Mkuu hili siyo dhumuni la uzi huu,
Lakini kwasababu umeuliza ngoja nijitahidi kukujibu kwa kadiri ya uwezo wangu.
Mosi,
Korea Kaskazini anatamani sanaa kuungana na Korea Kusini. Ukweli ni kwamba mbali na yote haya wale wawili ni ndugu wa damu na hata mgawanyiko wao ulitokana na mataifa ya nje.
Ushahidi wa hili ni ile vita ya mwaka 1950-1953 ambayo Korea Kaskazini aliianzisha dhidi ya Korea Kusini ili aziunganishe nchi zote mbili kuwa moja. Kwasababu wakati wa Vita ya pili ya dunia Korea ilikuwa chini ya Japan na baada ya Japan Kushindwa basi The Grand Alliance (Marekani, Urusi na Uingereza) wakaigawa Kaskazini na Kusini na kuwela mpaka uitwao 38th Parallel.
Hivyo tangia siku ile Korea zote mbili japo ni maadui lakini bado wanatamani sana kuungana kama ndugu. Sema tatizo ni kwamba mataifa makubwa yananufaika na ule ugomvi.
NB: Kim kutaka mawasiliano na Korea Kaskazini siyo dalili ya woga bali ni dalili ya uungwana kwasababu maongezi ya namna hii hayajaanza leo hii. Isitoshe leo mchana Serikali ya Kim imesema haya maongezi hayawahusu mataifa makubwa kabisa na wasijaribu kusogea.
Pili,
Utawala wa Kim hauwezi kuogopa kipindi hiki kwasababu wanajua kabisa Marekani siyo mjinga kuwavamia. Vikwazo vya Umoja wa mataifa haviwadhuru kabisa na imeshashuhudiwa kwamba Warusi na Wachina wanamsaidia sana Korea Kaskazini kukwepa vikwazo vya kiuchumi.
Ili Marekani aweze kuvamia Korea Kaskazini kwa njia ya Kijeshi inabidi apeleke Muswada kwenye Baraza la Ulinzi na Usalama ili wapitishe azimio la Uvamizi wa Kijeshi kama walivyofanya kule mwaka Libya. Bahati mbaya sana Wachina na Warusi hawawezi kuruhusu hicho kitu kwasababu wanajua madhara yake.
Tatu,
Korea Kaskazini mbali na ujinga wote ule ina kiongozi mwenye upeo mkubwa na dunia pia ni Kijana. Ukweli ni kwamba anafahamu ili Korea iweze kutoka hapo ilipo itahitaji kufanya mabadiliko makubwa sana kimfumo. Hawawezi kutegemea Urusi na Uchina kila siku.
Vurugu zote hizi za Kim ni kutafuta kukaa mezani na mataifa makubwa ili yamhakikishie usalama wake kama ambavyo alifanyika miaka ya 1996 na baba yake. Lakini bahati mbaya Marekani hataki kukaa meza moja na Korea kwasababu itaonyesha udhaifu na itakuwa na madhara makubwa kwenye diplomasia yake.
Kim anajua kwamba ana muda mrefu sana kutawala, na ili afike mbali anahitaji kujenge uchumi wa nchi yake hivyo njia mbadala ni kutafuta mbinu za kujiepusha na kutengwa kwa nama yoyote ile. (Political Isolation)
NB: Aanchokifanya Kim ndicho anachokifanya yule bwana mdogo wa Saudi Arabia, kuna baadhi ya vitu analegeza ili nchi yake ifike mbali kiuchumi kwasababu huwezi kuwategemea Marekani na Mafuta tu kila siku. Ameahidi hadi kuruhusu wanawake kufanya baadhi ya mambo ambayo wanakatazwa.
Haya machache tu mkuu.....