#COVID19 Malaria ndio inaua zaidi kuliko COVID19, mbona nguvu nyingi ziko kwenye COVID19

Variants mpya zinachochewa sana na watu wasiochanjwa.Hata huku, US kwa mfano, kuna watu wengi wanakataa chanjo kwa sababu ya kujazana ujinga.

Hao ndio wanaoumwa sana na kulazwa. Sasa hivi Marekani zaidi ya 97% ya wanaolazwa hospitalini kwa Covid ni wasiochanjwa.Hawa ndio wanaotengeneza new variants. Kati ya wanaokufa kwa Covid US zaidi ya 99% ni waliokataa chanjo.

Wengi wanaomba kuchanjwa baada ya kuumwa, wanaambiwa chanjo haifanyi kazi hivyo, unatakiwa uchanjwe kabla ya kuumwa.

Waliochanjwa hawatengenezi variants mpya, hata wakiambukizwa miili yao inaweza kufight viruses na kushinda mapema hata hawajui wamepata infection, hivyo hawatengenezi variants mpya.

Ukisema variants wapya wanakuwa hosted na wasiochanjwa ina maana waliochanjwa hawapati COVID-19?

Hilo ni moja, Mbona jana CDC wametoa ushauri hata waliochanjwa wavae Masks kama ni kweli ambao hawajachanjwa ndio wenye matatizo?
 
Marekani wali declare malaria free 1960, ni uzembe wetu
Point yangu ndio ipo hapo.

Magonjwa ambayo yanatuua sisi tumeyanyamazia as if COVID-19 ndio tatizo pekee au tatizo kubwa zaidi wakati ukweli ni kuwa watu wanakufa sana kwa malaria , Presha na Kisukari kushinda kufa na COVID-19.
 
Bro hii ni pandemic, viral diseases ndingi hazina dawa bali ni chanjo, na chanjo ina itaji mass vaccination hapa namaanisha kufikia herd immunity ndio maana kuna mass campaign, uki chanja watu wachache huta achieve chochote.
 
Really dude?

Sababu ni airborne contagious na ni virus ambaye hana dawa.
Pia anauwezo wa kuua immediately.

Malaria ina dawa na sio contagious kivyovyote na wala sio airborne.

Mimi naweza umwa malaria na nisitumie dawa yoyote nikapona ndani ya siku 3.
 
Variants mpya zinachochewa sana na watu wasiochanjwa.Hata huku, US kwa mfano, kuna watu wengi wanakataa chanjo kwa sababu ya kujazana ujinga.

Hao ndio wanaoumwa sana na kulazwa. Sasa hivi Marekani zaidi ya 97% ya wanaolazwa hospitalini kwa Covid ni wasiochanjwa.Hawa ndio wanaotengeneza new variants. Kati ya wanaokufa kwa Covid US zaidi ya 99% ni waliokataa chanjo.

Wengi wanaomba kuchanjwa baada ya kuumwa, wanaambiwa chanjo haifanyi kazi hivyo, unatakiwa uchanjwe kabla ya kuumwa.

Waliochanjwa hawatengenezi variants mpya, hata wakiambukizwa miili yao inaweza kufight viruses na kushinda mapema hata hawajui wamepata infection, hivyo hawatengenezi variants mpya.

All efficacy and safety profile ya hii vaccine ingetakiwa iwe backed up na data za clinical trial just like any other vaccine ...otherwise itakua ni porojo tu za ku rely on theory, ambapo achilia mbali kuleta madhara (kama yapo) ambayo hatujui ni % pia hatujui kama kweli inakinga kwa efficiency ipi.

Utajikingaje against new variant wakati ulichanja previous version ya chanjo?

Apparently, hizo data unazotoa bila kuwa backed up na clinical trial bado hazina uzito so as zimepatikana ndani ya miez tu
 
Ukisema variants wapya wanakuwa hosted na wasiochanjwa ina maana waliochanjwa hawapati COVID-19?

Hilo ni moja, Mbona jana CDC wametoa ushauri hata waliochanjwa wavae Masks kama ni kweli ambao hawajachanjwa ndio wenye matatizo?
Waliochanjwa wanapata maambukizi ya Covid-19, lakini maambukizi hayo hayashamiri, wengi wanakuwa hata hawaoni dalili, virusi vinauawa na antibodies zilizokuwa activated na vaccine.

Hiyo ndiyo idea ya vaccine, una activate antibodies ili mtu akipata maambukizi antibodies zishinde maambukizi.

Ndiyo maana Marekani wanaolazwa mahospitalini kwa Covid zaidi ya 97% ni wasiochanjwa, na wanaokufa kwa Covid zaidi ya 99% ni wasiochanjwa.

Wanaochanjwa wanashauriwa wavae mask kwa sababu haijulikani wasiochanjwa wanazalisha variants gani mpya ambazo zitareact vipi na vaccines za sasa.

Wakati tunaongelea Delta variant, tunaambiwa kuna Lambda variant imekuja, na tunapoongelea Lambda variant, hatujui kuna variant gani inaanza kuzunguka leo.

Ingewezekana wote wachanjwe siku moja, au hata 95% ya watu wangekuwa vaccinated siku moja, hizi new variants zingekuwa contained sana.

Lakini, kwa sababu kuna watu hawataki kuchanjwa, hilo lina maana kuna new variants zinaanzishwa kila siku.
 
All efficacy and safety profile ya hii vaccine ingetakiwa iwe backed up na data za clinical trial just like any other vaccine ...otherwise itakua ni porojo tu za ku rely on theory, ambapo achilia mbali kuleta madhara (kama yapo) ambayo hatujui ni % pia hatujui kama kweli inakinga kwa efficiency ipi.

Utajikingaje against new variant wakati ulichanja previous version ya chanjo?

Apparently, hizo data unazotoa bila kuwa backed up na clinical trial bado hazina uzito so as zimepatikana ndani ya miez tu
Unataka clinical trial data kwa chanjo ambazo zishakuwa administered kwa hundreds of million of people na kuna data zinazotokana na real life vaccination, si clinical trial?
 
Bro hii ni pandemic, viral diseases ndingi hazina dawa bali ni chanjo, na chanjo ina itaji mass vaccination hapa namaanisha kufikia herd immunity ndio maana kuna mass campaign, uki chanja watu wachache huta achieve chochote.
Marekani kule si wanatoa chanjo ya Flu, vipi imewahi kuisha!

Tuachane na hayo, wewe utakuwa tayari kucheza Russian Roulette na chanjo ambayo hata FDA ( US) wameshindwa kuthibitisha usalama wake !
 
Really dude?

Sababu ni airborne contagious na ni virus ambaye hana dawa.
Pia anauwezo wa kuua immediately.

Malaria ina dawa na sio contagious kivyovyote na wala sio airborne.

Mimi naweza umwa malaria na nisitumie dawa yoyote nikapona ndani ya siku 3.
Uko sahihi.

Kati ya malaria na COVID-19 ugonjwa upi unaua watanzania wengi ?
 
Waliochanjwa wanapata maambukizi ya Covid-19, lakini maambukizi hayo hayashamiri, wengi wanakuwa hata hawaoni dalili, virusi vinauawa na antibodies zilizokuwa activated na vaccine.

Hiyo ndiyo idea ya vaccine, una activate antibodies ili mtu akipata maambukizi antibodies zishinde maambukizi.

Ndiyo maana Marekani wanaolazwa mahospitalini kwa Covid zaidi ya 97% ni wasiochanjwa, na wanaokufa kwa Covid zaidi ya 99% ni wasiochanjwa.

Wanaochanjwa wanashauriwa wavae mask kwa sababu haijulikani wasiochanjwa wanazalisha variants gani mpya ambazo zitareact vipi na vaccines za sasa.

Wakati tunaongelea Delta variant, tunaambiwa kuna Lambda variant imekuja, na tunapoongelea Lambda variant, hatujui kuna variant gani inaanza kuzunguka leo.

Ingewezekana wote wachanjwe siku moja, au hata 95% ya watu wangekuwa vaccinated siku moja, hizi new variants zingekuwa contained sana.

Lakini, kwa sababu kuna watu hawataki kuchanjwa, hilo lina maana kuna new variants zinaanzishwa kila siku.
Kwa maana nyingine kutokana na hizo variants zinazokuja kila siku, kupata chanjo ambayo FDA hawajathibitisha usalama wake na (huku Tanzania lazima usaini Disclaimer agreement , serikali haitohusika madhara ya hiyo chanjo) ni sawa na ujinga kwa sababu unachanjwa na bado unaendelea kuvaa mask, variants watakaokuja wanaweza wakawa wakali kuliko ilivyotarajiwa ikawa ni sawa na bure kuchanjwa
 
Marekani kule si wanatoa chanjo ya Flu, vipi imewahi kuisha!

Tuachane na hayo, wewe utakuwa tayari kucheza Russian Roulette na chanjo ambayo hata FDA ( US) wameshindwa kuthibitisha usalama wake !
Ndio. Fatilia historia ya chanjo ya polio ili fanya watu wengi vilema na ilitumika mapema kuliko hata hii ila ndio tuna itumia sasa. In a war use every weapon at youre disposal. Desperate times needs desperate measures
 
Chanjo Johnson And Johnson Covax
Ni Hiyari Kwanini Top Leaders Wanateseka Sana Hili Jambo
Wangetangaza Chanjo Ipo Utaamua Mwenyewe

Sasa Wao Wanawaziba Watu Midomo Wasiongee Mabaya Isipokuwa Mazuri Tu Ya Johnson And Johnson 😃😂😁😉😄😅😆

Kweli Wasomi Wa Sasa Hivi Kuna Namna Siyo Bure
 
Bro hii ni pandemic, viral diseases ndingi hazina dawa bali ni chanjo, na chanjo ina itaji mass vaccination hapa namaanisha kufikia herd immunity ndio maana kuna mass campaign, uki chanja watu wachache huta achieve chochote.
Mkuu acha kuelewesha majiwe hayo
 
Kwa maana nyingine kutokana na hizo variants zinazokuja kila siku, kupata chanjo ambayo FDA hawajathibitisha usalama wake na (huku Tanzania lazima usaini Disclaimer agreement , serikali haitohusika madhara ya hiyo chanjo) ni sawa na ujinga kwa sababu unachanjwa na bado unaendelea kuvaa mask, variants watakaokuja wanaweza wakawa wakali kuliko ilivyotarajiwa ikawa ni sawa na bure kuchanjwa
Ni muhimu kwenda na context na probabilities.

Yani mtu anakwambia leo wanaolazwa mahospitalini Marekani zaidi ya 97% ni wasiochanjwa, na zaidi ya 99% ya wanaokufa ni wasiochanjwa, halafu bado unakataa kuchanjwa kwa sababu hujui kesho variant gani itazaliwa? Na hapohapo unaambiwa kwamba kutochanjwa ni sababu kubwa ya variants mpya kuzaliwa? Huoni hapo kukataa chanjo kunakumaliza kwa sababu unaongeza nafasi ya kuugua na hata kufa?

Chanjo kama huku Marekani siku zote zimekuwa na disclaimer.Mimi nilivyoanza chuo niliulizwa rekodi za chanjo zangu za MMR. Sikuwa nazo. Nikachanjwa.Nilivyochanjwa nikapewa disclaimer kwamba kunaweza kutokea madhara.Hiki ni kitu cha kawaida hata kwa chanjo zilizokuwa fully confirmed.Ila, inabidi tuweke vitu katika muktadha sahihi. Kwa sababu unaweza kukataa chanjo kwa risk iliyo ndogo sana ya kukufanya uugue au ufariki, pia hapo hapo ukakubali kukaa bila kuchanjwa ukiwa na risk kubwa sana ya kuugua na kufa.

Narudia tena kusema, kuna watu wengi waliokataa chanjo wamepata ugonjwa, wamelazwa, wanalilia chanjo baada ya kuugua. Wanaambiwa chanjo haifanyi kazi hivyo, inatakiwa uchanjwe kabla hujaumwa. Wengine wanafariki.

Disclaimer si ujinga, ujinga ni kutoelewa nature ya disclaimer, kutoelewa proportionality, kutoelewa context.

Kwa jamii zetu ambazo hazijazoea kusoma disclaimer, hazijazoea nuance, hazijazoea transparency, disclaimer inaweza kuonekana ujinga.Lakini hilo ni tatizo la ujinga wa jamii, si tatizo la ujinga wa dislaimer.

Kwenye nchi legalistic kama US unaweza kutoa vaccine kwa watu milioni mia moja, akafa mtu mmoja tu.

Kama hujatoa disclaimer ambaye ingeokoa maisha ya huyo mtu mmoja, familia yake inaweza kushitaki serikali serikali ikalipa mamilioni ya dola na kuonekana haikufuata compliance ya disclosure, trasnparency na disclaimer.

Kwa hivyo wenzetu wanajua mambo haya, sisi tunaona ajabu kwa sababu tunalazimishwa na international conventions tu. Watu wetu wengi illiterate, innumerate, hawajui proportion, hawajui context, hawajui nuance, ndiyo maana disclaimer inaweza kuonekana ujinga.
 
Moja kwa moja kwenye uzi.

Ugonjwa unaongoza kuua watu Tanzania kwa miaka na miaka ni malaria, lakini hatujawahi kutumia nguvu yeyote ya kutisha kukabiliana nao zaidi ya kupeana neti za misaada.

Magonjwa mengine yaliyoua /yanayoua watu wengi sana ni Shinikizo la damu na Sukari//kisukari .

Ugonjwa wa Covid-19 ukiupata una asilimia zaidi ya 97 (97%) kupona.

Yaani tukitaja magonjwa kumi (10) yanayoua watu wengi zaidi hapa Tanzania corona haipo kabisa, inapitwa mbali sana.

Idadi kubwa ya watanzania ni vijana na watoto ambao hawa wana zaidi ya asilimia 98 (98%) za kupona huu ugonjwa wa Covid-19.

Ni kwanini tunatumia nguvu kubwa ya kutaka kufungia watu uchumi wao na uhuru wao wa kufanya ibada kwa ugonjwa ambao ni asilimia 2% tu ( kwa makadirio ya juu sana ) wanaweza kupoteza maisha ?

Kwanini nguvu tunayojifanya tunaiweka kwenye COVID-19 tusiiweke kwanza kwenye magonjwa yanayoua watanzania wengi zaidi ambayo ni Malaria, Presha , Kisukari . Huku kwenye COVID-19 tuendelee na utaratibu wa herd immunity kama mwaka jana!.

Yaani sisi ni kama mtu anayefuga kuku, ambapo ndani wiki moja , kuna mwewe anakula kifaranga mmoja tu halafu hapo hapo kuna paka anakula vifaranga nane kwa siku. Badala ya kuua paka anayekula vifaranga nane kwa siku , tunatumia nguvu kupambana na mwewe anayekula kifaranga mmoja kwa wiki huku tukiacha vifaranga nane vikiendelea kuliwa na paka.

Nimalizie kwa kusema, Hayati Rais Magufuli mtamsema kwa mabaya yote, lakini hili la COVID-19 ataendelea kusifika kwa maono yake. Nchi yetu maskini sana kuigiza maigizo ya kuwekeana limitations wakati watu kutwa wanajazana mwendokasi , hawana ustararaabu wa kunawa mikono mara kwa mara na wengine hizo barakoa ndio kabisa yaani hawawezi hata kuzinunua .

Tuache Maigizo kwenye Maisha ya watu.

Kwanza zingatia maabukizo ya covd19 na malaria ni tofauti pia hiyo asilimia 2% ya corona kuua ni ktk kipindi kifupi sana ukifananisha na malaria. pia tiba kubwa ya corona ni oxygen tiba hii pia ni aghali sana na adimu kuzidi ya maleria.
Na toka kuzaliwa hujawahi kusikia hospitali imeelemewa na wagonjwa wa maleria lakini korona hospitali zimeelemewa
Pia hajawahi kusikia wauguzi na madaktari kadhaa waliokua wanahudumia wagonjwa wa malaria wamekufa kwa malaria. Lakini korona imewabeba
Haya ni mambo machache sana yanayo tofautisha uhatari wa corona19 dhidi ya malaria kama utatuliza akili na kuchunguza zaidi uta pata mengi ya hatari zaidi ktk covid 19 dhidi ya malaria
 
Hizi nchi za kiafrika zinatawaliwa na mafala, hizo nguvu za kupambana corona wangeziamishia kwenye magonjwa yenye high mortality rate ingekuwa poa sana.
Kwani makaria haipambaniwi. Neti unayochomeka ya nini. Malaria inatibika ukiwahi corona haina dawa ndio maana ya kupata chanjo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom