DOKEZO Malalamiko kuhusu ukiukwaji wa taratibu katika mgodi uliopo Matanda, Katoro, Geita

DOKEZO Malalamiko kuhusu ukiukwaji wa taratibu katika mgodi uliopo Matanda, Katoro, Geita

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mamlaka husika tunaomba ufanyike uchunguzi kuhusu mgodi unaomilikiwa na Wachina uliopo Mkoa wa Geita, Wilaya ya Katoro, Kijiji cha Matanda, kutokana na madai ya kutokufuata sheria na taratibu za kazi.

Wafanyakazi wanadai kutolipwa stahiki zao, kutokupewa vitendea kazi, pamoja na kutokuwa na mikataba ya ajira. Aidha, inadaiwa kuwa mfanyakazi anapopata ajali akiwa kazini huambiwa aende kutibiwa kwa gharama zake mwenyewe.

Pia kuna wasiwasi kuhusu usalama wa wananchi kutokana na mgodi huo kuwa karibu na makazi ya watu na kutumia vilipuzi (baruti) mara kwa mara.

Tunaomba mamlaka husika zifuatilie suala hili na kuchukua hatua stahiki.

PXL_20260709_114700705.jpg
PXL_20260709_114802239.MP.jpg
 
Back
Top Bottom