Malengo yametimia sasa nahitaji mke wa kuoa

Malengo yametimia sasa nahitaji mke wa kuoa

igembe2018

Member
Joined
Mar 3, 2018
Posts
18
Reaction score
10
Wadau wote wa JF natumai ni wazima wa afya,

Binafsi kila mtu anayo malengo yake aliyojiwekea na muda wa kuyatimiza. Malengo yangu yametimia na sasa nahitaji mke ili kujenga familia imara yenye upendo wa dhati.

Wasifu wa mke
Awe mkristo na mcha mungu kweli kweli.
Awe mwenye mapenzi ya dhati na anayejua nini thamani ya ndoa
Awe kabila lolote sibagui
Awe anaishi Dsm na si vinginevyo
Awe na kazi halali inayomuingizia kipato.
Asiwe mrefu sana.
Kama ana mtoto basi awe mmoja tu.
Elimu yeyote maana mwanamke ana elimu pia ya kuzaliwa.
Awe tayari kufunga ndoa ili kuishi maisha ya kumpendeza mwenyezi Mungu.

Mimi binafsi nimeajiriwa na kampuni binafsi na shughuli zangu ziko hapa Dsm ndio maana sihitaji mtu kutoka nje ya Dsm.

Kwa yeyote atakayejipima na kuona ana sifa njoo PM tuyajenge.
 
Umekuja kutafuta humu ndani kwenye jf?
Au ili tangazo linapita tu humu.
 
kwanini mnakimbilia kusema mcha Mungu kweli kweli, ? watu wana mcha Mungu na bado ni wazizi na wahuni kweli kweli, fanya survey makanisani mkuu uone namaanisha nn
 
Wadau wote wa JF natumai ni wazima wa afya. Binafsi kila mtu anayo malengo yake aliyojiwekea na muda wa kuyatimiza. Malengo yangu yametimia na sasa nahitaji mke ili kujenga familia imara yenye upendo wa dhati.

Wasifu wa mke
Awe mkristo na mcha mungu kweli kweli.
Awe mwenye mapenzi ya dhati na anayejua nn thamani ya ndoa
Awe kabila lolote sibagui
Awe anaishi Dsm na si vinginevyo
Awe na kazi halali inayomuingizia kipato.
Asiwe mrefu sana.
Kama ana mtoto basi awe mmoja tu.
Elimu yeyote maana mwanamke ana Elimu pia ya kuzaliwa.
Awe tayari kufunga ndoa ili kuishi maisha ya kumpendeza mwenyezi mungu.

Mm binafsi nimeajiliwa na kampuni binafsi na shughuli zangu ziko hapa Dsm ndio maana sihitaji mtu kutoka nje ya Dsm.

Kwa yeyote atakayejipima na kuona ana sifa njoo pm tuyajenge.
Mkuu unatafuta MKE au unatafuta vigezo?

Bora ungesema asiwe mrefu ili anapokupm ajue kua yeye ni mfupi
Na jingine akupende.
Mengine yote unayoyataka wewe mkikubaliana kuoana utamwambia nataka uwe mchamungu.nk
 
[emoji16][emoji23][emoji115][emoji115][emoji115]
 
Malengo yapi ? Uliyotimiza had sasa?
Nkupe ndg yngu ili na mm npitie kwa ndg yngu nfanikiwe? Kuwa mkweli nisije nkamchanganya ndg yngu Una mtaji? Au nn ...
 
Id Yako Ya Zamani Ni Ipi?Maana Hii Mpya Imekuja Direct Kutafuta Papuchi
 
taja malengo uliyoyatulimiza wanawake wanahitaji kusikia labda ushatimiza malengo ya kununua gari au nyumba
 
Back
Top Bottom