@nacteHuyo aliyefanya hayo maamuzi, Mungu amuangalie huko alipo. Na aliyevujisha hiyo mitihani huko juu, Mungu amshughulikie, kosa wanafanya wenye vyeo, adhabu mnawapa watoto.
Watoto wanapataje mitihani bila juu kuwa na leakage, mlisema watu watawajibishwa, sijasikia mtu juu huko juu kuwajibishwa.
Wizara ya afya, Nacte mjiangalie na hivyo vyeo.
Hamuwez tesa watoto wakae nyumban mwaka mzima (miez 8) ndio mtu akafanye sup.
Stress ya Kwanza mmewapa ambayo adhabu ya kurudia mitihani ni sawa kabisa.
Sasa hivi hii tuiteje? Kukatisha tamaa watoto wasisome ama nini?
Hivi katika familia zenu hakuna watoto? Au nyie binafsi hamna watoto?
Mnawapa stress watoto Sana, masomo magumu, bado tena mnawakalisha nyumbani miezi 8, mm naita mwaka mzima sabab watoto toka mwaka Jana September wapo nyumbani,. December wamerudia.
Mmetoa matokeo, Sasa mnawaweka miezi 8.
Hivi akili za mtu mzima kweli hizi? Sup gani miezi 8? Ktk Sheria ipi?
Jipangeni huko juu.
Wizara ya Afya Tanzania