Wana JF naomba msaada wenu, ni takribani mwaka sasa sijawahi kupata nafuu kutokana na huu ugonjwa. Je tatizo hili lipo au ni mimi tu? Nimetumia dawa nyingi, za hospital mpaka mitishamba, huwa napata nafuu ya muda mfupi na ugonjwa unarudi tena. Kwa yeyote mwenye kuijua tiba ya uhakika anijulishe.Nipo DSM, asanteni
Tindikali...labda nikuulize swali, umejuaje kuwa unaugua malaria sugu? Kila ukijisikia dalili unaenda hospitali kufanya kipimo cha malaria ukaambiwa una malaria kweli na labda wadudu wangapi? Kwa sababu dalili za malaria zinatokea pia kwa maginjwa mengine meengi tu, inaweza isiwe malaria kama hukufanya kipimo husika kikathibitisha.
Vile vile...ili kusema malaria ni sugu, ni lazima upime malaria ithibitike (kipimo cha slide ya kioo na darubini) kisha upewe dawa, na utumie dozi sahihi kama ulivyo andikiwa na daktari..kisha ukimaliza dozi upime tena malaria, kama itaoneka basi hapo waweza sema una malaria sugu na hizo dawa zimeshindwa kukutibu. Kifupi na hapo mfano hujatumia dozi ipasavyo, hujamaliza dozi, hujapima baada ya kumaliza dozi..huwezi kusema ni malaria sugu.
Kuna wakati tunapata malaria mara kwa mara (new infection) halafu tunalaumu ni malaria sugu...mfano, unapata dalili za malaria, unaenda hospitali na inathibitika ni malaria, unapewa dawa unatumia ipasavyo, unapona...kisha unarudi kwenye tabia/mazingira yako ya kawaida ya kutojikinga na malaria, unapata malaria upya (new infection)...hiyo sio malaria sugu, ni malaria mpya ambayo inabidi utibiwe.
Pia kuna dawa nyiingi sana za malaria ambazo zimeshazuiwa kutumika kutibu malaria kwa sababu wadudu wa malaria wamepata usugu dhidi ya dawa hizo..mfano Chloroquine, SP, na baadhi ya dawa zisizo mseto mfano Amodiaquine, Arinate, Artesunate (vidonge) etc ambazo pekee bila kujumlisha dawa nyingine ufanisi wake ni mdogo. Lakini hizi bado zinapatikana kwa wingi kwenye pharmacy, maduka ya dawa, na zhanati binafsi. Hizi zimeshathibitishwa kutotibu malaria kwa ufanisi, lakini utakuta baadhi ya madaktari au wagonjwa wanazing'ang'ania.
Dawa zilizothibitishwa kuwa na ufanisi wa juu kutibu malaria (hata malaria sugu) ni dawa mseto mfano Coartem/ALu, DuoCotexcin, na zisizo mseto Quinine (sindano na vidonge), Artemether (sindano) na Artesunate (sindano). Kuna nyingine nyiingi zipo kwenye majaribio au zimeshamaliza majaribio lakini ni za jamii ya Artemisinin mseto.
Ushauri wangu....zingatia hayo niliyosema hapo juu ili utambue kuwa ni malaria kweli au tatizo jingine? kama ni malaria, ni sugu au new infection? Kisha muone daktari atakupatia matibabu na ushauri jinsi ya kujikinga..na malaria haitakusumbua tena.
NB: MALARIA INAUA KULIKO HATA UKIMWI, SI WATOTO TU..HATA WATU WAZIMA. KUWA MAKINI NA HUO UGONJWA.