Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Eleza kwa kifupi nini kinatokea, isije ikawa ndio mwanzo wa kuota matende..
Mmh ningeshakuwa nayo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Eleza kwa kifupi nini kinatokea, isije ikawa ndio mwanzo wa kuota matende..
Nimekuwa na tatizo hili kwa miaka 2, nilianza na typhord...nimepona typhod then tatizo hilo likaniandama hadi kufikia kuona naenda kufa, mwisho nimetunia dawa inaitwa Artequine, kwisha habari kwa sasa ila ina bei kubwa, ni 25,000 sijui kama nilibamizwa wala sikujali sana, nina afya njema sasa karibia miezi 6 sasa, you can also try it..pia pima typhord kwanza ..
mkuu hata mm naitumiaga na inanisaidia sana, ni dose ya vidonge 4 ila walikumbambika japo cjajua ni dose toka nchi gani may b, coz kuna china, england na n.k bt mi huwa natumia 12000
Wakuu
Nimekuwa na shida ya muda sasa..nimekuwa nikipata malaria mara kwa mara. Nimemeza dawa mbalimbali lakini siwezi kumaliza miezi mitatu inarejea tena. Naombeni ushauri
DAWA ASILIA YA MALARIA SUGU :
Majani -Ya -Aloe Vera
![]()
Majani Ya Aloe Vera
Kama unasumbuliwa na Malaria Sugu fuata maelekezo yafuatayo kutayarisha dawa ya asili.
MAHITAJI :
i.Majani ya mwarobaini kiasi cha viganja viwili vya mtu mzima.
ii.Majani ya Aloevela kiasi cha viganja viwili vya mtu mzima..
iii. Maji safi na salama lita tatu.
Hatua Za Kufuata
Changanya majani ya mwarobaini na alovela kwenye sufuria, kisha ongeza lita tatu za maji safi na salama halafu chemsha pamoja mpaka utakapo ona mchanganyiko wako unatoa mchuzi ama soup. Ipua , chuja, kasha ihifadhi dawa yako kwenye chupa ya chai.
MATUMIZI :
Kunywa kikombe kimoja cha dawa yako mara tatu kwa siku kwa muda wa siku tatu mfululizo na malaria itapona.
ALTERNATIVELY :
Vile vile unaweza kutumia ndimu na maji ya madafu kujitibu malaria sugu.
MAHITAJI :
i.Ndimu Saba Zilizo komaa vizuri.
ii.Maji Ya Madafu.
JINSI YA KUFANYA :
Chukua dafu, likate kisha maji yake uyahifadhi kwenye jagi, halafu chukua ndimu saba, zikamulie kwenye maji ya madafu halafu koroga mchanganyiko wako.
MATUMIZI :
Kunywa glasi mbili kwa siku, asubuhi glasi moja na jioni glasi moja. Fanya hivyo mpaka malaria itakapo ondoka.
KWA MAMA MJAMZITO USITUMIE HIYO DAWA TUMIA DAWA HII HAPA CHINI.Samahani, je mama mjamzito anaweza kuitumia bila kumletea madhara hii dozi yako?
Habari zenu wakuu, nilisumbuliwa na malaria kwa vipindi viwili tofauti january 2014 na mwanzoni mwa mwezi huu, nilienda vituo vya afya tofauti mara hizo mbili. Huko kote vipimo vimeonyesha malaria ipo ila nilipofika kwa daktari sehemu zote mbili naulizwa "mara ya mwisho ulitumia dawa gani" !! alafu naandikiwa dawa hiyo hiyo niliyotumia mwanzo . Swali langu hapo wataalam wa afya , je hakuna dozi ya vidonge au sindano za uhakika kumponya mgonjwa wa malaria kwa mda mrefu bila kumwuliza alitumia dawa gani mara ya mwisho?
Hakuna antibiotics; ila kuna mitishamba!
Kabla ya kukushauri kuhusu dawa huko unakokaa kuna mbu wengi wanaoambukiza malaria?
Kama jibu ni ndiyo unatumia njia gani kujikinga kung'atwa na hao mbu?
Mkuu kwa kweli kwa usiku najikinga vya kutosha kwanza kwa mafuta ya kuzuia mbu mida ya jioni na nalala ndani ya net isiyo na tobo hata moja kubwa zaidi ya design ya matundu yake!! Labda kwenye basi au sehemu za kazi mda wa mchana bila kufahamu!
Kukuandikia dawa ile ile uliyotumia kabla ni kukuepusha na complications za hizi dawa za malaria kwani ukiandikiwa nyingine inaweza isikutibu au ikakuletea madhara makubwa zaidi. Unapatikana wapi? Nina dawa ya asili ya malaria sugu tuwasiliane
Matibabu ya malaria yamegawanyika katika sehemu mbili muhimu.
Mosi:Malaria ya kawaida(Uncomplicated malaria)...hii yaweza kutibiwa na kundi la dawa lijulikanalo kama ACT Artimesinin combination therapy...kwa Tanzania kuna dawa kama ALU(MSETO WA ARTMETHER NA LUMEFANTRINE),ARTEQUICK,ARTEQUIN,DUOCOTEXIN...
PILI:Malaria kali(complicated or severe malaria)....hii hutibiwa kwa mgonjwa kulazwa na kupewa sindano za Artesunate au quinin au Artmether na kufuatiwa na vidonge.
Kwa ufupi na kwa umuhimu(specificicity) haya ndio matibabu ya malaria.
Kuna uwezekano mkubwa malaria inasingiziwa sana na watoa huduma wetu ndio maana unahisi malaria yako haiishi au kujirudia.
Habari zenu wakuu, nilisumbuliwa na malaria kwa vipindi viwili tofauti january 2014 na mwanzoni mwa mwezi huu, nilienda vituo vya afya tofauti mara hizo mbili. Huko kote vipimo vimeonyesha malaria ipo ila nilipofika kwa daktari sehemu zote mbili naulizwa "mara ya mwisho ulitumia dawa gani" !! alafu naandikiwa dawa hiyo hiyo niliyotumia mwanzo . Swali langu hapo wataalam wa afya , je hakuna dozi ya vidonge au sindano za uhakika kumponya mgonjwa wa malaria kwa mda mrefu bila kumwuliza alitumia dawa gani mara ya mwisho?