Malaria sugu inanitesa! Dawa gani itanipa tiba ya kudumu?


mkuu hata mm naitumiaga na inanisaidia sana, ni dose ya vidonge 4 ila walikumbambika japo cjajua ni dose toka nchi gani may b, coz kuna china, england na n.k bt mi huwa natumia 12000
 
mi nilichukua ya sweden

mkuu hata mm naitumiaga na inanisaidia sana, ni dose ya vidonge 4 ila walikumbambika japo cjajua ni dose toka nchi gani may b, coz kuna china, england na n.k bt mi huwa natumia 12000
 
Wakuu

Nimekuwa na shida ya muda sasa..nimekuwa nikipata malaria mara kwa mara. Nimemeza dawa mbalimbali lakini siwezi kumaliza miezi mitatu inarejea tena. Naombeni ushauri



DAWA ASILIA YA MALARIA SUGU :




Majani -Ya -Aloe Vera




Majani Ya Aloe Vera


Kama unasumbuliwa na Malaria Sugu fuata maelekezo yafuatayo kutayarisha dawa ya asili.


MAHITAJI :


i.Majani ya mwarobaini kiasi cha viganja viwili vya mtu mzima.


ii.Majani ya Aloevela kiasi cha viganja viwili vya mtu mzima..


iii. Maji safi na salama lita tatu.




Hatua Za Kufuata


Changanya majani ya mwarobaini na alovela kwenye sufuria, kisha ongeza lita tatu za maji safi na salama halafu chemsha pamoja mpaka utakapo ona mchanganyiko wako unatoa mchuzi ama soup. Ipua , chuja, kasha ihifadhi dawa yako kwenye chupa ya chai.


MATUMIZI :
Kunywa kikombe kimoja cha dawa yako mara tatu kwa siku kwa muda wa siku tatu mfululizo na malaria itapona.


ALTERNATIVELY :


Vile vile unaweza kutumia ndimu na maji ya madafu kujitibu malaria sugu.


MAHITAJI :
i.Ndimu Saba Zilizo komaa vizuri.
ii.Maji Ya Madafu.




JINSI YA KUFANYA :


Chukua dafu, likate kisha maji yake uyahifadhi kwenye jagi, halafu chukua ndimu saba, zikamulie kwenye maji ya madafu halafu koroga mchanganyiko wako.


MATUMIZI :


Kunywa glasi mbili kwa siku, asubuhi glasi moja na jioni glasi moja. Fanya hivyo mpaka malaria itakapo ondoka.

 

Attachments

  • Aloe_vera_plant.jpg
    11.1 KB · Views: 486

Samahani, je mama mjamzito anaweza kuitumia bila kumletea madhara hii dozi yako?
 
Samahani, je mama mjamzito anaweza kuitumia bila kumletea madhara hii dozi yako?
KWA MAMA MJAMZITO USITUMIE HIYO DAWA TUMIA DAWA HII HAPA CHINI.



DAWA YA KUTIBU MALARIA SUGU FANYA HIVI:

Malimao na Kiitunguu Saumu.

Chukua vitunguu Saumu vilivyo menywa kiganja kimoja cha mkono, twanga vilainike,

halafu kamulia limao moja au mawili. Acha vikae angalao kwa masaa 2 halafu weka maji

salama, ya uvuguvugu ndio mazuri. Chuja na unywe.

Fanya hivyo mara 2 kwa siku, halafu angalau siku 3 au siku 7 kwa uhakika zaidi.

Huo mpango pia inatibu typhoid sugu. Homa ya Matumbo hii dawa.

Pia kunywa maji mengi ya Uvuguvugu ili kuondoa sumu mwilini.
 
Habari zenu wakuu, nilisumbuliwa na malaria kwa vipindi viwili tofauti january 2014 na mwanzoni mwa mwezi huu, nilienda vituo vya afya tofauti mara hizo mbili. Huko kote vipimo vimeonyesha malaria ipo ila nilipofika kwa daktari sehemu zote mbili naulizwa "mara ya mwisho ulitumia dawa gani" !! alafu naandikiwa dawa hiyo hiyo niliyotumia mwanzo . Swali langu hapo wataalam wa afya , je hakuna dozi ya vidonge au sindano za uhakika kumponya mgonjwa wa malaria kwa mda mrefu bila kumwuliza alitumia dawa gani mara ya mwisho?
 

Hakuna antibiotics; ila kuna mitishamba!
 
Kabla ya kukushauri kuhusu dawa huko unakokaa kuna mbu wengi wanaoambukiza malaria?

Kama jibu ni ndiyo unatumia njia gani kujikinga kung'atwa na hao mbu?
 
Kabla ya kukushauri kuhusu dawa huko unakokaa kuna mbu wengi wanaoambukiza malaria?

Kama jibu ni ndiyo unatumia njia gani kujikinga kung'atwa na hao mbu?

Mkuu kwa kweli kwa usiku najikinga vya kutosha kwanza kwa mafuta ya kuzuia mbu mida ya jioni na nalala ndani ya net isiyo na tobo hata moja kubwa zaidi ya design ya matundu yake!! Labda kwenye basi au sehemu za kazi mda wa mchana bila kufahamu!
 
Mkuu kwa kweli kwa usiku najikinga vya kutosha kwanza kwa mafuta ya kuzuia mbu mida ya jioni na nalala ndani ya net isiyo na tobo hata moja kubwa zaidi ya design ya matundu yake!! Labda kwenye basi au sehemu za kazi mda wa mchana bila kufahamu!

Mkuu nimekupata!

Umeshafanya vipimo kujua hali ya afya yako kwa jumla?

Nakuuliza hivi kwa sababu vituo vingine vya afya hawapimi malaria kiusahihi. Unaweza ambiwa una malaria wakati huna, au huna wakati unayo! Kuna magonjwa mengine ambayo dalili zake zinaweza onekana kama malaria k.m. typhoid, High blood pressure, kisukari n.k. n.k

Unaweza ukawa unatumia dawa za malaria wakati una tatizo jingine!
 
vituo vya afya nilivyokwenda ni vya uhakika kabisa! Tatizo ni hili kwa nini waniulize nilitumia dawa gani mara ya mwisho then wananiandikia dawa hiyo dawa tena sehemu tofauti badala ya wao kuniandikia dawa (kama ipo ya kutibu mda mrefu zaidi hata ukiumwa na mbu mwenye vimelea vya wadudu wa malaria), au hakuna dawa ya uhakika ya malaria?
 
Kukuandikia dawa ile ile uliyotumia kabla ni kukuepusha na complications za hizi dawa za malaria kwani ukiandikiwa nyingine inaweza isikutibu au ikakuletea madhara makubwa zaidi. Unapatikana wapi? Nina dawa ya asili ya malaria sugu tuwasiliane
 
Matibabu ya malaria yamegawanyika katika sehemu mbili muhimu.
Mosi:Malaria ya kawaida(Uncomplicated malaria)...hii yaweza kutibiwa na kundi la dawa lijulikanalo kama ACT Artimesinin combination therapy...kwa Tanzania kuna dawa kama ALU(MSETO WA ARTMETHER NA LUMEFANTRINE),ARTEQUICK,ARTEQUIN,DUOCOTEXIN...

PILI:Malaria kali(complicated or severe malaria)....hii hutibiwa kwa mgonjwa kulazwa na kupewa sindano za Artesunate au quinin au Artmether na kufuatiwa na vidonge.

Kwa ufupi na kwa umuhimu(specificicity) haya ndio matibabu ya malaria.

Kuna uwezekano mkubwa malaria inasingiziwa sana na watoa huduma wetu ndio maana unahisi malaria yako haiishi au kujirudia.
 
Kukuandikia dawa ile ile uliyotumia kabla ni kukuepusha na complications za hizi dawa za malaria kwani ukiandikiwa nyingine inaweza isikutibu au ikakuletea madhara makubwa zaidi. Unapatikana wapi? Nina dawa ya asili ya malaria sugu tuwasiliane

kwa iyo dawa za malaria zina ingridients tofauti kabisa? mi napatikana hapa jjn dsm.
 

kwa mtiririko huo nimekuelewa mkuu, ntakuwa naenda zaid ya hospitali mbili ku check status, mda mwengine isije ikawa ni kusingiziwa kama ulivyosema. shukrani.
 
weka utaratibu wa kunywa maji kama nusu lita au lita na zaidi kila siku alfajiri kabla ya kuswaki..
huu ni ushuhuda ndugu na malaria
_kujamba kitu kinachonuka
_mdomu kutoa harufu
_kikohozi
_mafua
vitakuwa history kwako,kila la heri
 

TIBA YA MALARIA


Ugonjwa wa malaria umekuwa na tiba za asili nyingi ambazo baadhi tumeshaziandika na zimewasaidia wengi, leo tunawaletea tiba nyingine inayomaliza kabisa maradhi hayo.

Bamia
Chukua mbegu za bamia uzikaange, uzisage mpaka ziwe unga.
Chemsha nusu kikombe cha unga huo katika glasi 2 za maji kisha chuja.

Dozi:
Wakubwa kikombe 1 x 3 kwa siku kila baada ya mlo.
Miaka (7-12 ) anywe nusu kikombe x 3 kwa siku kila baada ya mlo. Huruhusiwi kuchemsha na kuweka bali fanya hivyo kila unapotaka kunywa.
Miaka (2-6) robo kikombe x 3 kwa siku.
Kwa watoto wachanga kijiko kikubwa 1 x 3, mpatie baada ya kunyonya au kunywa maziwa na kushiba.

Papai

Chukua mbegu za papai zikaushe kivulini, baada ya hapo zisage ziwe unga laini.

Dozi:
Weka kijiko kimoja cha chai kwenye uji, kama huwezi kutumia uji unaweza kuweka kwenye chai lakini muhimu sana kwenye uji.
Kwa siku tumia mara tatu.
Kwa mtoto miaka 5-10 unaweza kumgawia nusu ya mtu mzima.
Kwa mtoto wa miaka 3-5 unaweza kumgawia ¼ wote x 3 kutwa.

Alizeti
Chemsha kilo moja ya majani ya alizeti katika lita 2½ za maji kwa dakika 15. Dozi:
Kunywa nusu glasi x 3 kwa siku, tumia tiba hii kwa muda wa siku 5.
Miaka (7-12) ¼ glasi x 3 kwa siku. Miaka (2-6) kijiko 1 x 3 kwa siku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…