KERO Malalamiko ya Nyongeza ya Ada ya EXTENSION kwa Wanafunzi wa Shahada ya Umahiri (MASTERS) – UDSM

KERO Malalamiko ya Nyongeza ya Ada ya EXTENSION kwa Wanafunzi wa Shahada ya Umahiri (MASTERS) – UDSM

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
BARUA YA WAZI KWA WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA NA TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU)

KUHUSU MALALAMIKO YA NYONGEZA YA ADA YA EXTENSION KWA WANAFUNZI WA SHAHADA YA UMAHIRI (MASTERS) – CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

YAH: MALALAMIKO KUHUSU NYONGEZA YA ADA YA EXTENSION KWA WANAFUNZI WA SHAHADA YA UMAHIRI (MASTERS) – CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

Kwa heshima na taadhima, napenda kuwasilisha malalamiko yangu pamoja na ya wanafunzi wenzangu wa shahada ya umahiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuhusu ongezeko la ada ya extension (kuongeza muda wa masomo) lililotangazwa June 2024 na kuanza kutekelezwa hivi karibuni.

Ongezeko hili la ada ya extension limekuwa kubwa na la ghafla, bila maandalizi ya kutosha kwa wanafunzi wengi. Ikumbukwe kuwa wanafunzi wengi wanaolazimika kuomba extension hawafanyi hivyo kwa hiari, bali kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo ucheleweshaji wa usimamizi wa tafiti, upatikanaji wa wasimamizi (supervisors), taratibu za kitaasisi, pamoja na majukumu ya kikazi na kifamilia.

Hivyo basi, kuongeza ada hii kwa kiwango kikubwa kinazidi kuwaumiza wanafunzi ambao tayari wako katika mazingira magumu ya kukamilisha masomo yao. Hatua hii imesababisha/ inaweza kusababisha baadhi ya wanafunzi kushindwa kabisa kuhitimu, hali ambayo siyo tu inaathiri maisha yao binafsi bali pia maendeleo ya rasilimali watu ya taifa.

Kutokana na hali hiyo, tunaomba yafuatayo yazingatiwe:
1. Kupitiwa upya kwa kiwango cha ada ya extension ili kiwe rafiki na kinachomudu hali halisi ya wanafunzi.
2. Kusitishwa kwa utekelezaji wa ongezeko hilo hadi hapo tathmini na majadiliano ya kina yatakapofanyika na wadau.
3. Kuwepo kwa utaratibu wa kuzingatia sababu za mwanafunzi kuomba extension kabla ya kutozwa ada kubwa.
4. Serikali kupitia Wizara husika na TCU kuingilia kati ili kuhakikisha haki na ustawi wa wanafunzi unalindwa.
Tunaamini kuwa dhamira ya serikali ni kuhakikisha elimu ya juu inakuwa bora, jumuishi na inayofikika kwa wote. Hivyo, tunategemea malalamiko haya yatapokelewa na kufanyiwa kazi kwa haraka ili kulinda ndoto na mustakabali wa wanafunzi wengi wa Kitanzania.

Master student Udsm
 
Pole sana.
Na mwenzako wa Udom naye ametoka kulalamika muda si mrefu. Na wote shida zenu zinafanana!
 
Back
Top Bottom