#COVID19 Malaria ndio inaua zaidi kuliko COVID19, mbona nguvu nyingi ziko kwenye COVID19

#COVID19 Malaria ndio inaua zaidi kuliko COVID19, mbona nguvu nyingi ziko kwenye COVID19

Randy orton

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2019
Posts
1,338
Reaction score
3,561
Moja kwa moja kwenye uzi.

Ugonjwa unaongoza kuua watu Tanzania kwa miaka na miaka ni malaria, lakini hatujawahi kutumia nguvu yeyote ya kutisha kukabiliana nao zaidi ya kupeana neti za misaada.

Magonjwa mengine yaliyoua /yanayoua watu wengi sana ni Shinikizo la damu na Sukari//kisukari .

Ugonjwa wa Covid-19 ukiupata una asilimia zaidi ya 97 (97%) kupona.

Yaani tukitaja magonjwa kumi (10) yanayoua watu wengi zaidi hapa Tanzania corona haipo kabisa, inapitwa mbali sana.

Idadi kubwa ya watanzania ni vijana na watoto ambao hawa wana zaidi ya asilimia 98 (98%) za kupona huu ugonjwa wa Covid-19.

Ni kwanini tunatumia nguvu kubwa ya kutaka kufungia watu uchumi wao na uhuru wao wa kufanya ibada kwa ugonjwa ambao ni asilimia 2% tu ( kwa makadirio ya juu sana ) wanaweza kupoteza maisha ?

Kwanini nguvu tunayojifanya tunaiweka kwenye COVID-19 tusiiweke kwanza kwenye magonjwa yanayoua watanzania wengi zaidi ambayo ni Malaria, Presha , Kisukari . Huku kwenye COVID-19 tuendelee na utaratibu wa herd immunity kama mwaka jana!.

Yaani sisi ni kama mtu anayefuga kuku, ambapo ndani wiki moja , kuna mwewe anakula kifaranga mmoja tu halafu hapo hapo kuna paka anakula vifaranga nane kwa siku. Badala ya kuua paka anayekula vifaranga nane kwa siku , tunatumia nguvu kupambana na mwewe anayekula kifaranga mmoja kwa wiki huku tukiacha vifaranga nane vikiendelea kuliwa na paka.

Nimalizie kwa kusema, Hayati Rais Magufuli mtamsema kwa mabaya yote, lakini hili la COVID-19 ataendelea kusifika kwa maono yake. Nchi yetu maskini sana kuigiza maigizo ya kuwekeana limitations wakati watu kutwa wanajazana mwendokasi , hawana ustararaabu wa kunawa mikono mara kwa mara na wengine hizo barakoa ndio kabisa yaani hawawezi hata kuzinunua .

Tuache Maigizo kwenye Maisha ya watu.
 
Tulia kijana. Sisi tunahakikisha mnapata chanjo ya corona. Pia tumeahidiwa ten% ya mauzo ya hizo chanjo zitakapopata soko kwenye nchi yenu. Mpango uliopo nikuwa tunajua corona haiwadhuru waafrika hivyo tunalazimisha chanjo ili ije ionekane hamjadhurika kwakuwa mumechanja ila ukweli nikuwa hamjadhurika kwakuwa kinga zenu zinahimili hao virus kupambana nao.
 
Soon wataumbuka
 
Malaria imetengeneza variants ngqpi katika miaka miwili iliyopita?
 
Back
Top Bottom