila idhini ya vikao halali vya uongozi (SMT), kughushi nyaraka na kujilipa posho pamoja na malipo ya vikao yasiyo halali. Inasemekana sehemu kubwa ya fedha za shule hutumika kwa manufaa binafsi.
- Uchangishaji usiofuata taratibu: Anadaiwa kukusanya michango mbalimbali kutoka kwa wazazi kinyume na miongozo ya Wizara ya Elimu, ikiwemo michango ya ukarabati na ream za karatasi. Badala ya wazazi kuleta vifaa, huwataka watoe fedha taslimu zinazokusanywa kupitia baadhi ya walimu.
- Unyanyasaji wa wanafunzi: Wanafunzi wanaodaiwa kushindwa kulipa michango huadhibiwa kwa kupigwa, kurudishwa nyumbani au kuzuiwa kuingia shuleni, hali inayochangia utoro, kushuka kwa ufaulu na msongo wa mawazo.
- Matumizi ya lugha isiyofaa: Inadaiwa kuwa katika baraza la kufunga shule mwezi Juni aliwatukana wanafunzi kwa kutumia maneno ya kudhalilisha mbele ya walimu na wanafunzi.
- Kugawa walimu katika makundi: Inadaiwa hutumia uteuzi wa nafasi, posho na fursa mbalimbali kuwashawishi baadhi ya walimu ili wapate taarifa kuhusu wenzao, jambo linalodhoofisha mshikamano kazini.
- Uuzaji wa miti ya shule bila utaratibu: Kuna madai kuwa miti ya shule hukatwa na kuuzwa au kuchakatwa bila idhini ya vikao vinavyohusika na bila uwazi kuhusu matumizi ya mapato yake.
- Upokeaji wa wanafunzi kinyume cha utaratibu: Inadaiwa hupokea wanafunzi wa Kidato cha Kwanza ambao hawakuchaguliwa rasmi kupitia makubaliano ya siri na baadhi ya wazazi.
- Ukiukwaji wa taratibu za matumizi ya fedha na manunuzi: Kuna madai kuwa fedha za shule hutumika nje ya mafungu yaliyokusudiwa bila idhini, huku miradi ya ujenzi na ukarabati ikitekelezwa bila kufuata taratibu za manunuzi ya umma au kushirikisha Bodi ya Shule na SMT.
- Adhabu zisizozingatia sheria: Inadaiwa huwafukuza au kuwasimamisha masomo wanafunzi bila kufuata taratibu za kisheria, pamoja na kutumia adhabu za viboko kupita kiasi.