Malawi: Kupokea shahada ya Heshima hakumfanyi Mtu kustahili Cheo cha "Profesa" au "Daktari."

CC. Mama
 
Kama Mwalimu angekuwa anapenda hizi sifa za kijinga, basi angejiita/angeitwa Daktari Dokta Dr. Doctor..................... J K Nyerere! Maana katika utumishi wake alipewa zaidi PhD 20 za heshima na vyuo vikuu tofauti kote duniani!

 
Kenya kuna phd holders wengi sana East.africa ila hawaitwi dr. Ruto mwenyewe ni phd holder.

Kikwete pia.wamuite Mr President sio Daktari tena watu wa TBC.
 
Hii nchi inajidhalilisha kwa mengi, hivi kuna rais marekani aliwahi kuitwa Dr, sijui Prof, . Ulimbukeni mbaya sana
 
Eti Dokta Samia!? Kuna heshima ya juu kama kuwa Rais!?
 
Tanzania karibua 3/4 ya wananchi wana hadhi ya udaktari wa heshima!
 
Wenye elimu ya hapa na pale ambao hata vyuo walivyosoma havijulikani wakienda Malawi wanaitwa Ndugu tu. Ndugu. Hangaya karibu Lilongwe 😂
 
Obama ana Masters, hana Ph.D. Ni Rais mmoja tu wa Marekani alikuwa na Ph.D. Wengi wana Masters na wengi hawakupata elimu ya Chuo. Badala ya Obama ungetoa mifano ya watu kama Nyerere ( mpaka mwisho alitaka aitwe Mwalimu), Desmond Tutu, Nelson Mandela ambao hawakutaka kabisa mambo ya u Dokta.

Amandla...
 
Mara nyingi vilaza ndio wapenda sifa
 
Hiyo iwafikie TBC maana ndo wanapenda kueneza sifa hizo kwa wanasiasa ili kujipendekeza wapate teuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…