Ni nani anayesambaza taarifa binafsi za watumishi, hususan namba zao za simu, kwa taasisi za mikopo? Kumekuwa na hali ya watumishi kupigiwa simu na kutumiwa ujumbe wa matangazo ya mikopo bila kuomba huduma hizo.
Hali hii inazua maswali kuhusu chanzo cha taarifa hizo na namna taasisi hizo zinavyopata namba za simu za watumishi. Je, taarifa hizo zinatolewa na maafisa utumishi au kuna njia nyingine zinazotumika kuzipata?
Nashauri tabia hii ikomeshwe na mamlaka husika zichunguze namna taarifa binafsi za watumishi zinavyopatikana na kutumiwa. Watumishi hawapaswi kusumbuliwa na simu au ujumbe wa matangazo ya mikopo ambayo hawajaomba.
Kukopa ni uamuzi binafsi wa mtumishi, si lazima. Kila mtumishi ana haki ya kuamua kama anahitaji mkopo au la, bila kushinikizwa au kufuatiliwa na taasisi za mikopo.
Tunaomba faragha ya taarifa za watumishi iheshimiwe na hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya usambazaji au matumizi ya taarifa hizo bila ridhaa husika.