KERO Malalamiko kuhusu hali mbaya ya barabara ya Mbezi Makonde, bajeti zinatengwa ila haitengenezwi

KERO Malalamiko kuhusu hali mbaya ya barabara ya Mbezi Makonde, bajeti zinatengwa ila haitengenezwi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Barabara ya Mbezi Makonde kuelekea Baraza la Mitihani, kupitia eneo la kwa Mzee Warioba, Waziri Mkuu mstaafu, imekuwa katika hali mbaya kwa muda mrefu bila kufanyiwa ukarabati wa kudumu.

Kila tunapouliza kuhusu uboreshaji wa barabara hii, tunaambiwa wananchi tujichangie na kuitengeneza wenyewe. Tumekuwa tukishirikiana kusafisha na kurekebisha maeneo mbalimbali ili angalau barabara iweze kupitika, lakini sasa tumechoka. Pia, tumekuwa tukisikia kuwa bajeti za barabara zinatengwa, lakini hatuoni utekelezaji wake katika eneo letu.

Diwani na Mbunge wetu hatuwaoni mara kwa mara, hivyo wananchi hatujui wanachofanya kutatua changamoto hii.

Wakati wa mvua hali huwa mbaya zaidi. Udongo wa mfinyanzi huteleza na kufanya barabara isipitike, huku magari yakiharibika mara kwa mara. Kwa kuwa msimu wa mvua unakaribia, tunaomba eneo hili pia likumbukwe katika mipango na bajeti za maandalizi.

Maeneo mengine yanayozunguka kuelekea Goba yamewekewa lami, lakini bado kuna changamoto katika barabara ya kutoka Mbezi Garden kuelekea Baraza la Mitihani, njia ya Kanisa la Roma kuelekea Viwandani na inayounganisha maeneo hayo na Mbezi Africana.

Tunaomba mamlaka husika zifanyie kazi changamoto hii na kuhakikisha barabara hizi zinaboreshwa kwa kiwango cha kudumu. Wananchi tunahitaji barabara salama na inayopitika wakati wote, si kutegemea michango yetu kila mara.
 
Back
Top Bottom