Yea na kuna vichaa watz hapa ambao wanacomment kuhusu suala ambalo hawajalielewa hata kidogo. Kisa lugha gongana, alafu wameamua kufa nayo hivyo hivyo, tu mithili ya mtu anayesoma gazeti juu chini. [emoji1] Kiswahili kinatosha pia, wapo wengi humu ambao wanaweza wakawapa tafsiri, acheni ubishoo. KQ wameulizia kuhusu uwezekano wa usafiri wa anga kurejea nchini Malawi, wakiwa na nia ya kuanza safari zao. Ila wamalawi wakajibu kwamba hawajafungua anga zao kwa ndege zozote kutoka nje ya Malawi. Wanasema kwa sasa bado wanaendelea na shughuli za kuwezesha usafiri wa anga ambao utatilia maanani tahadhari dhidi ya maambukizi ya COVID-19. Eti KQ imepigwa stop, kwani ATCL au hata ET na Emirates wamekubaliwa? [emoji1] Si huwa mnafunzwa kwa kiingereza kuanzia kidato cha kwanza? Sasa nikisema kwamba wote ambao hamkuelewa hata sentensi moja tu ya barua hiyo ni madrop out wa darasa la saba nimekosea? [emoji1]