Malamba Mawili, Msikitini: Mtoto ajinyonga hadi kufa, inadaiwa alikuwa anasoma Malamba Mawili Darasa la 6

Malamba Mawili, Msikitini: Mtoto ajinyonga hadi kufa, inadaiwa alikuwa anasoma Malamba Mawili Darasa la 6

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Mtoto mdogo anayedaiwa kuwa alikuwa ni mwanafunzi wa darasa la 6 Shule ya msingi Malamba Mawili amejinyonga eneo la Msikitini.

Mwili huo umegunduliwa ukining'inia chini ya mti mbele ya nyumba ya mtu ambaye inadaiwa watu hawakai hapo.

Polisi wamefika eneo la tukio wamechukua mwili wa marehemu, pamoja na mtoto aliyegundua mwili huo.

20240522_083516.jpg

20240522_083703.jpg

Picha: Baadhi ya watu wakikata mti muda mfupi baada ya polisi kuchukua mwili na kuondoka​
 
Mtoto mdogo anayedaiwa kuwa ni mwanafunzi wa darasa la 6 Shule ya msingi Malamba Mawili amejinyonga eneo la Msikitini.

Mwili huo umegunduliwa ukining'inia chini ya mti mbele ya nyumba ya mtu ambaye inadaiwa watu hawakai hapo.

Polisi wamefika enwo la tukio wamechukua mwili wa marehemu, pamoja na mtoto aliyegundua mwili huo.
View attachment 2996476
Picha: Baadhi ya watu wakikata mti muda mfupi baada ya polisi kuchukua mwili na kuondoka
Hawa watoto siku hizi wamekuwa wakituachia simanzi sana sisi wazazi.

Wamepatwa na nini?

Mwingine juzi kanyanganywa simu na kaka yake akajitundika.

Mwingine kapigwa shuleni na Mwl kajimaliza.

Yaani hawawezi kuhandle any kind of stress
 
Uchunguzi ufanyike kwa kina, inawezekana kabisa kanyongwa.
Jeshi la polisi lifanye uchunguzi.
Pole sana kwa wazazi.

Wazazi nawaomba tuongeze umakini sana sana kwa watoto wetu.
wabakaji na walawiti wanaweza kabisa kufanya unyama huo.
 
Mwili huo umegunduliwa ukining'inia chini ya mti mbele ya nyumba ya mtu ambaye inadaiwa "watu hawakai hapo".
Yani mtu kajenga nyumba halaf kaitelekeza, haishi hapo. Na ndio hapo hapo alipokutwa mtoto kajinyonga 🤔

Ngoja tuwaachie polisi wafanye uchunguzi wao...

Pole kwa waliopoteza mtoto.
 
Back
Top Bottom