Malaria sugu inanitesa! Dawa gani itanipa tiba ya kudumu?

weka utaratibu wa kunywa maji kama nusu lita au lita na zaidi kila siku alfajiri kabla ya kuswaki..
huu ni ushuhuda ndugu na malaria
_kujamba kitu kinachonuka
_mdomu kutoa harufu
_kikohozi
_mafua
vitakuwa history kwako,kila la heri

mkuu ntajaribu tena maana nilianzaga nikashindwa kabisa kunywa maji alfajiri, nafahamu uzima hauna duka ni kuulinda kwa nguvu zote. Shukrani
 

Nashukuru kwa msaada, nitaitengeneza hiyo dawa na kuitumia atlist dozi moja kila mwezi au miezi miwili kulinda afya.
 

Mimi sio mtaalam persay ila I can suggest something, kwanza inatakiwa ujue kwamba maambukizi mapya yapo yaweza kuwa ulipata maambukizi mapya ndio mana malaria haikutoka, Pili kweli yawezekana dawa imefail kwako ila ilitakiwa ulivyokwenda kwa doctor ungemwambia pia ulitumia na dozi gani haikutoa hiyo malaria ili aangalie dozi mbadala. Mwisho sasa nenda hospitali uombe kutumia Quinine ipo vidonge japokua ni vichungu sana,ipo ya dripu pia ipo ya sindano kwahiyo unaweza kumueleza wakutibu kwa quinine sasa unaweza kuamua kurudi kwa hizo hospital au uende tofauti ya hizo zote ili usipate upinzani katika kuchagua dozi, Quinine ni dawa yenye nguvu kutibu malaria yoyote ile na nina imani ukiweza kucontrol mbu unaweza kukaa kipindi kirefu bila kuumwakuumwa, Ni hayo tu mzee
 
Mkuu kuna dawa ya kipare inaitwa MVORO hiyo ni komesha.ni pm
 
Waungwana poleni sana kwa usumbufu ila naomba msaada wenu, nasumbuliwa sana na malaria.

Nimeshatumia ACT (combination therapy ya artesunate na amodiaquine) nimetumia pia IV ya quinine na vidonge vyake.

IV niliwekewa ya siku tatu na baadae wakanipatia quinine tabs. Hii ni wiki ya pili toka nitoke hospital lakini dalili za malaria zinaanza chipua tena.

Sasa nauliza kwa madaktari na wanaojua nitumie dawa gani nipone malaria hii?

ahsante sana.
 
tumia aback sauda.
mimi imenisaidia sana kuimarisha afya yangu.
mtumie pm MZIZI MKAVU atakupa maelezo mazuri zaidi.
Ugua pole .
 

TIBA YA UGONJWA WA MALARIA

Ugonjwa wa malaria umekuwa na tiba za asili nyingi ambazo baadhi tumeshaziandika na zimewasaidia wengi, leo tunawaletea tiba nyingine inayomaliza kabisa maradhi hayo.

BAMIA
Chukua mbegu za bamia uzikaange, uzisage mpaka ziwe unga.
Chemsha nusu kikombe cha unga huo katika glasi 2 za maji kisha chuja.

DOZI
Wakubwa kikombe 1 x 3 kwa siku kila baada ya mlo.
Miaka (7-12 ) anywe nusu kikombe x 3 kwa siku kila baada ya mlo. Huruhusiwi kuchemsha na kuweka bali fanya hivyo kila unapotaka kunywa.
Miaka (2-6) robo kikombe x 3 kwa siku.
Kwa watoto wachanga kijiko kikubwa 1 x 3, mpatie baada ya kunyonya au kunywa maziwa na kushiba.

PAPAI
Chukua mbegu za papai zikaushe kivulini, baada ya hapo zisage ziwe unga laini.

DOZI
Weka kijiko kimoja cha chai kwenye uji, kama huwezi kutumia uji unaweza kuweka kwenye chai lakini muhimu sana kwenye uji.
Kwa siku tumia mara tatu.
Kwa mtoto miaka 5-10 unaweza kumgawia nusu ya mtu mzima.
Kwa mtoto wa miaka 3-5 unaweza kumgawia ¼ wote x 3 kutwa.

ALIZETI
Chemsha kilo moja ya majani ya alizeti katika lita 2½ za maji kwa dakika 15.

DOZI
Kunywa nusu glasi x 3 kwa siku, tumia tiba hii kwa muda wa siku 5.
Miaka (7-12) ¼ glasi x 3 kwa siku.
Miaka (2-6) kijiko 1 x 3 kwa siku.
 
wakubwa, nawasalimu kwa jina la UKAWA!
hivi hii dawa ya kichina ya Malaria ARCO dose Sahihi kwa mtu wa kilo 80 ni vidonge vingapi.Nimeandikiwa 4 lakini nikisoma mtandaoni zinasema 8. Ushauri madaktari.
 
umenichefua tu kwa salam yako,, UKAWA ndo nini,, salam ya Mola wetu, waweza sema Assalam aleikum au bwana asifiwe
 
Kwanza malaria imegawanyika kwenye makundi 2 ambayo ni malaria ya kawaida ambayo hutibiwavnaALU(mseto wa lumefantrine,artmether)
2 ni severe malaria ambayo hutibiwa na sindazo za (quinini au artesunate) kinacho fanya uonekane kama mgonjwa wa malaria kila siku ni due to uelewa mdogo wa bahashi ya madaktari. M2 unapo pata treatment ya malaria huwa plasmodium wana kufa ila wanakuwa wana acha antigen kwenye damu ivyo mgonjwa huendele kuumwa ata zaidi ya week 3 tangu ameze dawa..!!kinacho fanya aonekane na malaria tena ni kipimo cha MRDT kwani huwa kina detect antibody zilizo mwilini na syo plasmodium ivyo always utaonekana una malaria..!!ili kuthibitisha auna malaria nilazima upimwe kwaku 2mia gold standard(microscope.)
 
Unapoulizwa dawa ulotumia mara ya mwisho ni kwa faida yako, kumbuka kuna wengne dawa zenye sulphur zinawadhuru.
 
nipigie 0714522518 namimi ni muhanga wa tatizo la malaria sugu
 
mkuu nielekeze namna ya kuitumia zandu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…