Malaria sugu kwa mwanangu!

Malaria sugu kwa mwanangu!

wende

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2009
Posts
714
Reaction score
66
Nina mtoto wa mwaka 1 na miezi mi2 todate. For the 1st time,aligundulika na malaria 5 akatibiwa na kupata nafuu kabisa. Miezi mi2 baadaye akaanza kuonekana na dalili za malaria. Alipimwa again akakutwa na malaria 3. Akatibiwa,once again baada ya kama miezi mi2 ivi akaugua the same na kukutwa na malaria 2! This time tukashauriwa atumie sindano,akachomwa sindano 5 za quinin. Juzi tena ameonekana na dalili za malaria,alivyopimwa this time amekutwa na malaria 1 na amepewa quinin ya syrup. We dont know what is next!
To you doctors na wote wenye uzoezi na this terrible parasite,naombeni ushauri nifanye nini?
NB:Nahisi hili tatizo limemrudisha nyuma sana ata kutembea kwa sababu at this age bado hawezi to walk on her own,,,,anatembea by being supported na vitu kama vile baiskeli ya tairi 3 ya watoto,tables,walls,makochi n.k.
Kwa heshima,nawasilisha.
 
pole sana.kama mzazi mtoto akiumwa unakuwa hauna raha.haya wenye tiba humu msaidieni.jee dokta alikushauri nini?
 
jaribu kumpa vyakula bora ambavyo vinasaidia kuimarisha immune system yake mwilini.watoto wakiwa wadogo,kinga zao zinakuwa sio imara kama watu wazima.pole maybe utapata msaada
 
Jitahidi umsagie anywe kwa maji au maziwa mbegu za mlonge kila siku at least for 1month itakua kinga,pia mpime uti,masikio kama yana infections
 
pole sana.kama mzazi mtoto akiumwa unakuwa hauna raha.haya wenye tiba humu msaidieni.jee dokta alikushauri nini?
Asante sana. Dota anasema,hali kama hiyo kwa watoto kama hawa ni ya kawaida tu na kwamba yataisha tu!!
 
Jitahidi umsagie anywe kwa maji au maziwa mbegu za mlonge kila siku at least for 1month itakua kinga,pia mpime uti,masikio kama yana infections
Haya na asante kwa ushauri wako!
 
jaribu kumpa vyakula bora ambavyo vinasaidia kuimarisha immune system yake mwilini.watoto wakiwa wadogo,kinga zao zinakuwa sio imara kama watu wazima.pole maybe utapata msaada
Asante kwa ushauri wako. Upo sahihi kabisa!
 
pole sana.kama mzazi mtoto akiumwa unakuwa hauna raha.haya wenye tiba humu msaidieni.jee dokta alikushauri nini?
Dokta anasema hii ni hali ya kawaida tu kwa watoto kama hawa na kwamba haya malaria yataisha tu!
 
Nenda kwenye duka la wahindi la madawa, labda sijui upo mkoa gani... Maana yana majina tofauti! Mwambie akupe ZANDU ya malaria sugu kwa ajili ya mtoto! Pia wakati unatumia zandu anza kumpa mlonge atlest mbegu mbili daily! Pia kama una kauwezo mpatie juice za nutrients za forever living Alovera Gely na ile development ya kuchanganyia kupunguza uchungu, Kama vp ni pm nikuunganishe na mtaalamu Wa dozi za forever living.
 
Pole sana wende.

Kwa mtoto wa mwaka na miezi miwili kushindwa kutembea mwenyewe sio tatizo. Kila mtoto huwa anaatiba yake ya kuweza kutembea, kuongea etc. Hivyo swala la mtoto wako kutokuanza kutembea mapema kama ulivyotarajia lisiwe lenye kukupa shaka.

Kuhusu malaria. Kwanza naomba kujua huyo mtoto huwa unampima katika kituo hicho hicho kimoja? Je, huwa wanatumia njia gani kumpima?
Ushauri wangu ni huu: mpeleke mtoto kupima katika vituo viwili au vitatu tofauti kwa njia ya microscope na njia ya RDT (Rapid diagnostic test). Angalia kama majibu yote yanaonyesha ni malaria na kama kiwango chake kinafanana.

Mtoto kuwa na vidudu vya malaria haimaanishi kuwa homa au dalili nyingine alizo nazo zinakuwa lazima zimesababishwa na uwepo wa hivyo vidudu. Kwa mfano mtoto anaweza kuwa na malaria na UTI au ugonjwa mwingine kwa pamoja. Katika hali kama hiyo, iwapo utanendelea kutibia malaria tu, ugonjwa mwingine unapata fursa ya kuwa sugu. Kwa hiyo, kwa mtoto wako kuna haja ya kutafuta sababu nyingine zinazoweza kuwa zimesababisha kuumwa kwake.

Pata ushauri wa daktari ambaye atampima mtoto.
 
Nenda kwenye duka la wahindi la madawa, labda sijui upo mkoa gani... Maana yana majina tofauti! Mwambie akupe ZANDU ya malaria sugu kwa ajili ya mtoto! Pia wakati unatumia zandu anza kumpa mlonge atlest mbegu mbili daily! Pia kama una kauwezo mpatie juice za nutrients za forever living Alovera Gely na ile development ya kuchanganyia kupunguza uchungu, Kama vp ni pm nikuunganishe na mtaalamu Wa dozi za forever living.
Nakushukuru sana kwa ushauri wako na yote haya nitayafanyia kazi ASP!!
 
Nenda kwenye duka la wahindi la madawa, labda sijui upo mkoa gani... Maana yana majina tofauti! Mwambie akupe ZANDU ya malaria sugu kwa ajili ya mtoto! Pia wakati unatumia zandu anza kumpa mlonge atlest mbegu mbili daily! Pia kama una kauwezo mpatie juice za nutrients za forever living Alovera Gely na ile development ya kuchanganyia kupunguza uchungu, Kama vp ni pm nikuunganishe na mtaalamu Wa dozi za forever living.
Mimi nipo Kishapu - Shinyanga.
 
Pole sana wende. Kwa mtoto wa mwaka na miezi miwili kushindwa kutembea mwenyewe sio tatizo. Kila mtoto huwa anaatiba yake ya kuweza kutembea, kuongea etc. Hivyo swala la mtoto wako kutokuanza kutembea mapema kama ulivyotarajia lisiwe lenye kukupa shaka. Kuhusu malaria. Kwanza naomba kujua huyo mtoto huwa unampima katika kituo hicho hicho kimoja? Je, huwa wanatumia njia gani kumpima? Ushauri wangu ni huu: mpeleke mtoto kupima katika vituo viwili au vitatu tofauti kwa njia ya microscope na njia ya RDT (Rapid diagnostic test). Angalia kama majibu yote yanaonyesha ni malaria na kama kiwango chake kinafanana. Mtoto kuwa na vidudu vya malaria haimaanishi kuwa homa au dalili nyingine alizo nazo zinakuwa lazima zimesababishwa na uwepo wa hivyo vidudu. Kwa mfano mtoto anaweza kuwa na malaria na UTI au ugonjwa mwingine kwa pamoja. Katika hali kama hiyo, iwapo utanendelea kutibia malaria tu, ugonjwa mwingine unapata fursa ya kuwa sugu. Kwa hiyo, kwa mtoto wako kuna haja ya kutafuta sababu nyingine zinazoweza kuwa zimesababisha kuumwa kwake. Pata ushauri wa daktari ambaye atampima mtoto.
Ahsante sana Zemarcopolo kwa ushauri wako.Nishampeleka kwa madaktari kama wa3 ivi ila wote si specialists wa watoto kutokana na mazingira nilipo yaani shinyanga vijijini. Ktk hao,wa1 ndo hakuona kitu kabisaa wakati wa 2 ndo akagundua hiyo malaria5. Wa3 ndo kagundua hiyo malaria 3,2 na 1. Kuhusu namna wanavyopima sielewi,maana utakuta dokta anachukua damu ktk kidole na baadae anakuletea majibu. Sure at the time being,itabidi tucheki na magonjwa mengine kama vile UTI na kupata ushauri zaidi kwa doktari anayempima mtoto. Thanks indeed kwa ushauri wako wa kitaabibu!
 
kwa mtoto mdogo wa miaka 1.2 kutumia dawa kali kama hizo (quinine) na kwa kipindi kirefu hiyo pia ni Tatizo. Tatizo sasa siyo malaria bali ni sumu ya hizo dawa. Hospital ya mkoa au Bugando wanaweza kukusaidia kikamilifu kuliko zahanati au hawa jamaa wa pharmacy. Meanwhile mpe fresh orange juice (kamua mwenyewe na dilute by water 1:1)na maji masafi kwa wingi.
 
madoctor hapa itabidi muwaongeze posho,bado sijaona wazo hata moja la maana la kumsaidia huyo mtoto,mama mwenye mtoto nenda kamface doctor maalum kwa magonjwa ya watoto katika hospitali yoyote uliyokaribu nayo ili uwe na amani na kile kinachoendelea hata mtoto akizidiwa haitokulazimu urudi humu jamii forums umuulize aliekushauri nini ufanye:wink:!!
 
kwa mtoto mdogo wa miaka 1.2 kutumia dawa kali kama hizo (quinine) na kwa kipindi kirefu hiyo pia ni Tatizo. Tatizo sasa siyo malaria bali ni sumu ya hizo dawa. Hospital ya mkoa au Bugando wanaweza kukusaidia kikamilifu kuliko zahanati au hawa jamaa wa pharmacy. Meanwhile mpe fresh orange juice (kamua mwenyewe na dilute by water 1:1)na maji masafi kwa wingi.
Thanks George. Noted!
 
Back
Top Bottom