Mwanahisa
JF-Expert Member
- Jun 29, 2012
- 1,382
- 513
Hali hii imekua ikinitatiza kwa muda sasa, jinsi mataifa masikini na yenye hali duni yakiwekwa kwenye kivuli cha maradhi. Kubwa kuliko yote ni hili gonjwa la malaria, na pengine Ukimwi pia jinsi muonekano wake ulivyo kimapambano zaidi kama adui wa vita wakati biashara ya tafiti, kinga na madawa ikishamiri zaidi duniani.
Nifunguliwe macho na mimi nione hicho nisichokiona, kwani wakati fulani tulipotajiwa MAADUI zetu wakuu watatu (3) adui maradhi alikuepo, ni wazi kabisa maradhi yanachangia kupunguza nguvu kazi ya Taifa lolote lile duniani, na baadae pato na uchumi kwa ujumla unaathirika.
Ni nani kati yetu asiyejua mazalia ya mbu jike ambaye ndie anaebeba na kuambukiza wadudu wa Malaria? Labda kwa karne hii ya 21 mapambano ya binadamu na utashi wake dhidi ya mbu ni zaidi ya Chandarua. Miaka ya hivi karibuni alikuja Raisi wa taifa kubwa na lenye nguvu ya kiuchumi duniani, moja ya kazi aliyoifanya akiwa hapa kwetu ni uzinduzi wa kiwanda cha ufumaji wa vyandarua, je isingekua vizuri zaidi akatusaidia Maabara, na mitambo ya kisasa zaidi pia wataalam kwa ajili yakupambana na mifumo ya mazalia ya mbu? Je isingewezekana kikosi kazi na ndege au helkopta zakunyunyiza dawa katika mazalia haya na sio vyandarua ambavyo ni nyenzo duni sana yakupambana na adui Malaria?
Labda mawazo haya ndio yangeharibu biashara ya madawa na pengine mfumo mzima wa jinsi mataifa yenye nguvu yataendelea kuyakandamiza mataifa duni. Tumebaki kua kama panya wa majaribio wa kila dawa mpya itakayo ingia sokoni na itakayotoboa mifuko yetu ili wakubwa washibe kwa dhiki inayotukabili. Kipekee nafikiri chandarua ni uzio wa kifikra hata dhidi ya mdudu asiyeweza kupenya kwenye tundu, ambaye hana mbinu wala utashi tulio nao wanadamu. Nisaidieni wadau nataka kufunguka macho.......!