Malecela avunja ukimya!

watu wako tiyari kumng'oa kikwete ndio maana wanataka isiende kamati kuu
wajumbe wa nec wakipewa nafasi ya kupiga kura watampa mtu mwingine tu na ndio maana wapambe wa JK (malecela na chilagati) wanawakatisha watu tamaa na wanajua ni wakina nani kwa ajili kampeni zi shaanza
 


- umetoa mifano iliyokufa je walishinda hao waliowachallenge sitting president wa vyama vyao? Kama hawakushinda kwa nini usiitwe utamaduni wa chama cha Democrat cha USA kwamba incumbent aliye rais lazima amalize term mbili?

- Malecela hajamzuia mtu kugombea urais, wakuu kumbe mnamuogopa namna hii maneno mengi ya blah blah hapa ohh mzee hachaguliki, pohhh amepitwa na wakati kumbe ni nyinyi ndio mmepitwa na wakati, sasa tizama mnaogopa demokrasia hamtaki wazee waseme chaguo zao, mkuu na wewe tuambie unamtaka nani awe rais next?

FMES!


 

Utamaduni wa CCM kama wanataka kuufanya basi waufanye ndani ya chama chao si kuufanya kwa nchi nzima na kuwaathiri Watanzania milioni 36 ambao si wanachama wa CCM (Hata hao milioni 4 tulioambiwa na Chiligati nina wasi wasi nao maana wengi wao si wanachama hai kwa miaka mingi tu kutokana na kutoridhika na mwenendo ndani ya chama cha mafisadi. Hawa jamaa naona wamejisahau kupita kiasi na kudhani chochote watakachosema hata kama hakina kichwa wala miguu kitakubalika na Watanzania. Hawana chochote kizuri cha kusema kuhusu utendaji wa Kikwete ambacho kinastahili kumrudisha tena madarakani kati ya 2010 – 2015, bali ni "utamaduni wao ndani ya chama"

Ndiyo maana nasema CCM imefilisika kisiasa wanataka kuiburuza nchi bila kujali maslahi ya nchi kwao wao ni bora liende tu mradi yuko Kikwete basi aachiwe tu aendelee kuvurunda hadi 2015 ili kukidhi utamaduni uliopo ndani ya CCM wa kuachiana Urais kwa miaka 10 bila bughudha yoyote hata kama unavurunda namna gani!!! Tukiundekeza huu utamaduni ambao hauweki mbele maslahi ya nchi bali ya akina Kikwete na CCM kuachaiana kukaa madarakani kwa vipindi viwili basi nchi itazidi kuangamia. Kweli CCM imeshika utamu!!! Kigumu cha cha mafis.....Kigumu!!!!!
 

Sema baba!!!! Watanzania tumechoshwa na unafiki wa miaka nenda wa miaka rudi. Miaka miwili ijayo tutakuwa tunasherehekea miaka 50 ya uhuru wetu I hope tutakuwa na Rais mpya huyu ambaye hajui atendalo inabidi apumzishwe kwa maslahi ya nchi.
 


- Ukweli ni kwamba haya maneno yote yana-describe matatizo yako mwenyewe, kumbe mnamuogopa mzee huyu aliyepitwa kisiasa namna hii? Eti wewe ndiye mwenye kuamua mawazo ya Malecela yawe vipi hiyo ni aibu mkuu!

- Tanzania sasa tuko huru kila mtu hata Malecela ana haki ya ksuema mawazo yake hutaki mawazo yake kula chupa, lakini wewe huwezi amulia mwananchi yoyote asiseme anachokitaka mradi hakuvunja sheria.

- Malecela ametoa uchaguzi wake na wewe toa wa kwako na mimi, nitatoa wa kwangu, lakini CCM sio chama chako unalilia nini sasa? Umesema Kikwete amevurunda sana na wananchi hata wenye elimu ndogo wanajua sasa si ungefurahia kwamba atagombea tena mumshinde na mgombea wako makini?

Wakuu siasa sio mchezo rahisi kama mnavyofikiri, na ishus kama hizi ndio mnaonyesha kwa nini wananchi wa Tanzania tunawaogopa sana Upinzani, kwa sababu nyinyi sio wapinzani ni waganga njaa tu, sijawahi kusikia mpinzani anakosa usingizi wka ishu za chama kisischokuwa chao, acheni kurukia kazi za watu jamani.

Kumbe mnamuogopa namna hii huyu mzeee, maneno mengi hapa kumbe ni hewa tu! Wazee sisi CCM ndio tunaondoka hivyo hatuangalii nyuma mzee ameweka msingi na sisi hatupo ndio imetoka hiyooo!

FMEs!
 

Mie nakenua 🙂 tu hapa jinsi unavyoshusha mavitu yako. Nakubaliana nawe 100 kwa 100.
 

- Alitumia jukwaa kama mwananchi na kiongozi wa kudmu wa CCM, kama vile Chadema walivyotumia jukwaa jana, wakuu nendeni mkaawamshe wananchi wa Tanzania huko vijijini na sijui kama mtaweza maana hata hapa JF hamuwezi kuamsha mtu, eti asiyekua na mawazo kama yenu mnafiki sasa huo ndio unafiki wenyewe.

- Kidumu CCM, tuna matatizo ya uongozi, lakini pole pole tunajirekebisha na tunasonga mbele, kumeb Malecela kiboko yenu, wallahi ninawaahidi wkamba hii mijadala yote mnayoonyesha fears zenu nitaifkisha CCM, waone vioja vya internent, hata mimi sikutegema siku nne sasa Malecela tu, that is wasup!

FMEs

 
.............-JK alikubali ushauri wa Melecela kumgeuka Lowassa na kumtapeli. Awali walikubaliana aandike barua ya kujiuzuru lakini sisikubaliwe. Kwa ushauri wa Malecela, JK akaikubali......


mmmhh........where is William Malecela.........
 

- Maneno mazito sana mkuu haya na ubarikiwe.

Idumu CCM.

FMEs!
 




Mkuu makaayamawe,mimi nilisema hili kwenye ile thread nyingine.huyu mzee ni mnafiki tu.kwavile yeye anajijua ni tingatinga la ccm na hawezi kupitishwa kwenye mchujo anataka kuwavuruga wengine wanaokubalika wasiende kuchukua fomu.huyu mzee hana nguvu kivile ndani ya chama kama alivyokuwa nyerere.yeye atulie tu kama maji ya mtungi,aache wanamume kina shibuda wafanye mambo.
 
.huyu mzee hana nguvu kivile ndani ya chama kama alivyokuwa nyerere.yeye atulie tu kama maji ya mtungi,aache wanamume kina shibuda wafanye mambo.

- I like the hana nguvu part, ila tu ni kwamba bila Malecela hata Shibuda anajua kua angekua amefukuzwa CCM na Mkapa siku nyingi sana, hata sasa anajua kuwemo kwake CCM ni nguvu ya Malecela, lakini still bado ninaipenda hiyo fact yako kwamba hana nguvu tena ndani ya CCM, lakini zipo thread karibu 10 hapa JF kati ya jana na juzi that is wasup! Bwa! ha! ha! ha! ha!

- Naona hoja zimesiha sas ngoja tupumzike.

FMES!
 

thread kitu gani bwana hata zikiwa 1000 hazitamfanya malecela kuwa kama nyerere ndani ya ccm.mbona kuna ma threads kibao hapa ya mafisadi?huyu mzee mkapa tu alimdhibiti,tena baada ya kummwaga 2005 alimwambia kabisa kama hataki atoke..
 
thread kitu gani bwana hata zikiwa 1000 hazitamfanya malecela kuwa kama nyerere ndani ya ccm.mbona kuna ma threads kibao hapa ya mafisadi?huyu mzee mkapa tu alimdhibiti,tena baada ya kummwaga 2005 alimwambia kabisa kama hataki atoke..

- Lakini akabaki na sasa kimgeuka kilio cha damu kwako Bwa! ha
! ha! ha!
 
- Lakini akabaki na sasa kimgeuka kilio cha damu kwako Bwa! ha
! ha! ha!

akabaki anamnunia mwenyekiti wake.kama mwenyewe alishaambiwa na wakulu atoke sasa hizi guts za kuita watu majina watoke anazitoa wapi?
 

Bubu, hii ndi sababu nasema watanzania inabidi ile tu JK akichukua form ya urais ni kuitisha maandamano nchi nzima kupinga uamuzi wake hata kama ni wakikatiba. Sababu hatumkubali kwa kuwa hakutenda yale tuliyo tegemea toka kwake au tumemchoka.
 

Kwanza hiyo kauli kuwa wanawanachama 4 mil hawaoni kuwa inathibitisha kuwa wao ni wezi wa kura?
 
naomba nitajiwe competent candidates wa urais kwa sasa tanzania
 

Mimi si CCM, lakini kuna mambo kweli tunajadili bila hata kuangalia ukweli. Rais ni wetu wote, lakini Katiba inasema ili ugombee uRais lazima uwe umepitishwa na Chama cha kisiasa kilicho na usajili wa kudumu. CCM ni Chama kimojawapo, na wana taratibu zao, hatuwezi kusema kwa kuwa Rais ni wetu wote basi taratibu za CCM zigeuzwe. Sisi kama wananchi tuna eneo letu, wakati wa kupiga kura, lakini kuilaumu CCM haitusaidii, tujiunge basi ili kama ni hivyo tukamng'oe tukiwa kama wanachama.

Tukija CCM, hakuna wanachama atajitokeza kuchukua fomu na Rais aliyepo madarakani, hii ni kwa sababu hawezi kupitishwa na wana CCM wenzake kwa njia yoyote ile. Hivi kweli inaweza ingia akilini Rais aliyeshika dola, anayeidhibiti tume ya uchaguzi aangushwe, unajua inaweza kutokea nini kwa CCM, ni kuifanya tume ya uchaguzi iwe huru ili naye awakomoe. Hivyo tunatakiwa tuweke mikakati ya kuing'oa CCM na si kuwapangia eti CCM wabadilishe Rais, hilo halipo. Tutakuwa tunapoteza muda na hilo, hata akija mwingine, CCM ni walewale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…