KERO Malalamiko kuhusu kuchelewa kwa matokeo ya wanafunzi waliyozuiliwa kufanya Test 1 katika Chuo cha MUST

KERO Malalamiko kuhusu kuchelewa kwa matokeo ya wanafunzi waliyozuiliwa kufanya Test 1 katika Chuo cha MUST

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tunaomba kufahamu hatima ya wanafunzi waliozuiliwa kufanya Test 1 katika Chuo cha MUST, ambapo mfumo wa matokeo umeonyesha alama za ABSC. Kwa mujibu wa taarifa kutoka chuoni, wanafunzi hao watafanya mtihani huo kipindi cha SUPP mwezi Oktoba.

Changamoto kubwa ipo kwa wanafunzi wa Diploma mwaka wa tatu, ambao wanahitaji matokeo yao kwa ajili ya kuomba masomo ya Shahada (Degree) kupitia TCU. Endapo matokeo yatachelewa, wanafunzi hao wanaweza kukosa dirisha la maombi kutokana na kutokuwa na matokeo kamili, na kulazimika kusubiri hadi mwaka 2027 bila sababu ya msingi.

Tunaomba uongozi wa chuo utoe ufafanuzi na kutafuta suluhisho la haraka ili wanafunzi hao wasipoteze muda wao wa masomo kutokana na kuchelewa kwa mchakato wa matokeo.
 
Back
Top Bottom