Malcom Lumumba Live: Tusemezane...

Malcom Lumumba Live: Tusemezane...

Heri ya mwaka mpya.
Binafsi sina swali ila napenda kukupongeza kwa kwazi zako mkuu. Wewe ni miongoni mwa watu ninaowakubali humu jf kwa kutoa nyuzi makini.

HONGERA MKUU
 
Sawa mkuu. Ila sijazungumzia uzuri, style and design, kuna design za vijana kama zile wanaita Supra halafu nyekundu.
Hahaha,.
Sivai Supra mkuu.
Huwa navaa viatu vya mazoezi na buti tu.
 
Heri ya mwaka mpya.
Binafsi sina swali ila napenda kukupongeza kwa kwazi zako mkuu. Wewe ni miongoni mwa watu ninaowakubali humu jf kwa kutoa nyuzi makini.

HONGERA MKUU
Ahsante sana mkuu.
Appreciate this ....
 
Mungu yu mwema kwanza heri ya mwaka mpya na kwako pia mm nina kaswali kangu kadogo tu kama kameulizwa huko utanisamehe nilikua natamani kukuuliza hili swali bora umetupa uwanja

Una miaka mingapi? huwa nawaza kama mtu mzima flani hiviii yaan usiyependa kuzeeka ni hilo tu hata ukiwa kaben10 niambie tu
 
Mkuu,
Ukitaka kufanikiwa kwenye maish haya ni lazima ujitambue wewe binafsi kuliko mtu yeyote yule. (Know you)

Usitamani kuwa kama Malcom Lumumba.
Naamini kwamba wewe una kitu cha ziada ambacho hakuna mwanadamu mwingime ambaye anacho hapa duniani. Hicho ndicho uanze kukifanyia kazi.

Ukishafanikiwa kujua nini unaweza kufanya hapo sasa ndiyo unaanza kujifunza vitu vipya kwa kusoma sana, kujihusisha na watu wapya na pia kutafuta muda peke yako wa kutafakari vitu ilivyoviingiza kichwani ili uone lipi litakusaidia au linahusiana na maisha yako au kipaji chako.

NB: Jifunze kuwa msikilizaji sana na siyo msemaji, kwenye mambo muhimu tafuta watu wenye uwezo kukushinda wewe. Nasisitiza tena "spare some time alone to meditate and reflect your life"
Wow....
 
Mungu yu mwema kwanza heri ya mwaka mpya na kwako pia mm nina kaswali kangu kadogo tu kama kameulizwa huko utanisamehe nilikua natamani kukuuliza hili swali bora umetupa uwanja

Una miaka mingapi? huwa nawaza kama mtu mzima flani hiviii yaan usiyependa kuzeeka ni hilo tu hata ukiwa kaben10 niambie tu

Ahsante sana Shunie,
Umenichekesha sana ndugu yangu.
Mimi ni ntu mzima lakini siogopi kuzeeka hataa!

Nakuwa hivi unavyoniaona hapa kwasababu naamimi ili mwanadamu ufurahie Maisha hapa duniani ni lazima uwe na uone mpana usio na mipaka katika kila jambo.

My life is simply connected and deeply imbedded to a great pond called LIFE OF PURPOSE. Hivyo nafurahia sana busara za Uzee na Kuipenda kufikiri kama mzee, huku nikimuomba Mola anipe nguvu ya kufanya kazi na kutimiza majukumu kama kijana mdogo na mwishowe kabisaa nafurahia maisha kama kitoto kichanga ambacho hakifikirii matatizo ya leo na kutoyaogopa majanga ya kesho..

NB: Nisipokuwa hivi basi sintakuwa MALCOM LUMUMBA unayeniona leo hii,...Life has many faces and my heart is just passionate to see reflect all of them at once.
 
Asante sana nimekuelewa vizuri kwahiyo unaweza kuwa sawa na babu yake keanu lemutuz eenh usinichoke jaman
 
Wewe ni kati ya wanaJF makini chifu bila shaka unasoma saana kama hausomi saana basi wewe ni mhadhiri kama sio

mhadhiri basi mwandishi wa habari kama zile za kina Jeff koinange[wa kipindi kile cha Niger lakini] bila kumsahau izzo.

Lengo sio kutaka kukujua nakupa hongera tu.
Hizi sifa unataka nini?
 
Mkuu hili siyo dhumuni la uzi huu,
Lakini kwasababu umeuliza ngoja nijitahidi kukujibu kwa kadiri ya uwezo wangu.

Mosi,
Korea Kaskazini anatamani sanaa kuungana na Korea Kusini. Ukweli ni kwamba mbali na yote haya wale wawili ni ndugu wa damu na hata mgawanyiko wao ulitokana na mataifa ya nje.

Ushahidi wa hili ni ile vita ya mwaka 1950-1953 ambayo Korea Kaskazini aliianzisha dhidi ya Korea Kusini ili aziunganishe nchi zote mbili kuwa moja. Kwasababu wakati wa Vita ya pili ya dunia Korea ilikuwa chini ya Japan na baada ya Japan Kushindwa basi The Grand Alliance (Marekani, Urusi na Uingereza) wakaigawa Kaskazini na Kusini na kuwela mpaka uitwao 38th Parallel.

Hivyo tangia siku ile Korea zote mbili japo ni maadui lakini bado wanatamani sana kuungana kama ndugu. Sema tatizo ni kwamba mataifa makubwa yananufaika na ule ugomvi.

NB: Kim kutaka mawasiliano na Korea Kaskazini siyo dalili ya woga bali ni dalili ya uungwana kwasababu maongezi ya namna hii hayajaanza leo hii. Isitoshe leo mchana Serikali ya Kim imesema haya maongezi hayawahusu mataifa makubwa kabisa na wasijaribu kusogea.

Pili,
Utawala wa Kim hauwezi kuogopa kipindi hiki kwasababu wanajua kabisa Marekani siyo mjinga kuwavamia. Vikwazo vya Umoja wa mataifa haviwadhuru kabisa na imeshashuhudiwa kwamba Warusi na Wachina wanamsaidia sana Korea Kaskazini kukwepa vikwazo vya kiuchumi.

Ili Marekani aweze kuvamia Korea Kaskazini kwa njia ya Kijeshi inabidi apeleke Muswada kwenye Baraza la Ulinzi na Usalama ili wapitishe azimio la Uvamizi wa Kijeshi kama walivyofanya kule mwaka Libya. Bahati mbaya sana Wachina na Warusi hawawezi kuruhusu hicho kitu kwasababu wanajua madhara yake.

Tatu,
Korea Kaskazini mbali na ujinga wote ule ina kiongozi mwenye upeo mkubwa na dunia pia ni Kijana. Ukweli ni kwamba anafahamu ili Korea iweze kutoka hapo ilipo itahitaji kufanya mabadiliko makubwa sana kimfumo. Hawawezi kutegemea Urusi na Uchina kila siku.

Vurugu zote hizi za Kim ni kutafuta kukaa mezani na mataifa makubwa ili yamhakikishie usalama wake kama ambavyo alifanyika miaka ya 1996 na baba yake. Lakini bahati mbaya Marekani hataki kukaa meza moja na Korea kwasababu itaonyesha udhaifu na itakuwa na madhara makubwa kwenye diplomasia yake.

Kim anajua kwamba ana muda mrefu sana kutawala, na ili afike mbali anahitaji kujenge uchumi wa nchi yake hivyo njia mbadala ni kutafuta mbinu za kujiepusha na kutengwa kwa nama yoyote ile. (Political Isolation)

NB: Aanchokifanya Kim ndicho anachokifanya yule bwana mdogo wa Saudi Arabia, kuna baadhi ya vitu analegeza ili nchi yake ifike mbali kiuchumi kwasababu huwezi kuwategemea Marekani na Mafuta tu kila siku. Ameahidi hadi kuruhusu wanawake kufanya baadhi ya mambo ambayo wanakatazwa.

Haya machache tu mkuu.....
ahsante kwa maelezo yako mkuu,

kutokana na hali inayoendelea Syria ikiwa kwa asilimia kubwa utawala wa Al Assad umefanikiwa kubaki madarakani,na wameweza kukomboa eneo kubwa toka mikononi mwa waasi na wanamgambo.Ila Marekani wamegoma kuondoka
nini Syria anaweza kufanya kulazimisha Marekani aondoke.

Pia elezea nini kinaendelea Iran na maandamano yake...je kwa maoni yako kuna dalili za kuanguka kwa utawala wa Iran
kama tawala za Iraq na Libya???
 
Back
Top Bottom