MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Nawasalimu kwa jina la Chama Cha Mapinduzi.
Ninaandika nikionyeshwa kusikitishwa sana na matamko yanayotolewa na watu mbalimbali hasa wanasiasa maarufu wa kiafrika kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth wa Uingereza. Julius Malema wa SA pamoja na watu wengine wameonyesha chuki zao kwa hoja za mambo ya ukoloni wa UK kwenye nchi za kiafrika.
Mimi naona ni sawa na kupoteza muda kwa sasa kuanza kumlaumu malkia kuhusu ukoloni wakati miaka zaidi ya 60 baada ya uhuru bado Afrika haina maendeleo. Lazima tukubali kuna mambo mabaya yalishawahi kutokea na hatuna jinsi kuyaondoa kwenye historia yetu hivyo yatupasa kushikilia vizuri tulicho nacho mkononi na kusonga mbele. Muhimu tupambane tusiporudi tulipotoka.
Waafrika tukibaki kukumbatia mambo yaliyopita tutabaki hivi hivi kwa vizazi vingi vijavyo. Mbona India na nchi zingine za Asia zilitawaliwa ila wakakataa kubaki walivyokuwa na sasa hivi wana maendeleo karibia au hata kuwazidi wakoloni wao?
Kumchukia Mwendazake Malkia pamoja na mabeberu wenzake haina msaada wowote kwenye maendeleo yetu. Ni kujipa tu stress. Mabeberu walishakuwa na akili nyingi sana kitambo. Tujiulize wakati Mabeberu Mababu walipokuwa wanajenga Eiffel Tower Paris mwaka 1905 sisi mababu zetu walikuwa wanafanya nini?
Wakati mabeberu mwaka 1903 wanapambana kuunda ndege je sisi tulikuwa tunafanya nini? Wakati babu wa mabeberu Isak Newton anapambania mambo yake ya kisayansi je babu zetu walikuwa wanafanya nini? Kuna muda tukubali tu kuna mambo ilibidi yatokee ili sisi pia tupige hatua. Tusamehe na tu-move on.
Baadhi ya wanasiasa na wanaharakati acheni upuuzi wa kupotosha umma ili kupata sifa za kisiasa. Mabeberu bado wana umuhimu mkubwa hata kama tunajifanya kuwapinga. Nendeni hapo Zimbabwe muone maisha magumu ya raia kwa ushenzi uliofanywa na mtu aitwae Mugabe. Halafu pia kwa mila zetu huu sio wakati wa kuonyeshana chuki.