Malcom Lumumba Live: Tusemezane...

kujua mambo mengi kama ww nizingatie nini hasa
Mkuu,
Ukitaka kufanikiwa kwenye maish haya ni lazima ujitambue wewe binafsi kuliko mtu yeyote yule. (Know you)

Usitamani kuwa kama Malcom Lumumba.
Naamini kwamba wewe una kitu cha ziada ambacho hakuna mwanadamu mwingime ambaye anacho hapa duniani. Hicho ndicho uanze kukifanyia kazi.

Ukishafanikiwa kujua nini unaweza kufanya hapo sasa ndiyo unaanza kujifunza vitu vipya kwa kusoma sana, kujihusisha na watu wapya na pia kutafuta muda peke yako wa kutafakari vitu ilivyoviingiza kichwani ili uone lipi litakusaidia au linahusiana na maisha yako au kipaji chako.

NB: Jifunze kuwa msikilizaji sana na siyo msemaji, kwenye mambo muhimu tafuta watu wenye uwezo kukushinda wewe. Nasisitiza tena "spare some time alone to meditate and reflect your life"
 
Watu wa Linguistics kuna ishu wanaita Speech community.

Unaweza kujua huyu ni mwanasheria kwa urahisi, huyu ni kijana wa uswahilini kwa urahisi, huyu kakulia ushuwani kiurahisi.

Ila sio kila siku.

Indeed mkuu!
Uko sawa kabisa katika hili.
Nimefurahi uliposema "ila siyo kila siku"
 
Indeed mkuu!
Uko sawa kabisa katika hili.
Nimefurahi uliposema "ila siyo kila siku"
Nilitaraji kama kawaida yako ukipewa title unashuka nondo[speech community].

Kuna uzi jukwaa la international mlikuwa mnajadili uhalali wa Israel palestina[Yerusalemu] traced back kwa Ibrahim. nilipick mambo ila sikujua msimamo wako
 
Nilitaraji kama kawaida yako ukipewa title unashuka nondo[speech community].

Kuna uzi jukwaa la international mlikuwa mnajadili uhalali wa Israel palestina[Yerusalemu] traced back kwa Ibrahim. nilipick mambo ila sikujua msimamo wako
Hahaha Daby bwana,
Kwenye ishu ya Palestina msimamo wangu ni wazi kabisa. Palestina ni lazima ipewe Statehood kwasababu wamezaliwa pale na hawana mahali pa kwenda zaidi ya pale.

Wayahudi nao wakae pale,
Kwasababu hawana mahali pengine kwenda.
Wakienda Ulaya watu wanatamani kuwaua kabisa.

Hivyo tunaweza kurudi kwenye msimamo wa two State Solution with Jerusalem as a neutral sacred city for both states.

NB: One State Solution haiwezekani mpaka hapa tulipofika. Hakuna anayekubali kushuka.
 

Got you,

kila mmoja ana claim ni holy city kwa imani yake. UN walishaliona hili pia ndiyi maana hawataki kinachoitwa one state.

Mambo yalivurugika pale mmoja alipopewa mmalaka ya kumpiga mwenzake yeye akalie pa mwenzake[bible].

[emoji125] [emoji125]
 

Tuko pamoja mkuu....
 
Tufanyeje ili tuweze kuwa na mijadala au mabandiko yenye uzito kwa jamii ya JF ??
(Hasa kule IF na JI, tutumie lugha ya malkia labda, au tuandike kwa lugha ya kiswahili au njia yoyote ile ili kuwafikia watanzania kwa kiasi kikubwa)
Kama lengo Ni Kuwafikia Watanzania Bass Itumike Lugha Asili Ya Kitanzania
 
RC Olesendeka mbona anamsakama Mwenyekiti Mh Magufuli hivyo? Tena kwa rugha yao ya kimasai...nini kinaendelea ndani ya chama?
 
RC Olesendeka mbona anamsakama Mwenyekiti Mh Magufuli hivyo? Tena kwa rugha yao ya kimasai...nini kinaendelea ndani ya chama?
Teh teh teh teh,
Mimi sifahamu kabisa mkuu!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Teh teh teh teh,
Mimi sifahamu kabisa mkuu!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Mkuu kuna clip nimeshindwa kuattach hapa ameongea vibaya kuhusu Mwenyekiti...clip imesambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii.

Sasa najiuliza Magu kamkosea nini jamani huyu, shukrani ya punda ni mateke sio...
 
Mkuu kuna clip nimeshindwa kuattach hapa ameongea vibaya kuhusu Mwenyekiti...clip imesambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii.

Sasa najiuliza Magu kamkosea nini jamani huyu, shukrani ya punda ni mateke sio...
Kama kweli amemkashifu Mwenyekiti basi hatua stahiki za kinidhamu zitafuatwa ndani ya chama chake.

NB 1:Kikubwa zaidi ni kwamba kama haridhiki na utendaji wa serikali yake basi aachie ngazi kwa wengine ambao wanaweza kwendana na matakwa ya chama chake.

Kutokukubaliana na mwenyekiti au kiongozi huwa inatokea sana na siyo mara ya kwanza.
Lakini kiutawala, kama wewe ni kiongozi ndani ya Serikali ni lazima ujue kwamba maamuzi ya Baraza au Serikali ni ya kwenu wote kama viongozi.

Ukitaka usihusishwe na hayo maamuzi basi achilia madaraka ubakie kuwa mwanachama wa kawaida ili tubaki na kumbukumbu kwamba wewe ulikosea tu.

NB 2: Miaka ya nyuma Mzee Kingunge alipishana na chama chake katika mambo fulani wakati akaamua kuachilia madaraka.

Ikithibitika kafanya hivyo basi,
Itakuwa siyo uungwana kiutawala.....
 
Ufafanuzi murua Mkuu! Good night Malcom
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…