DOKEZO Malalamiko ya mkataba wa DP World yapelekwe CCM, Rais Samia hana makosa sababu anatekeleza sera za chama chake

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mr Why

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2019
Posts
2,235
Reaction score
4,252
Ndugu zangu Wananchi, kuna jambo tunasahau kuhusiana na mkataba wa DP World. Malalamiko ya mkataba huo yamekuwa mengi sana lakini tatizo letu wananchi tumeshindwa kujua kuwa Rais Samia Suluhu Hassan hapaswi kulaumiwa hata kidogo, ni Rais msafi na mcha Mungu.

Malalamiko yanayohusiana na mkataba wa DP World yapelekwe CCM kwasababu Rais anatekeleza sera za chama chake.

Rais yupo chini ya chama chake hivyobasi jambo lolote analofanya linatokana na kutekeleza sera za chama chake na sio yeye binafsi.

Raisi ndani ya chama ni sawa na mtumishi yeye anafanya yale yote anayoagizwa na chama chake ama kwa maana rahisi mwajiri wake.

Kitendo cha kumlaumu Rais Samia Suluhu Hassan ni kitendo cha unyanyasaji wa hali ya juu na sote tunapaswa kumtaka radhi kwasababu tunamuonea.
 
Mbona kama ni pongezi anapongezwa yeye tu?
 
Mtatajana tu na bado....
 
Ipo soma vizuri,kama unabisha kawaulize wabunge wenu walipiga kura ya Ndiyooooo

Raisi ccm
Makamu ccm
Waziri mkuu ccm
Spika ccm
Mawaziri wote ccm
Wabunge wote ccm

Mnachomokaje kwenye hili ccm?
Raisi kaajiriwa na CCM, muulizeni makamu mwenyekiti wa CCM kuhusu DP World
 
Jiheshimu,

Ilani ya 2020/2025 alikabidhiwa Magu.

Hakuna mahala ilani imesema bandari zigaiwe Bure Kwa mwarabu bila UKOMO.

Hili kajituma mwenyewe,

Ni lake hili mwenyewe, akinywee tu hicho kikombe, hamna namna.
 
Jiheshimu,

Ilani ya 2020/2025 alikabidhiwa Magu.

Hakuna mahala ilani imesema bandari zigaiwe Bure Kwa mwarabu bila UKOMO.

Hili kajituma mwenyewe,

Ni lake hili mwenyewe, akinywee tu hicho kikombe, hamna namna.
Kumbuka hawezi fanya jambo kama hajaruhisiwa na CCM
 
Kumbuka hawezi fanya jambo kama hajaruhisiwa na CCM
Magu mwenyewe akiwa hai alisema nanukuu " Ni MPUMBAVU tu ndo anaweza kukubali masharti ya mkataba wa bagamoyo port"

Kama Magu alikataanmkataba wa bagamoyo, huu wa kimangungo hata asingediriki.

Amejituma,

CCMM, Wala ilani haikumtuma.
 
Je mliwasiliana na makamu mwenyekiti wa CCM?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…