Ni muhimu kwenda na context na probabilities.
Yani mtu anakwambia leo wanaolazwa mahospitalini Marekani zaidi ya 97% ni wasiochanjwa, na zaidi ya 99% ya wanaokufa ni wasiochanjwa, halafu bado unakataa kuchanjwa kwa sababu hujui kesho variant gani itazaliwa? Na hapohapo unaambiwa kwamba kutochanjwa ni sababu kubwa ya variants mpya kuzaliwa? Huoni hapo kukataa chanjo kunakumaliza kwa sababu unaongeza nafasi ya kuugua na hata kufa?
Chanjo kama huku Marekani siku zote zimekuwa na disclaimer.Mimi nilivyoanza chuo niliulizwa rekodi za chanjo zangu za MMR. Sikuwa nazo. Nikachanjwa.Nilivyochanjwa nikapewa disclaimer kwamba kunaweza kutokea madhara.Hiki ni kitu cha kawaida hata kwa chanjo zilizokuwa fully confirmed.Ila, inabidi tuweke vitu katika muktadha sahihi. Kwa sababu unaweza kukataa chanjo kwa risk iliyo ndogo sana ya kukufanya uugue au ufariki, pia hapo hapo ukakubali kukaa bila kuchanjwa ukiwa na risk kubwa sana ya kuugua na kufa.
Narudia tena kusema, kuna watu wengi waliokataa chanjo wamepata ugonjwa, wamelazwa, wanalilia chanjo baada ya kuugua. Wanaambiwa chanjo haifanyi kazi hivyo, inatakiwa uchanjwe kabla hujaumwa. Wengine wanafariki.
Disclaimer si ujinga, ujinga ni kutoelewa nature ya disclaimer, kutoelewa proportionality, kutoelewa context.
Kwa jamii zetu ambazo hazijazoea kusoma disclaimer, hazijazoea nuance, hazijazoea transparency, disclaimer inaweza kuonekana ujinga.Lakini hilo ni tatizo la ujinga wa jamii, si tatizo la ujinga wa dislaimer.
Kwenye nchi legalistic kama US unaweza kutoa vaccine kwa watu milioni mia moja, akafa mtu mmoja tu.
Kama hujatoa disclaimer ambaye ingeokoa maisha ya huyo mtu mmoja, familia yake inaweza kushitaki serikali serikali ikalipa mamilioni ya dola na kuonekana haikufuata compliance ya disclosure, trasnparency na disclaimer.
Kwa hivyo wenzetu wanajua mambo haya, sisi tunaona ajabu kwa sababu tunalazimishwa na international conventions tu. Watu wetu wengi illiterate, innumerate, hawajui proportion, hawajui context, hawajui nuance, ndiyo maana disclaimer inaweza kuonekana ujinga.