Malcom X akipunga upepo Dar es Salaam

Hivi mpaka anafungwa, aliwahi kufikishwa mahakamani kweli ?..

...Na kama wamgemfikisha mahakamani unadhani wangemshitaki kwa kosa gani ?
 
Nianze na maelezo ya picha "Wengi hawajui hili lakini alikuwa akifikia mitaa Gerezani".
Mohamed Said unaweza kunisaidia uelewa kutoka Maktaba yako endapo kuna uhusiano wowote uliopo katika Safari za Malcolm X mitaa ya Gerezani na Gerezani na harakati za uhuru wa Tanganyika/ Siasa za mji wa Dar es Salaam katika miaka ya 1950. Pamoja na kuwa picha haijataja ni ya mwaka gani, lakini maandiko yanaeleza kuwa baada ya kuhitilafiana na mwenzake Elijah Poole a.k.a Elijah Muhammad kuhusu muelekeo na mtizamo wa kisiasa wa Nation of Islam (NoI), Malcolm X aliachia ngazi katika uongozi wa harakati za NoI mwaka 1964 na ni katika kipindi hicho ndipo aliposafiri sana barani Afrika na hata Mashariki ya Kati ambako alienda Hijja na kuitwa el-Hajj Malik el Shabazz.
1. Inawezekana alikuwa akifika Gerezani miaka ya 1950s?,
2. Je, hapo Gerezani alikuwa akipenda kufikia mitaa ipi kati ya Kipata, Kitchwele (Uhuru), Kirk (Lindi), Somali au Kiungani?
3. Nation of Islam ilianzishwa mwaka 1931, Je?, Kuna mahusiano yeyoye kati ya Nation of Islam ya Waamerika Weusi na Chama cha Waislamu wa Tanganyika (Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika) kilichoanzishwa Gerezani mwaka 1933?

Natanguliza shukrani zangu za dhati.
 
Changa...
Ndugu yetu aliandika akiwa na nia ya kunifedhehesha kwa kuwa mimi nimeeleza mengi kuhusu Gerezani katika harakati za TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nami kwa kuwa aliitaja Gerezani yangu nami nikaona nimlipe "in his own coin," ndipo nikamtajia na kumwekea picha nikiwa Harlem, New York mitaa ya Malcolm X kumfanya afikiri.

Na mwengine aliyenipiga kijembe kuwa mie limbukeni wa New York nikamwekea picha niko Paris kumdhihirishia kuwa mbona nimefika kwingi?
 
Wengi hawajui hili lakini alikuwa akifikia mitaa Gerezani.

View attachment 2187679
Kweli Malcom X aliwahi kufika Tz , ila bado nina mashaka kama hapo ni Tu kweli isije ikawa picha ya uwongo kuzushiwa hapo ni Gerezani Tz kama ya Puttin ile yupo Tz hivyo nataka kujua uhakika kama hapo Gerezani inatokea wapi ?
 
Nataka kujua mambo gani mtunzi(Alex Haley) aliyobadilisha kwenye kitabu ?
 
Hongera mzee wetu
One day ntakua hapo
 
Hivi mpaka anafungwa, aliwahi kufikishwa mahakamani kweli ?..

...Na kama wamgemfikisha mahakamani unadhani wangemshitaki kwa kosa gani ?
Proved,
Swali lako Waingereza wangesema ni "tricky," yaani linatatanisha.

Ali Muhsin hakufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Serikali halali imepinduliwa.

Viongozi wa serikali halali iliyopinduliwa washitakiwe mahakamani.

Kisha unauliza, "hypothetical question," endapo angeshitakiwa kosa lake lingekuwa lipi?
 
Adrian,
Sijui Alex Hailey alibadilisha kitu gani.
Mimi nimekisoma mwaka huu nimeona mtunzi amekitendea haki kuna vitu sikutarajia kabisa kuvikuta(kama kuficha hivyo vingekuwa vya kwanza) katika kitabu chake mfano Malcom X anapoelezea uislamu kwa mazuri na kuupampa nk ila kwenye vitu alivyofuta nahisi itakuwa sehemu za kuzungumzia vibaya mahayudi .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…