Wakuu naomba msaada wa tiba ya malaria sugu tangu ujana wangu hadi leo nakaribia 50yrs nimekuwa nauguwa na kutibu malaria kila mwezi, tangu wakati wa chroloquine, fansider, Halfan,Metakhafin, Amodiaquine, mseto,,,,dawa za asili mshana, mwarobaini, soku-masai, n.k kwa yeyote atakae niwezesha kukaa angalau kila baada ya mwaka mmoja naahidi kutoa zawadi nono shs 100,000 hadi shs 2,000,000.
Nimekuwa na mawazo kuwa immunity yangu kwa malaria ni very weak, sababu sijasumbuliwa na magonjwa mengine labda kdg tonslitis kwa mwaka x2, minyoo x3 kwa mwaka, Mafua ndio mara kwa mara kila dalili za malaria tu
Swali langu je pana namna yeyote ya kuongeza immunity(kinga) ya mwili hasa dhidi ya malaria ?
Kwa kukurupuka naweza sema kwa uhakika 'siamini' kuwa tatizo lako ni Malaria, hakuna mtu anaugua Malaria sugu tangu ujana, japo sijui sasa una umri gani..lakini naweza kisia ni miaka mingi umekuwa ukiugua. Lakini pia jua kuwa kwa kuishi sehemu yenye Malaria kwa wingi (Malaria endemic area), si lazima kila illness episode basi ni Malaria, unaweza kuwa ukawa unaugua magonjwa/ugonjwa mwingine pia lakini unang'ang'ania ni Malaria.
Kabla hujaita ugonjwa ni 'Malaria Sugu', kuna vigezo inabidi vitimie:
1. Umepima kwa kipimo cha 'Malaria Blood Slide' (Gold Standard for Malaria Diagnosis) kikifanywa na qualified Lab Technician, na akona wadudu wa Malaria
2. Ukatumia dawa sahihi (iwe Chloroquine kwa enzi hizo, au SP wakati wa era yake, au sasa ARTs (Mseto), kwa dozi sahihi kulingana na uzito/umri wako, na ukatumia dozi kama ulivyoshauriwa na kumaliza
3. Ukapima tena Malaria baada ya kumaliza dozi na bado wadudu wa Malaria wakaonekana
Kifupi cha hapo juu...bado hujaita ugonjwa ni 'Malaria Sugu'! Jiulize kama mara zote hizo ulizougua tangu ujana ulienda hospitali ukapimwa Malaria ikaonekana, na ukapewa dawa sahihi na ukamaliza dozi, na bado wadudu wakaonekana baada ya kumaliza dawa.
Wakati mwengine watu huwa wanachanganya 'Malaria Sugu' (old inadequately treated infection)....na 'Malaria Maambukizo Mapya' (new infection after treatment). Ukipata Malaria ikatibiwa, haina maana hutapata Malaria tena kama utarudi kwenye mazingira na tabia zako zinazokuweka katika risk ya kupata Malaria. Kinachotokea ni mtu anapata Malaria, inatibiwa, hacheck kama imetibika yoote baada ya dozi, anarudi kwenye mazingiara na tabia zake za kutojilinda na Malaria, anapata maambukizi mapya ya Malaria, akirudi hospitali kupima na kuambiwa ana malaria...anaiita 'Malaria Sugu'! Hiyo si Malaria sugu, bali ni new infection kutokana na kutojilinda na Malaria. Je wewe unajilinda na Malaria tangu huo ujana wako?
Au inawezekana pia ukawa unasumbuliwa na ugonjwa mwingine ambao si Malaria, na labda unaenda kwenye dispensary (hasa private) ambazo capacity yake ni ndogo, lakini wanataka kutengeneza hela toka kwako...wanapima hawaoni kitu lakini for the sake of selling medicines wanakuambia una Malaria, wengine wanaambiwa na daktari kabisa kuwa wana Malaria Sugu (jaribu kumdadisi, ana maana gani akikuambia una Malaria Sugu?)...ulijaribu kubadili hospitali/madaktari tangu enzi hizo za ujana wote wakakupima na kukupa majibu hayo hayo ya Malaria Sugu?
Watu tunaoishi katika maeneo yenye Malaria (Malaria Endemic areas) huwa tunapata aina fulani ya kinga (natural immunity) dhidi ya Malaria. mara nyingi hii hudevelop kwa watu wanaoishi maeneo hayo tangu utoto, na wakaugua Malaria mara kadhaa utotoni. hata hivyo, si kila mtu aishiye kwenye hayo maeneo atapata natural immunity hiyo. We umezaliwa na kuishi utoto wako hapa kwetu (Tanzania) hasa sehemu za Pwani, Morogoro, kanda ya Ziwa...mara chache unapata immunity hiyo sehemu za Nyanda za juu (kusini na kaskazini) na sehemu za baridi sana, kwa sabau huko rate ya kuugua Malaria ni ndogo.
Jiulize hayo maswali kabla hujajivika ugonjwa wako 'Malaria Sugu' ....chunguza, usije kuta una tatizo kubwa kuliko hilo la Malaria, ukalizembea kwa kuridhika kuwa ni malaria sugu tu!
NB: Namna nyingine ya kuongeza kinga dhidi ya ugonjwa (zaidi ya natural immunity) ni kwa kutumia chanjo. Chanjo ya Malaria haijathibitishwa bado, japo imeonyesha matokeo mazuri katika majaribio. Kwa sasa hamna chanjo, hivyo hamna namna ya kuongeza immunity dhidi ya Malaria, zaidi ya natural immunity.