Malaria na Ukimwi, ni mapambano kweli au Biashara ya Wakubwa?

Mwanahisa

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2012
Posts
1,382
Reaction score
513
Hali hii imekua ikinitatiza kwa muda sasa, jinsi mataifa masikini na yenye hali duni yakiwekwa kwenye kivuli cha maradhi. Kubwa kuliko yote ni hili gonjwa la malaria, na pengine Ukimwi pia jinsi muonekano wake ulivyo kimapambano zaidi kama adui wa vita wakati biashara ya tafiti, kinga na madawa ikishamiri zaidi duniani.
Nifunguliwe macho na mimi nione hicho nisichokiona, kwani wakati fulani tulipotajiwa MAADUI zetu wakuu watatu (3) adui maradhi alikuepo, ni wazi kabisa maradhi yanachangia kupunguza nguvu kazi ya Taifa lolote lile duniani, na baadae pato na uchumi kwa ujumla unaathirika.

Ni nani kati yetu asiyejua mazalia ya mbu jike ambaye ndie anaebeba na kuambukiza wadudu wa Malaria? Labda kwa karne hii ya 21 mapambano ya binadamu na utashi wake dhidi ya mbu ni zaidi ya Chandarua. Miaka ya hivi karibuni alikuja Raisi wa taifa kubwa na lenye nguvu ya kiuchumi duniani, moja ya kazi aliyoifanya akiwa hapa kwetu ni uzinduzi wa kiwanda cha ufumaji wa vyandarua, je isingekua vizuri zaidi akatusaidia Maabara, na mitambo ya kisasa zaidi pia wataalam kwa ajili yakupambana na mifumo ya mazalia ya mbu? Je isingewezekana kikosi kazi na ndege au helkopta zakunyunyiza dawa katika mazalia haya na sio vyandarua ambavyo ni nyenzo duni sana yakupambana na adui Malaria?

Labda mawazo haya ndio yangeharibu biashara ya madawa na pengine mfumo mzima wa jinsi mataifa yenye nguvu yataendelea kuyakandamiza mataifa duni. Tumebaki kua kama panya wa majaribio wa kila dawa mpya itakayo ingia sokoni na itakayotoboa mifuko yetu ili wakubwa washibe kwa dhiki inayotukabili. Kipekee nafikiri chandarua ni uzio wa kifikra hata dhidi ya mdudu asiyeweza kupenya kwenye tundu, ambaye hana mbinu wala utashi tulio nao wanadamu. Nisaidieni wadau nataka kufunguka macho.......!
 
ni biashara ya wakubwa kwa asilimia (((99)))
 
Naanza kufunguka macho Mkuu, niondoe hizi tongotongo tafadhali, maana utasikia mapambano dhidi ya gonjwa fulani lakini ukiangalia kiundani ni mwanya wa biashara unatengenezwa,......!
Hii inanipa shaka kwa ushamiri wa Pharmaceutical Industries, kama kweli ni kupambana au ni kutengeneza hela kwa watu fulani.!
 
Hali hii imekua ikinitatiza kwa muda sasa, jinsi mataifa masikini na yenye hali duni yakiwekwa kwenye kivuli cha maradhi. Kubwa kuliko yote ni hili gonjwa la malaria, na pengine Ukimwi pia jinsi muonekano wake ulivyo kimapambano zaidi kama adui wa vita wakati biashara ya tafiti, kinga na madawa ikishamiri zaidi duniani.
Nifunguliwe macho na mimi nione hicho nisichokiona, kwani wakati fulani tulipotajiwa MAADUI zetu wakuu watatu (3) adui maradhi alikuepo, ni wazi kabisa maradhi yanachangia kupunguza nguvu kazi ya Taifa lolote lile duniani, na baadae pato na uchumi kwa ujumla unaathirika.

Ni nani kati yetu asiyejua mazalia ya mbu jike ambaye ndie anaebeba na kuambukiza wadudu wa Malaria? Labda kwa karne hii ya 21 mapambano ya binadamu na utashi wake dhidi ya mbu ni zaidi ya Chandarua. Miaka ya hivi karibuni alikuja Raisi wa taifa kubwa na lenye nguvu ya kiuchumi duniani, moja ya kazi aliyoifanya akiwa hapa kwetu ni uzinduzi wa kiwanda cha ufumaji wa vyandarua, je isingekua vizuri zaidi akatusaidia Maabara, na mitambo ya kisasa zaidi pia wataalam kwa ajili yakupambana na mifumo ya mazalia ya mbu? Je isingewezekana kikosi kazi na ndege au helkopta zakunyunyiza dawa katika mazalia haya na sio vyandarua ambavyo ni nyenzo duni sana yakupambana na adui Malaria?

Labda mawazo haya ndio yangeharibu biashara ya madawa na pengine mfumo mzima wa jinsi mataifa yenye nguvu yataendelea kuyakandamiza mataifa duni. Tumebaki kua kama panya wa majaribio wa kila dawa mpya itakayo ingia sokoni na itakayotoboa mifuko yetu ili wakubwa washibe kwa dhiki inayotukabili. Kipekee nafikiri chandarua ni uzio wa kifikra hata dhidi ya mdudu asiyeweza kupenya kwenye tundu, ambaye hana mbinu wala utashi tulio nao wanadamu. Nisaidieni wadau nataka kufunguka macho.......!

Nimeipenda hii thread sana kwa vile imenikumbusha mbali. Ni hivi ndugu yangu: Ugonjwa wa Malaria hauwezi kuisha kwa kutumia vyandarua, japo kisayansi, vyandarua vinapunguza maambukizi ya malaria kwa asilimia 35 hivi. Malaria ni ugonjwa wa Maskini. Leo hii, tukiangalia vipimo vya malaria kwa watu wa kule Mtogole, Buguruni kwa Mnyamani, Yembe Mbuzi, Manzense tukilinganisha na vimpimo vya Oyetsrbay, Masaki, Mbezi nk, utagundua kwamba ukichukua vipimo vya watu 10, wale maeneo duni ratio ni 6;1 (6 ni wale wa huko Manzense nk, 1 ni huko Masaki). Why? Nyumba nzuri pia zinachangia kupunguza malaria.
Hapo nyuma, kulikuwa na mradi wa JAICA ambao ulilenga kuzibua mifereji. Mradi huu ulifanikiwa sana ila wengi hawakufurahishwa. Pia, hata kwenye makabrasha ya wizara hawana hata kumbukumbu za mradi huu wenye mafanikio makubwa sana. Kumbukumbu walizonazo ni za vyandarua tu.
Ukija suala la dawa napo kuna walakini mkubwa katika kusambaza dawa hizi. Wakati fulani, dawa nyingi sana zili expire zikiwa hapa Dar wakati vijijini watu walikua wanakufa! Hizi zote ni mbinu za watu kuendelea kula tu.
 
Mkuu, naendelea kufunguka macho, swala kubwa hapa ni technology yakupambana na huyu mdudu ambae ndie mzizi mkuu wa hili gonjwa. Sasa ikiwa dunia imeendelea katika sekta hii ya sayansi mpaka kuna vitu kama biological weapons, wadudu wanapandikizwa sumu ili wakikung'ata kazi kwisha. Je mbu jike amashindwa kudhibitiwa kwa njia za vinasaba (DNA) au technolojia yoyote ile ya kibailojia? Au ndio biashara ya wakubwa itaingia mchanga?
 
Hali hii imekua ikinitatiza kwa muda sasa, jinsi mataifa masikini na yenye hali duni yakiwekwa kwenye kivuli cha maradhi. Kubwa kuliko yote ni hili gonjwa la malaria, na pengine Ukimwi pia jinsi muonekano wake ulivyo kimapambano zaidi kama adui wa vita wakati biashara ya tafiti, kinga na madawa ikishamiri zaidi duniani.
Nifunguliwe macho na mimi nione hicho nisichokiona, kwani wakati fulani tulipotajiwa MAADUI zetu wakuu watatu (3) adui maradhi alikuepo, ni wazi kabisa maradhi yanachangia kupunguza nguvu kazi ya Taifa lolote lile duniani, na baadae pato na uchumi kwa ujumla unaathirika.

Ni nani kati yetu asiyejua mazalia ya mbu jike ambaye ndie anaebeba na kuambukiza wadudu wa Malaria? Labda kwa karne hii ya 21 mapambano ya binadamu na utashi wake dhidi ya mbu ni zaidi ya Chandarua. Miaka ya hivi karibuni alikuja Raisi wa taifa kubwa na lenye nguvu ya kiuchumi duniani, moja ya kazi aliyoifanya akiwa hapa kwetu ni uzinduzi wa kiwanda cha ufumaji wa vyandarua, je isingekua vizuri zaidi akatusaidia Maabara, na mitambo ya kisasa zaidi pia wataalam kwa ajili yakupambana na mifumo ya mazalia ya mbu? Je isingewezekana kikosi kazi na ndege au helkopta zakunyunyiza dawa katika mazalia haya na sio vyandarua ambavyo ni nyenzo duni sana yakupambana na adui Malaria?

Labda mawazo haya ndio yangeharibu biashara ya madawa na pengine mfumo mzima wa jinsi mataifa yenye nguvu yataendelea kuyakandamiza mataifa duni. Tumebaki kua kama panya wa majaribio wa kila dawa mpya itakayo ingia sokoni na itakayotoboa mifuko yetu ili wakubwa washibe kwa dhiki inayotukabili. Kipekee nafikiri chandarua ni uzio wa kifikra hata dhidi ya mdudu asiyeweza kupenya kwenye tundu, ambaye hana mbinu wala utashi tulio nao wanadamu. Nisaidieni wadau nataka kufunguka macho.......!

wee mtanzania unaakili sana.
Hayo yote ni ya kweli kabisa kama wangekuwa na nia ya dhati wangetumia resource zao kutuondolea huyu mdudu Plasmodia na Anofelensi
 
Hakuna mwenye nia Mkuu, ndio maana hata sisi walengwa wa vyandarua tumeamua kuvitumia kujengea mabanda ya kuku, huwezi jikinga na mbu ukiwa kitandani tu, au tuvae vyandarua kazini usiku pia? Huku ni kudumaza fikra za watu tu...! Au sayansi ya mbu jike anaebeba hao wadudu ni ngumu kuliko kupeleka roketi mwezini?
 
Back
Top Bottom