Malalamiko ya Tozo za miamala na kodi za majengo kupitia Luku yamepungua, safi sana

Watanzania wana imani kubwa na Rais wetu . Matumaini makubwa yanaonekana hata kwenye nyuso zao
 
Ngozi nyeusi ndiyo maana yule Jamaa wa us alitutukana, hitla alitalia kuiondoa kabisa hii ngozi duniani! Kumbe ni kweli hatuna faida tunamaliza hewa ya Mwenyezi bure! Poor afr.
Si kweli kuwa Hitler alitaka kutokomeza rangi Nyeusi, kwani alihitaji watumwa wamfanyie kazi. Ukielewa maana ya nguvu kazi utaelewa kila mtu na kazi yake na pahala anapostahili kwa maoni ya mtumiaji.

Nakushauri kasome tena kitabu alichokiandika Hitler na ukielewe " The strugle au My camp"
 
Je pesa inayokusanywa nyingine kazi yake nini? au ni kulipa mishahara na posho?
Mahitaji yetu ni mengi na hayaishii tu kujenga madarasa na zahanati. Huko ndio kwenye kipau mbele.

Kuna barabara vijijini, kilimo, upimaji wa ardhi, ufufuaji/uendelezaji wa viwanda, mikopo kwa wanafunzi wa chuo kikuu, Usafiri Dar aka mwendokasi na....na....na

Hivyon ni pole pole huko kote serikali inakuja lakini katika wakati muafaka.
 
Miaka yote mlikuwa wapi?
 
Mitanzania ni miwatu ya fikra fupi, mingi inapelekeshwa na story zinazotrend mitandaoni,
 
Miaka yote mlikuwa wapi?
Muhimu kuanza, huko nyuma tulichelewa na ujamaa. Anyway kushusha gunia la lawama kwa watangulizi hakutatusaidia, la muhimu tuanze leo... Na hivyo ndivyo Rais anafanya.

Hakuna kutekana, wala kubambikiana makodi ya kifichoni, awamu hii kodi zote hadharani... Tufanyeni biashara, nyumbani kumenoga.....
 
Tatizo lililopo ni gharama za uendeshaji wa serikali kuwa kubwa, mfano halmashauri kuna DC, DAS, DED, Mbunge na Mwenyekiti wa halmashauri bado wakuu wa idara na vitengo, hawa wote wanalipwa mamilioni ya pesa pamoja na posho zao. tupunguze matumizi
 
Matumizi mengine ni ya kijinga sn mfano kuna TANROAD na TARURA hawa wote kazi yao ni moja barabara, hapo tunaongeza gharama kubwa za uendeshaji.
 
Mitanzania ni miwatu ya fikra fupi, mingi inapelekeshwa na story zinazotrend mitandaoni,
Watanzania ni watu poa sana, huko nje kila mtu anataka kuishi Tanzania. Si unaona mwenyewe Wa - Ethiopia wanavyokimbilia bongo pamoja na kuwa nchi yao ni kubwa kuliko yetu. Sijawasema akina .................... Jaribu tu kuachia mipaka uone wakenya na majirani watavyofurika TZ.
 
Matumizi mengine ni ya kijinga sn mfano kuna TANROAD na TARURA hawa wote kazi yao ni moja barabara, hapo tunaongeza gharama kubwa za uendeshaji.
Mmmmmm, mwenzangu hii shughuli ya barabara iache tu maana ni kubwa mno. Hivyo inahitaji mgawanyo mkubwa sana. Mi singeshangaa kama kungeanzishwa kitengo kingine cha kushughulikia madaraja tu. Mmmmm hapa paache tu.

Ungekuwa unafanya kazi huko wala usingesema, maana walivyobusy hao vijana ni kuwaonea huruma tu. Na bado inaonekana kama wafanyacho ni tone la maji katika bahari.
 
Kwanini hao watumishi wa TARURA wasiwe sehemu ya staff wa TANROAD? kumbuka hapo kuna ofisi, mkuu taasisi, na matumizi mengine ambayo siyo ya lazima
 
Kwanini hao watumishi wa TARURA wasiwe sehemu ya staff wa TANROAD? kumbuka hapo kuna ofisi, mkuu taasisi, na matumizi mengine ambayo siyo ya lazima
Ni habari ndefu ya kuanzishwa TARURA, ila ilijikita sana katika sababu za kiutendaji. Kiufupi hao wafanyakzi wa TARURA walikuwepo hata kabla ya jina TARURA kuanzishwa. Kilichofanyika ni hilo group la kitaalamu kulipa nguvu zaidi ya kitaalam na kuitenga toka kwenye maamuzi ya kisiasa (madiwani & company). Hii imewaletea hawa wataalamu kupumua sana na kuwa na ufanisi mzuri zaidi. Kimsingi ilikuwa ni hatua muhimu sana.

Kimgawanyo na uwajibikaji, TANROAD na TARURA tofauti kabisa, kwani kama nilivyosema huko awali kuwa wafanyazazi na majukumu yao TARURA yalikuwepo hata kabla ya kuanzishwa hii TARURA. Ukianisha majukumu yao ndio utaona utafauti wao.
 
Kwani wangetoka halmashauri wakaenda moja kwa moja TANROAD kungekuwa na tatizo gani?
 
Hebu tafuta hata gemu la nyoka ucheze kwenye sim yako. Huna hoja ya msingi, usitupandishe khasira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…