MALAWI: Asilimia 80 ya wanaume waliopima DNA wagundulika sio baba wa watoto


Tatizo tafiti hazikubali assumption zako, swali ni kupima DNA ni unethical issue?? Au utahitaji kuijengea mazingira ya utafiti husika.

Kazi ya consent/ridhaa kwenye utafiti ni nini?
 
hao tayari walikua na mashaka kuhisi watoto si wao hivyo wakaenda kuthibitisha kwa DNA inaonyesha 80% kweli si wao


wamekwambia sample ya kawaida inaonyesha 90% ni watoto wao kweli
 
hao tayari walikua na mashaka kuhisi watoto si wao hivyo wakaenda kuthibitisha kwa DNA inaonyesha 80% kweli si wao


wamekwambia sample ya kawaida inaonyesha 90% ni watoto wao kweli
Wababa wakiwa na shaka ya watoto kuwa si wao, wakipeleka kupima 80% inakuwa kweli si wao. Wakati wababa wanaokwepa majukumu wakipelekwa kupimwa 90% wanakutwa ni wazazi halisi wa watoto.
 
Nazan naongea na mtu ambae uwezo wake ni mdogo, mambo ya consent hayana uhalisia Kwenye data kama hzo ukiondoa kutaja majina sample public

Uwezi ukipata sampling ya DNA kwa kutafuta data mpya zaid ya kutumia zilizopo

Maana lolote utalofamya lazma liwe na bias na halitaleta majibu sahihi

Nazan kwanza ukajifunze aina za research
 


Tujifunze zaidi, hata kama unafanya data extraction, hizo data hutoi nyumbani kwako labda huko unakofanyia utafiti hakuna governig board. Huwezi kukwepa consent kwa kusema unachukua tu data zilizopo, hiyo taasisi gani utaingia tu bila kibali au wewe consent unafikiri ni kwa mhusika wa moja kwa moja/physical tu? (Data extraction consent inahusika).

Pia, nimezungumzia consent hapo kabla ili mtu aweze kufanya utafiti kwenye jamii mchanganyiko ( kwa msingi wa parterity issues). Je sheria zinazuia kufanya utafiti husika kwa 100%?

Pamoja na hilo hapo juu, hii si sababu ya kitafiti kukuruhusu kutumia watu wanaokuja kwako wakiwa tayari na wasiwasi/malalamiko ya kuwa si wazazi wa watoto na baada ya hapo kutumia majibu husika kama sample ya jamii nzima. Hakuna utafiti wa aina hiyo. Sample unayoitumia ni BIASED TAYARI kwenye conclusion yako/target population. Hii inajibia watue wenye malalamiko tu. ndo maana nikakwambia ukasome kuhusu study population vs target population.

Data unazozipata kwenye SAMPLE YAKO, uliyoitoa kwenye STUDY POPULATION zinaenda kuzungumzia TARGET POPULATION IPI/jamii gani kwa ujumla ya wahusika?

Huwezi kuchukua watu wanaokuja kwenye kituo chako cha afya wakiwa wana homa ukawapima malaria, kiasi cha watu utakaowakuta na malaria dhidi ya utakaowakuta hawana unatafuta asilimia na unasema asilimia hiyo ya watu wa eneo husika wana malaria!!!???

Sijui kama unafanya tafiti au ulisoma na kuondoka?

Ukizungumzia bias kwenye kufanya utafiti mpya, hakuna utafiti utaufanya chini ya jua bila bias. Isipokuwa wewe ndo unatakiwa kujenga mazingira ya kupunguza hizo bias. mfano: data extraction bias: Unclear forms/tools, selective reporting and single reviewer errors.
 
Huu upupu uloandika hapa hakuna taasisi yoyote iliyowahi fanya hivo kwenye angle ya DNA na AIDS

Wote wanatumia secondary data
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…