Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimeanza utaratibu wa kuwatoza wanafunzi malipo kwa ajili ya Carryover na Supplementary Examinations, utaratibu ambao umeanza kutumika hivi karibuni katika mwaka wa masomo 2025/2026.
Utaratibu huu umekuwa changamoto kubwa kwa wanafunzi, hasa wale wenye hali duni kiuchumi, kutokana na gharama kubwa zinazotozwa kwa ajili ya kurudia masomo. Kwa mfano, ada ya Carryover inaanzia takribani Shilingi 100,000 kwa kila somo, huku malipo ya Supplementary Examination yakiwa ni Shilingi 30,000 kwa kila mtihani.
Wanafunzi tunaomba ufafanuzi kutoka kwa uongozi wa chuo kuhusu msingi wa malipo haya, kwani tunataka kujua:
Malipo haya yanafanyika kwa mujibu wa utaratibu gani?
Fedha hizi zinapelekwa wapi na zinatumika kwa ajili ya huduma zipi?
Je, utaratibu huu unaendana na kanuni na miongozo inayosimamia elimu ya juu nchini?
Aidha, malipo hayo yanafanyika kupitia Control Number, hivyo wanaomba kuwepo kwa uwazi zaidi kuhusu makusanyo hayo na matumizi yake.
Tangu walipoweka ada ya kujisajili kwa wanafunzi wa mwaka wapili na kendelea nilijua tu yajayo yanafurahisha. Registration fee ilikuwa kwa mwaka wakwanza tu pale wabapojiunga chuo.Saivi kila mwaka wamasomo ubalipia kujisajili hadi umalize chuo