Malecela avunja ukimya!

Malecela avunja ukimya!

Awali kasema ccm ni chama cha masikini. ni kweli nchi imeubariki umasikini? tunajivunia kuwa nao? Pili kasema kuwa Kikwete hana mpinzani 2010. na wanaojaribu wasahau. inamaanisha ile demokrasia ya miaka mitano mitano kwishnei?

Hana chochote huyu cha kutufundisha Watanzania. Mawazo yake yamepitwa na wakati.
 
Big Nooo! Mkuu FMEs
Malecela ametufundisha kuwa WANAFIKI ili mradi ya kwetu binafsi yametunyookea.
  1. Kama Kikwete alipoingia madarakani nchi ilikuwa haina umeme na sasa hivi hali ni mbaya zaidi je hayo ni mafanikio yanayohitaji kuzawadiwa?
  2. Kama Kikwete alipewa ripoti ya Bunge juu ya rushwa ya Richmond lakini hadi leo hajashughulikia madondoo yake, je huu ni utendaji unaohitaji kuzawadiwa mvua 5 nyingine??
  3. Kama hali ya elimu imezidi kuwa mbaya, hospitali hazifai mpaka upelekwe India, SA, UK n.k., vyuo vikuu ndio usiseme, je haya yanahitaji zawadi?
  4. Kama imeshindikana kuwashughulikia wala rushwa wa, EPA, BOT, RadarGate n.k., ambao habari zao zimezagaa kila kona ukiachia hao wachache anaotumia kututengenezea viini macho, je hii sio failure??
  5. Kama mpaka leo nikitaka kwenda Mwanza ni lazima nipitie Kenya, je haya ni maendeleo??
  6. Kama inakuwa nafuu kwa mfanyabiashara wa Tanzania kuingizia mizigo yake bandari za Durban au Mombasa badala ya bandari ya Dar es salaam, je huku ni kwenda mbele au ndio twafa hivyo??
Je, ina maana kwenye milioni 40 ya waTZ au milioni 4 ya wanaCCM hakuna anayeweza kuwa mtendaji bora kuliko alivyotenda Kikwete?

Ingawa namheshimu sana Mzee Malecela, lakini emetudhihirishia wazi kuwa kwake yeye, maslahi binafsi ni bora mara 100% kuliko maslahi ya nchi.

- Sasa mkuu haya ni mawazo yako, kwa nini unataka yawe na yake pia? yaani kutokuwa na mawazo kama yako kunamfanya Mzee kuwa mnafiki? Haya ni mawazo yako tu mimi nina yangu na kila mtu ana yake, na sio lazima kwa kuwa tofauti na mawazo yako basi tunakwua wanafiki ni hoja finyu sana mkuu, kiasi kwamba inaondoa hata ladha ya baadhi ya hoja nzito ulizozitoa hapo juu.

- Acha name calling ili ueleweke unasema nini bro, hizi za yeye kuhomngwa na rais sijui unazitoa wapi? Kwa nini usiweke ushahidi wa yeye Mzee kuhongwa na rais?

FMES!
 
Ingawa namheshimu sana Mzee Malecela, lakini emetudhihirishia wazi kuwa kwake yeye, maslahi binafsi ni bora mara 100% kuliko maslahi ya nchi. [/SIZE][/B][/COLOR]

Nashauri tuyataje maslahi binafsi ya Malecela katika safu hii, na mimi naanza:

-JK alimteua kuwa mjumbe wa kudumu katika CC bila ridhaa ya chama ili kumpangusa machozi ya kukosa urais. Kawaida Makamu angekuwa mjumbe NEC ingetosha.
-JK alikubali ushauri wa Melecela kumgeuka Lowassa na kumtapeli. Awali walikubaliana aandike barua ya kujiuzuru lakini sisikubaliwe. Kwa ushauri wa Malecela, JK akaikubali.
-Wabaya wa Malecela katika mtandao wanashughulikiwa na JK, kwa hiyo mzee huyo anachekelea.
-JK kufuata ushauri wa Malecela unamharibia mambo ndani ya chama. Yakiharibika, Malecela anacheka pia na kutumabia yeye ndiye angefaa na siyo JK. Wengine ongezea.
[/QUOTE]

- Hapa labda kuna hoja moja tu ya msingi inayotakiwa kujibiwa nayo ni kwamba unaonekana ulikuwa hujui kwamba CCM ina tabia ya kuwafanya viongozi wake wote waliofikia nafai ya Mwenyekiti wa taifa na Makamu wa taifa kuwa mjumbe wa kudumu wa CC na NEC kwa hiyo hii mkuu uko nje kidogo!

- Seif Mwenyekiti wa CUF analipwa mafao na serikali kama huyu Mzee, na Seif hajikombi kwa yoyote, unaona hoja ilivyokuwa finyu, hayo mengine ya Lowassa hata kuelewa unachosema sielewi ni nini?

Malecela ana haki ya kutangaza rasmi nani anamtaka awe rais, kama huna waulize serikali ni kwa nini lakini sio ksoa la Malecela.

FMEs!
 
Hana chochote huyu cha kutufundisha Watanzania. Mawazo yake yamepitwa na wakati.

- Sasa kwa nini toka juzi kuhangaika na kiongozi aliyepitwa na wakati, kwa nini thread kila kona kwa ajili ya kiongozi asiyekuwa na anyhting to offer? Why hata kupoteza muda kuja ku-comment on his comments?

- Wakuu vipi mbona maneno yenu hayafanani na matendo, kiongozi aliyepitwa na wakati siwezi kuwa na muda hata wa ku-comment on his comment only yule tu mwenye umuhimu na siasa za taifa langu ndio nita-comment.

Inaonekana aliyosema ndio yatakayokuwa, saafi sana kutoka kwa kiongozi aliyepitwa na wakati, hebu tutajieni ambao hawajapitwa na wenye mapya, au Zitto? Bwa! ha! ha! ah i mean this is fun!

Wazee wa sauti ya umeme FMEs!
 
Inakuwaje mtu anayekemea press conferences awe anatufundisha ukweli na uwazi?
 
- Labda ungeongelea utamaduni wa upinzani tu mkuu, maana ni kwa maneno yako kwamba utamaduni wa CCM haukuhusu, sasa why waste time na utamaduni usiokuhusu tena wa CCM na wala sio taifa? Bwa! ha! ha! ah!

- Utamaduni wa CCM haukuhusu basi ongelea unaokuhusu, yaani utamaduni wa Upinzani, au?

FMES
!
 
Inakuwaje mtu anayekemea press conferences awe anatufundisha ukweli na uwazi?

- kwani Malecela ni nani mpaka awe na effect kwa kuikemea press, wewe na mimi tukiikemea press tunaongeza au kupunguza nini kwa shughuli zao?

- Malecela according to people hapa amepitwa na wakati na hana effect yoyote sasa hiki kilio ni cha nini? Imena ukiona panafuka moshi ina maaana chini kuna something au? Hatuwezi kwua tunafoka like this bila sababu eti sababu ni nini hasa an huyu Mzee aliyepitwa na wakati? I do not get it!

FMES!
 
CCM haiwezi kusema ni chama cha kidemokrasia na wakati huo huo ikawa na culture ya kumpitisha tu rais incumbent bila mchuano.

Either

CCM ni chama cha kidemokrasia na mgombea urais hapatikani automatically kama rais anayemaliza muhula wa kwanza

Or

CCM si chama cha kidemokrasia na kina "culture' ya kumpitisha tu rais anayemaliza muhula wa kwanza kuwa mgombea wa chama wa muhula wa pili, bila ya mchuano wowote wa kweli.

Vitu viwili hivi haviwezi kwenda pamoja.
 
- Mkuu it does not matter what CCM is or not, kinachojali vipi utamaduni wa chama chako cha siasa ukoje?

- CCM haimzuii yoyote kugombea urais, kama ambavyo Obama atapita bila tatizo ndani ya Democratic Party, next time je nao huko US hawana demokrasia?

FMES!
 
- Mkuu amelazimisha akiwa kama nani? mbona mnapenda kukuza maneno hivi, yeye ameongelea chama chake cha CCM na wewe ongelea chama chako cha siasa,

- hii fear inatoka wapi kwa sababu ya maneno ya mzee mmoja tu amabye maepitwa na wakakti, hana akili, ni mzee na balh! baln! sasa vilio vyote hivi ni vya nini kwa sababu ya mzee asiye na lolote kwa taifa?

FMES!

Mkuu FMES, kauli ya Mzee Malecela sio ya kupuuzia hata kidogo. Mzee huyu ni mwanasiasa mzoefu katika nchi hii, amewahi kushika madaraka makubwa sana katika Taifa na ana influence kubwa vile vile (ndani na nje ya CCM). Siwezi kuthubutu kusema wala kufikiria licha ya kukubali kuamini kuwa hana akili, amepitwa na wakati wala ni Mzee wa Blah blah kama ulivyosema. Huyu ni mtu wa maana na ataendelea kuwa hivyo mpaka siku yake ya mwisho.

Kauli aliyoitoa inawataka CCM wote waache kufikiria kutafuta nafasi za kugombea uRais 2010, kwakuwa utamaduni wa chama hauwaruhusu na kwamba JK anatakiwa kuwa ndie mgombea wa CCM katika uchaguzi mkuu ujao. Sina ubaya na matokeo hayo, ila sidhani kuwa ni vyema kwake kuwakaisha tamaa wana CCM kupata nafasi hiyo ya kikatiba kuomba kuchaguliwa.
 
- Mkuu kwa kawaida huwa ninaheshimu sana mawazo yako maana yametulia, mkuu CCM walipoamua kwamba kila Mwenyekiti wa CCM taifa na Makamu wake lazima wawe viongozi wao wa kudumu, nia na madhumuni ilikuwa moja tu nayo ni kuhakikisha kwamba wanakuwa mstari wambele kukiweka sawa chama wanapoona kinakwenda mrama.

- Ninaamini kwamba unaelewa vizuri operations za siasa za vyama na utawala, ulipotokea msuguano kwenye uchaguzi wa UV-CCM huyu mzee na Kinana waliingilia kati na kushauri wagombea wote wa bara kupigwa chini, sasa huwezi sema this time amekurupuka tu, lazima ameona kuna msuguano ambao ni hatari kwa chama chetu, amekaa na wazee wenziwe na wakaamua aliyoyasema juzi kukinusuru CCM.

Mwalimu alsiema hivi hivi kukinusuru CCM, kwamba Mrema agombee ubunge na sio urais, tena alimwambia haya Msasani Mrema akagoma na kugombea urais akaishia kula chuya, sasa hawa ndio wazee wetu wa CCM tunaowaamini kukiweka sawa chama chetu, maana ndio utamaduni wetu kwekana sawa tukiwa nje ya mstari.

Lakini una hoja nzito sana na unaelewa sana siasa ya bongo mkuu, ninakukubal, ila tuachieni utamaduni wetu ndani ya CCM ambao tulifundishwa na Mwalimu baba wa taifa letu.

FMES
 
- Sasa mkuu haya ni mawazo yako, kwa nini unataka yawe na yake pia? yaani kutokuwa na mawazo kama yako kunamfanya Mzee kuwa mnafiki? Haya ni mawazo yako tu mimi nina yangu na kila mtu ana yake, na sio lazima kwa kuwa tofauti na mawazo yako basi tunakwua wanafiki ni hoja finyu sana mkuu, kiasi kwamba inaondoa hata ladha ya baadhi ya hoja nzito ulizozitoa hapo juu.

- Acha name calling ili ueleweke unasema nini bro, hizi za yeye kuhomngwa na rais sijui unazitoa wapi? Kwa nini usiweke ushahidi wa yeye Mzee kuhongwa na rais?

FMES!

Mkuu FMES,
  1. Hali ya umeme kuwa mbaya haya sio mawazo yangu ni facts
  2. Elimu, Afya, Barabara n.k. kurudi nyuma au kutosonga mbele ipasavyo sio mawazo yangu ni facts
  3. Mafisadi kutokushughulikiwa sio mawazo yangu hizo ni facts
Sasa kama waTanzania hata wale walio na elimu ndogo kuliko Mzee Malecela wameyaona hayo lakini Mzee anatuambia kuwa anayewajibika nayo amefanya kazi nzuri, unataka huu tuuiteje;
a. Ujanja
b. Unafiki
c. Upunguwani​

Hizi ni sifa za matendo ya mtu na sio name calling. Mzee Malecela alichotufanyia ni UNAFIKI.
 
- Labda ungeongelea utamaduni wa upinzani tu mkuu, maana ni kwa maneno yako kwamba utamaduni wa CCM haukuhusu, sasa why waste time na utamaduni usiokuhusu tena wa CCM na wala sio taifa? Bwa! ha! ha! ah!

- Utamaduni wa CCM haukuhusu basi ongelea unaokuhusu, yaani utamaduni wa Upinzani, au?

FMES
!

Kama vile unafahamu jamaa ni chama gani. Huyu rais mchovu siyo wa sisiemu tu ni wa taifa lote la wadanganyika na unafahamu vema hilo. kusema huo utaratibu haumhusu ni kuonyesha tabia ya ki-chama cha mafisadi (CCM) kitu ambacho naamini uko juu yake maana kwenye thread ya "malechela avunja ukimya"
ulitonya kuwa ungependa dr silaha awe rais, swali hapa ni wewe sisiemu mambo ya chadema yanakuhusu vipi?
 
- Mkuu it does not matter what CCM is or not, kinachojali vipi utamaduni wa chama chako cha siasa ukoje?

- CCM haimzuii yoyote kugombea urais, kama ambavyo Obama atapita bila tatizo ndani ya Democratic Party, next time je nao huko US hawana demokrasia?

FMES!

Hakuna guarantee ya kuwa Obama atapita next time? Itategemea na utendaji wake.
  • Robert Kennedy alimchalenge Lyndon Johnson 1968
  • Ronald Regan alimchalenge Gerald Ford 1976
  • Edward Kennedy alimchalenge Jimmy Carter 1980
Sasa, kwa nini mtu ambaye anaelewa wazi kuwa binafsi hachagulikiki kwenye vinyang'anyiro vya uraisi, ajaribu kuwazuia wengine wasijaribu bahati zao?

Demokrasia ya sasa haiangalii cha utamdaduni ambao umetufelisha.

Huo utamaduni unaousemea usingekuwa umeishiwa nguvu kutokana na mazingira ya kiuchumi na kisiasa, Mzee Malecela asingekuwa na haja ya kutembezea watu mkwara.
 
kama huo ndio utaratibu na utamaduni wa chama
ni bora wauingize kwenye katiba ili hii kitu ifanyike "automatic"
bila gharama kubwa ya kipesa. vinginevyo itakuwa ni ufujaji wa pesa
ambazo naamini kiasi kikubwa kinatokana na ruzuku ambazo nazo
hutokana na kodi ya wananchi na si wanachama tu.
 
Last edited:
Hadi hivi sasa tumeona viongozi watatu wakiwapiga watu Mkwara kutokujaribu kumuingilia Kikwete. Nao ni;

  1. Jakaya Kikwete akiwapiga mkwara viongozi wa zamani
  2. Chiligati - Watanzania kwa ujumla
  3. Mzee Malecela - Wenye ubavu wa kugombea uraisi, akina Mwandosya, Mwakyembe n.k.

Kuna nini ndani ya Ikulu ya Kikwete kinachowaogopesha.
 
inaonekana kikwete anawasiwasi sana ndio maana ametuma watu wake, mtu ambaye anamuogopa ni MWANDOSYA na ndio maana amempa wizara ya Umwagiliaji ili asisikike lakini mpaka sasa hivi watu wake wapya ni ovyo(masha, ngeleja, mkullo, membe labda pinda) na hamna hata mmoja ambaye anakubalika zaidi ya mwandosya. kuna taarifa kwamba "rebels are backing mwandosya" na kikwete ajui afanye nini maana yake akimfukuza kazi ndio chati inapanda. Only time will tell
 
- Sasa kwa nini toka juzi kuhangaika na kiongozi aliyepitwa na wakati, kwa nini thread kila kona kwa ajili ya kiongozi asiyekuwa na anyhting to offer? Why hata kupoteza muda kuja ku-comment on his comments?

- Wakuu vipi mbona maneno yenu hayafanani na matendo, kiongozi aliyepitwa na wakati siwezi kuwa na muda hata wa ku-comment on his comment only yule tu mwenye umuhimu na siasa za taifa langu ndio nita-comment.

Inaonekana aliyosema ndio yatakayokuwa, saafi sana kutoka kwa kiongozi aliyepitwa na wakati, hebu tutajieni ambao hawajapitwa na wenye mapya, au Zitto? Bwa! ha! ha! ah i mean this is fun!

Wazee wa sauti ya umeme FMEs!

hawa wazee hawajapitwa na wakati kiivyo, ila sometime kauli zao zinatupigisha butwaa. kwa lugha nyingine alitumia press conference kama jukwaa la kampeni za siasa? (CCM) Pia bado hofu yangu iko palepale. mbona tunaubariki umaskini? "CCM ni chama cha maskini"
 
Hivi hakuna wanaCCM wenye ubavu wa kuandamana kupinga kauli za Malecela na Chiligati?

Hakuna anayetaka kuingia katika historia?
 
Naona hawajakosea na vile vile kuwapa tahadhari wale wenye tamaa ya kutaka kugombea,kwani ukijiingiza hivi sasa na kuomba kugombea uhakika wa kuikosa nafasi hiyo ni mia kwa mia na hivyo utaharibu nafasi ambayo itakuwepo 2015,kwani itasomeka uliwahi kuogombea na ukapata kura moja ,hivyo hilo ni pigo ,kwa CCM kugombea katikati utakachovuna ni pigo tu,ndio Malechela amewapa mwanga kuwa kwanza wasubiri ili kujaribu bahati yao wakati ule wa kipindi cha mwisho kutokana na Culture yao.Nafikiri Malecela angewambia wasubiri ingeonekana ametumia kauli nzuri tu ,hata kikwete aliambiwa asubiri.
 
Back
Top Bottom