Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
KATIBU MKUU
CHAMA CHA MAPINDUZI,
S. L. P. 50
DODOMA
22/07/2020
Ndugu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi,
Dkt Bashiru Ally
YAH: UKIUKWAJI WA TARATIBU ZA UCHAGUZI JIMBO LA HANDENI VIJIJINI
Husika na kichwa cha Habari,
Kwa heshima kubwa kwanza tunakupongeza kwa kusimamia taratibu, kanuni na Sheria zinazotawala katika chama chetu tangu ulipoteuliwa na Mwenyekiti wa Chama Chetu Dkt John Pombe Joseph Magufuli ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ndugu Katibu Mkuu, sisi ni baadhi ya wagombea tuliokuwa tukiomba ridhaa kutoka kwa wanachama wenzetu kupeperusha bendera ya chama kwa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Handeni Vijijini, tunaleta malalamiko kwako kuhusu ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi.
Malalamiko Yetu ya msingi yapo katika maeneo haya ,:
1. Idadi ya wajumbe waliohudhuria kikao cha uchaguzi kuwa tofauti baada ya uchaguzi (waliohudhuria ni 1,070 na waliopiga kura ni 1,203) idadi ya wajumbe wote jimbo zima ni 1,273 kwa maana ya wajumbe 840 kutoka katika matawi, wajumbe 406 kutoka katika Kata na wajumbe 27 wa wilaya. Hapa tunachotaka kusema ni kwamba tuliotangaziwa kuwa wamo ukumbini ni wajumbe 1,070 sasa hao wengine walitoka wapi?
2. Wajumbe kutolewa nje ya ukumbi ili kurahisisha kuingizwa kwa wagombea haramu na kuwatafutia ushindi.
3. Zoezi la uhesabuji wa makaratasi kukosa uwazi kwa sababu wagombea walikosa fursa ya kuhakiki makaratasi ya wagombea wengine ili kujiridhisha ya kwamba makaratasi walipokea ni kweli kura zao.
4. Waandishi wa habari kutolewa nje katika zoezi zima la uchaguzi hii ilitoa mwanya kwa kupitisha mamluki ili kusaidia baadhi ya wagombea.
5. Rushwa ya wazi kwa wagombea,
Mboni Mhita(Na.7)
Charles Sungura(3)
John Salu(25)
Diria Ramadhani(9)
Omary Ngole(10) na
Mkweso Hemedi(32)
Ndugu Katibu Mkuu, kwa barua hii, tunapenda kuleta malalamiko yetu ya namna tulivyoona kukiukwa aidha kwa makusudi au kwa bahati mbaya na viongozi wa wilaya hadi msimamizi wa zoezi zima la uchaguzi.
Kwanza Ndugu Katibu Mkuu, ifahamike wazi kuwa viongozi wa wilaya Mwenyekiti, Katibu wa Wilaya na wajumbe wa Kamati ya Siasa, wagombea wote tulikuwa na haki sawa katika zoezi zima la uchaguzi huo.
Lakini tulishangaa Mwenyekiti Malunda alikuwa akimtembeza kwa wajumbe bila kificho Ndugu Sungura wiki moja kabla ya zoezi la kupiga kura.
Mwenyekiti amempitisha mgombea kwa wajumbe Karibu kata zote 21 za jimbo la Handeni Vijijini, huku akiwaeleza wajumbe kwamba "Zile semina za ujasiriamali mlizokuwa mkizipata bure huku mkilipwa posho, sasa ni wakati wa kulipa fadhila, mchagueni Charles Sungura ili alete semina nyingi, nyingi Zaidi, ".
Lakini pia licha ya kumsaidia kufanya kampeni wana ahadi ya kwamba utakapofika uchaguzi wa UWT Ndugu Sungura amsaidie mke wa mwenyekiti ambaye atagombea ujumbe katika ngazi ya Mkoa.
Lakini pia kuna ushahidi wa wazi kabisa kwamba ndugu Sungura tayari ameanza kumjengea nyumba Mwenyekiti huyo eneo la Mkata.
Mbali na mwenyekiti lakini pia Katibu wa CCM wilaya yetu ya Handeni ndugu Saleh Kikweo amepewa na Mboni Mhita Shilingi milioni 10 na ahadi ya kumsaidia mke wake ambaye anagombea Ubunge wa Viti Maalum mkoa wa Tanga. Mke wa Kikweo hivi sasa ni Katibu wa Siasa na Uenezi wa Mkoa wa Tanga.
Hata katika kikao cha awali kwa wagombea wote kuweka utaratibu wa uchaguzi uliofanyika Julai 18 pale Mkata, Katibu alisema kwamba kutokana na kukosekana kwa fedha za uchaguzi hasa kuwaleta wajumbe eneo la uchaguzi, chakula na kukodisha viti, wagombea wachangie zoezi hilo ambapo Mboni na Sungura walitumia nafasi hiyo kujifanyia kampeni kwa kila mmoja kutoa kiasi kikubwa cha fedha ili kuishawishi meza kuwapa upendeleo wa aina yoyote ile katika zoezi zima la kupiga kura na kuhesabu.
Mboni alitoa Shilingi million 2 na Sungura alitoa Shilingi milioni 1 licha ya kikao kukubaliana kila mgombea achangie chama kiasi cha Sh. 250,000 baada ya upungufu wa bajeti ya wilaya. Tunajua pia Mboni aliwalipia fedha za kuchukua fomu wagombea wenzetu wapatao 15.
Ukiondoa Mazingara hayo Ndugu Katibu Mkuu, tulipoingia ukumbini kabla ya maelekezo yoyote yale tulishangaa wapambe wa Mboni na Sungura walianza kuwapokea wajumbe na kuwapa namba na majina ya kuwapigia kura wakati wagombea wote hawakuwa wakijua namba zao ambazo zilitolewa baadae wakati wagombea, wajumbe na watu wengine waalikwa walipofika ukumbini.
Ndugu Katibu Mkuu hii ilitupa picha kwamba wagombea hao wenzetu Usiku wa kuamkia upigwaji wa kura walikutana na watendaji hao ambao waliwapa karatasi za kupigia kura hivyo wakawapa wapambe wao wawaeleze wajumbe hata kabla hawajafika ukumbini.
Lakini pia wagombea wanne akiwemo Josephine Mgaza jina lake lilikosewa kusudi katika karatasi ya kupigia kura lakini pia katika beji walizopewa wagombea zilizoandikwa majina yao.
Badala ya kuandikwa Josephine Mgaza, jina lake liliandikwa JOSEPHINE MBEZI kusudi kama njia mojawapo ya kumdhoofisha au kuwachanganya wajumbe ambao walikuwa wakimtambua kwa jina hilo.
Ndugu Katibu Mkuu, pamoja na kasoro hizo lakini pia karatasi za kura ambazo awali tulikubaliana ziwe na picha zetu wagombea hazikuwekwa na hivyo kuharibu kabisa zoezi hilo kwasababu baadhi ya wajumbe waliwatambua wagombea kwa sura.
Karatasi ya kupigia kura yenye majina 50 kukosa picha kuliwachanganya wajumbe, hili lilifanywa kusudi kabisa na viongozi wa wilaya kwa Maslahi ya kuwabeba wagombea wao.
Ndugu Katibu Mkuu, suala jingine hatukuwa na imani na msimamizi wa uchaguzi Ndugu Zawadi Nyambo ambaye ni Katibu wa UVCCM Mkoa wa Tanga, kwani licha ya kupewa Shilingi Laki Tano na Mboni lakini pia alilipiwa hotel ya KN pale Mkata.
Mwenyekiti wa CCM, Rais wetu John Magufuli kabla ya kuanza kwa zoezi la kura za maoni alisema kwamba zoezi hilo litaendeshwa kwa uwazi na waandishi wa habari watarusha live bila kificho, lakini cha kushangaza katika uchaguzi wetu hali imekuwa tofauti.
Mara baada ya wajumbe wote kupiga kura msimamizi wa uchaguzi Ndugu Nyambo, aliwatoa wajumbe wote pamoja na waandishi wa habari kisha wagombea wote tukakaa pamoja akaanza kutugawia kura za kila mmoja.
Ndugu Katibu Mkuu, tukiri kabisa kama sehemu ambayo tumepigwa bao ilikuwa ni katika zoezi hili ambalo asilimia 100 tulipigwa hapo.
Ni hivi kwanza kwa majira yale usiku ule giza ama taa hazikuwa zikiwaka vizuri lakini pia Ndugu Nyambo alikuwa akiita Mboni ile kura hakuionesha kwa wagombea wote aliikunja na kumpa hivyo hivyo alikuwa akiwapa wagombea hao kiasi kwamba tukaona tumepigwa.
Na mara kwa mara Mboni alikuwa akitoka nje kila alipokuwa anakabiliwa na uhaba wa kura akirudi kura anapewa yeye. Lakini pia wagombea wote tulilazimishwa tusaini kukubali matokeo hata pale tulipoonesha wasiwasi.
tunahisi kura nyingi hasa za Kanyika na Mgaza amepewa Mboni maana kwa Mazingara aliyoyaweka ya Jimbo wananchi walishangaa Mboni kushika nafasi ya pili kiukweli kama angepata kura katika uchaguzi ule basi angestahili kupata kura 50.
Baada ya zoezi kiukweli lilituchanganya hasa baada ya Usiku majira ya saa nane msimamizi Ndugu Nyambo aliingia na maboksi yenye kura katika hotel ya MACHETO na kisha kujifungia humo ndani. Tunahisi alikuwa na kura nyingine ambazo alihalalalisha matokeo yale.
Kwa vile katika hotel ile mmoja ya wagombea ambaye alilala katika hotel hiyo alipoona hali ile na Mazingara yenye kumtia mashaka alimpigia simu Mkuu wa Wilaya, Ofisa Usalama pamoja na watu wa Takukuru kutaka waje wawatoe wasiwasi kuhusu kura kuhifadhiwa hotelini.
Viongozi hao waliaahidi wangefuatilia ili watutoe katika Mashaka hayo lakini hadi Usiku hakukuwa na kiongozi aliyefika na kura zikachukuliwa huo Usiku zikapelaka Ofisi ya CCM baada ya kumalizika uchaguzi wa Handeni Mjini ambako pia Ndugu Nyambo alisimamia uchaguzi huo.
Mwisho Ndugu Katibu Mkuu, tunaomba zoezi hilo lirejewe upya kwasababu hatuamini kwamba walioshika nafasi za juu walipata kihalali kura hizo. Hivyo turudie tena ili tumpate mwakilishi halali atakaye peperusha Bendera ya chama chetu Handeni Vijijini.
NI SISI WAGOMBEA UBUNGE JIMBO LA HANDENI VIJIJINI.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI