KERO Malalamiko kuhusu huduma kwa wagonjwa wanaotumia bima ya afya katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi

KERO Malalamiko kuhusu huduma kwa wagonjwa wanaotumia bima ya afya katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kwa kuzingatia juhudi za Serikali za kuhamasisha mpango wa huduma ya afya kwa wote, ninajiuliza kuhusu hali inayoendelea katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, hususan namna wagonjwa wanaotumia bima ya afya wanavyohudumiwa.

Kuna siku nilimpeleka mgonjwa wangu aliyekuwa na jeraha la kuvunjika mguu lililoacha mfupa wazi (open fracture). Nilifika hospitalini saa 3:00 asubuhi, lakini mgonjwa alianza kuhudumiwa saa 7:00 mchana.

Kilichotokea ni kwamba mtumishi aliyekuwa na funguo za chumba cha upasuaji (theatre) hakuwepo kituoni, huku akiwa ameondoka na funguo za ofisi. Licha ya kupigiwa simu mara kadhaa, tulipewa majibu ya kuendelea kusubiri kwa sababu alikuwa anakuja.

Baada ya muda kupita, nilimsikia mmoja wa wahudumu wa hospitali hiyo akimpigia simu mtu ambaye nilidhani alikuwa mhusika mwingine wa chumba cha upasuaji, akimwambia: “Aisee, njoo haraka, kuna dili la laki mbili hapa.”

Haikupita hata dakika tano, mhusika huyo alifika akiwa na funguo. Alianza kutuuliza maswali kuhusu kilichotokea, nasi tukamweleza hali tuliyokuwa tumepitia na kumfahamisha kuwa tulikuwa tunatumia bima ya afya ya NHIF. Baada ya kusikia hivyo, mtumishi huyo alibwaga funguo na kuondoka zake.

Tukio hili limeniacha na maswali mengi kuhusu namna wagonjwa wanaotumia bima ya afya wanavyopokelewa na kuhudumiwa katika hospitali hiyo. Je, ni kweli wagonjwa wanaotumia bima wanapaswa kukutana na changamoto za aina hii wanapohitaji huduma za afya?

Tunaomba mamlaka husika, ikiwemo uongozi wa hospitali na mamlaka zinazosimamia huduma za afya na bima, zifanye uchunguzi wa kina kuhusu tukio hili na kuchukua hatua stahiki endapo yatabainika kuwepo kwa ukiukwaji wa taratibu.

Ikiwa kuna changamoto katika kupokea au kuhudumia wagonjwa wanaotumia NHIF katika hospitali hiyo, ni vyema wananchi wakaelezwa wazi ili wajue haki zao na utaratibu unaopaswa kufuatwa.

Huduma za afya zinapaswa kutolewa kwa wakati, kwa heshima na bila ubaguzi wa aina ya malipo. Maisha ya mgonjwa hayapaswi kuhatarishwa kwa sababu ya kucheleweshwa kwa huduma au masuala yanayohusiana na bima ya afya.

FB_IMG_1791538336449.jpg

FB_IMG_1791538346914.jpg
 
Tukiweka porojo pembeni.

MASLAHI YA WAHUDUMU WA AFYA TANZANIA NI DUNI SANA.

SWALA LAKO LA KUPAZA SAUTI TU KWA KUWAZA MGONJWA WAKO NA KUWASAHAU HAO WATUMISHI,INAONYESHA UBINAFSI NA KUTOKUWA NA NIA YA DHATI KUTAFUTA UFUMBUZI WA KIINI CHA TATIZO.

KUMPATA SPECIALIST WA MIFUPA NI GHARAMA NYINGI SANA.MUDA,JASHO NA DAMU.HUYU DAKTARI AMEJITOA SADAKA MAMBO MENGI KATIKA MAISHA MPAKA ANAKUWA BINGWA.

WATUMISHI WENGI WA AFYA WAISHI KWA KUPIGA DILI KAMA HIZO NDIO UNAONA WANAPATA VIHELA HATA VYA KUNYWA BIA,KUCHOMA NYAMA,WATOTO WANASOMA MAGARI YA NJANO,WANAENDESHA VIIST,VIPREMIO NA SPACIO.

KWA GROUND MAISHA YAO NI MAGUMU SANA WANAMIKOPO WANAILIPIA(WALIOKOPA KUFADHILI MASOMO YAO) NA MDENI KILA MAHALI.NA UHAKIKA WA KUPATA MATIBABU KWA BIMA YAKO PEKEE BILA KUCHANGIA HATA SENTI HIYO HAIPO KWENYE HII NCHI.

📌MFUMO MZIMA UNATAKIWA KUBADILIKA.BIMA IMEINGIZWA SIASA NYINGI KIASI HAKUNA UHALISIA WOWOTE NA HAIKIDHI MAHITAJI YA WALENGWA.
 
Back
Top Bottom