DOKEZO Malalamiko ya wafanyakazi wa Bandari waliosimamishwa kazi kwa tuhuma za kushindwa kukusanya tozo za wharfage katika bandari kavu

DOKEZO Malalamiko ya wafanyakazi wa Bandari waliosimamishwa kazi kwa tuhuma za kushindwa kukusanya tozo za wharfage katika bandari kavu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Habari wanajamvi wote wa Jamii Forums,

Naomba kushea nao maumivu waliyonayo baadhi ya waliokuwa wafanyakazi wa Mamlaka ya BAndari Tanzania (TPA) ambao walikutwa na kadhia ya kusimamishwa kazi kwa tuhuma za kushindwa kukusanya tozo za wharfage katika bandari kavu.

Wafanyakazi hawa walisimamishwa na baadaye wakaundiwa tume kwa ajili ya kutafuta ukweli wa hizi tuhuma kupitia tume ya Mwenyekiti NURU MUHANDO ilifanyika kazi zake katika ukumbi wa chuo cha Bandari Tandika. Kabla ya tume hii kukabidhi ripoti Bandari aliyekuwa mwenyekiti wa tume hiyo bibi NURU MUHANDO aliajiriwa kama Mkurugenzi wa Fedha (DF) na baada ya kukabidhi hiyo ripoti wafanyakazi wote ambao waliwahoji katika sakata hili waliwafukuza bila ya hata kuwasomea kile kilichopatikana katika tuhuma hizo wala kuwapeleka katika kamati ya ajira nidhamu ya Bandari maarufu kama PAC.

Wakati haya yote yakifanyika wafanyakazi hao walikuwa wakiripoti katika ofisi ya ZCO kituo cha polisi cha kati(Central) kwa ajili ya mahojiano. Mnamo mwezi December 2016 wafanyakazi hao qalifukuzqwa rasmi ajira huku wakiwa wanaaendelea na uchunguzi katika ofisi ya ZCO mpaka mwaka December 2019 baadhi yao walifunguliwa kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji Fedha ambazo ziliwafanya wakae gerezani mpaka pale walipoondolewa shtaka la Utakatishaji Fedha ambalo halina dhamana na kuanza kupata dhamana na kausikiliza kesi wakiwa wako nje. Kesi hizo kwa sasa zote zimeondolewa na DPP mahakamani na watuhumiwa hao wako huru .

Kesi hii pia ilijumuisha wafanyakazi wa benki ya CRDB katika baadhi ya bandari kavu ila wafanyakazi wote wa CRDB walikuwa wako kazini na wanahudumiwa na mwajiri wao kuanzia mishahara yao mpaka kulipia mwanasheria kwa ajli ya utetezi wa mashauri hayo. Hali ilikuwa tofauti kwa wafanyakazi wa Bandari kwani wengi walikuwa wameshafukuzwa kasoro wafanyakazi wawili tu na hawa walikuwa wakihudumiwa na Bandari kama kawaida huku wengine wakiwa wanahudumiwa na familia zao.

Kibaya zaidi hawa wafanyakazi wawili baada ya kutoka walirudishwa kazini na mpaka sasa wanafanya kazi ila wengine wote pamoja na kuwa kesi zao zimefutwa kama hawa wengine ila Mwajiri amekataa kuwarudisha na hata walipomfata kwa ajili ya kuliweka sawa hili jambo lakini alikataa kwa kigezo kama mlishafukuzwa hamna chenu kabisa.

Kwa kweli haya maamuzi ni mabaya sana na yanatuumiza hata sisi wafanyakazi wengine a mbao bado tuko kazini kwani tunajisikia vibaya sana kwa maamuzi haya hasa tunapowaona hawa wafanyakazi wili ambao walikuwa jela na wenzao wakiwa wanaendelea na kazi huku wengine wakiendelea kusalia nyumbani. Binafsi jambo hili halileti afya kabisa katiika machoo ya sheria kwani tunaamini kwamba Sheria ya Utumishi ya Umma ni moja kwa watumishi wote wa Umma sasa inakuwaje kunakuwa na double standards kama hivi, kidogo ingeeleweka kama watuhumiwa wote wangeondolewa ila sio wengine wameondoůewa na wengine wako kazini.

Kuna baadhi ya wafanyakazi wa NIDA ambao nao walikuwa na tuhuma na kesi yao iko mahakamani baada yakufutwa kwa kesi hiyo wafanyakazi hao walirudishwa kazini na wanafanya kazi mpaka leo.Sasa shaka iliyoko ni kuwa kwa nini hawa watuhumiwa ambao wameondolewa kesi na DPP nao wasirudishwe kama atumishi wa idara nyengine za serikali

Kwa sasa wanaisha maisha magumu sana na hawna hatia yoyote ndo mana wamefutiwa kesi na DPP. Hili jambo kwa kweli linavunjisha moyo sana na linarudisha ari ya kazi.

Sisi wafanyakazi wa Bandari tunaomba hawa wafanyakazi wenzetu wasaidiwe kama Bandari hawataki basi muwahamishie idara nyingine za serikali kama ilivyofanyika kwa wafanyakazi wa idara nyengine

UMOJA WA WAFANYAKAZI WA BANDARI
BANDARI YA DAR ES SALAAM
PO BOX 9187
DAR ES SALAAM
 
Pole sana, kiukweli ukiwa mgeni mtaani ni pagumu!! Pambaneni, hio isije ikawa ndo tabia zao.... Mkiona wenzenu wanapitia Hali ngumu Kama hio (shirikianeni, huwezi jua wanaweza wakaifanya kuwa tabia Yao) na wafanyakz wengi wakaanza kupitia situation Kama hio..

Mkimchekea nyani mtavuna mabua
 
Back
Top Bottom