Tujifunze zaidi, hata kama unafanya data extraction, hizo data hutoi nyumbani kwako labda huko unakofanyia utafiti hakuna governig board. Huwezi kukwepa consent kwa kusema unachukua tu data zilizopo, hiyo taasisi gani utaingia tu bila kibali au wewe consent unafikiri ni kwa mhusika wa moja kwa moja/physical tu? (Data extraction consent inahusika).
Pia, nimezungumzia consent hapo kabla ili mtu aweze kufanya utafiti kwenye jamii mchanganyiko ( kwa msingi wa parterity issues). Je sheria zinazuia kufanya utafiti husika kwa 100%?
Pamoja na hilo hapo juu, hii si sababu ya kitafiti kukuruhusu kutumia watu wanaokuja kwako wakiwa tayari na wasiwasi/malalamiko ya kuwa si wazazi wa watoto na baada ya hapo kutumia majibu husika kama sample ya jamii nzima. Hakuna utafiti wa aina hiyo. Sample unayoitumia ni BIASED TAYARI kwenye conclusion yako/target population. Hii inajibia watue wenye malalamiko tu. ndo maana nikakwambia ukasome kuhusu study population vs target population.
Data unazozipata kwenye SAMPLE YAKO, uliyoitoa kwenye STUDY POPULATION zinaenda kuzungumzia TARGET POPULATION IPI/jamii gani kwa ujumla ya wahusika?
Huwezi kuchukua watu wanaokuja kwenye kituo chako cha afya wakiwa wana homa ukawapima malaria, kiasi cha watu utakaowakuta na malaria dhidi ya utakaowakuta hawana unatafuta asilimia na unasema asilimia hiyo ya watu wa eneo husika wana malaria!!!???
Sijui kama unafanya tafiti au ulisoma na kuondoka?
Ukizungumzia bias kwenye kufanya utafiti mpya, hakuna utafiti utaufanya chini ya jua bila bias. Isipokuwa wewe ndo unatakiwa kujenga mazingira ya kupunguza hizo bias. mfano: data extraction bias: Unclear forms/tools, selective reporting and single reviewer errors.