KERO Malalamiko kuhusu kuchelewa kuunganishiwa huduma ya TTCL Fiber Kigoma

KERO Malalamiko kuhusu kuchelewa kuunganishiwa huduma ya TTCL Fiber Kigoma

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wakazi wa Kigoma wanalalamikia kuchelewa kupatiwa huduma ya TTCL Fiber licha ya kulipia gharama za kuunganishiwa huduma hiyo zaidi ya miezi miwili iliyopita.

Inadaiwa kuwa kila wanapowasiliana na ofisi za TTCL huambiwa kuwa kuna uhaba wa vifaa, huku wakipewa ahadi za mara kwa mara ambazo hazijatekelezwa.

Kinachozua maswali zaidi ni kwamba baadhi ya nyumba za viongozi wa serikali zimeweza kuunganishiwa huduma hiyo ndani ya siku chache baada ya kuomba, tofauti na wananchi wa kawaida ambao wameendelea kusubiri kwa muda mrefu.

Wakazi hao wanataka kufahamu kama huduma hiyo inalenga viongozi na watu wenye uwezo pekee au inapatikana kwa wananchi wote. Ikiwa ni kwa ajili ya wote, wanaomba TTCL iharakishe kuwapatia huduma hiyo au irejeshe fedha zao ili waweze kutumia huduma mbadala zenye ubora.
 
Walilipia mtandaoni au cash kwenye office husika?
 
Nimesubiri huduma hadi nimekata tamaa, TTCL kunachangamoto.
 
Sijui kwa nini Kigoma huwa nahisi ni sehemu ya nchi ya Burundi.

Ila acha tu na wao wapate huduma za kijamii kutoka serikali ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom