Malengo yangu mwaka 2021 ni kuacha pombe, umalaya na ku-bet

Malengo yangu mwaka 2021 ni kuacha pombe, umalaya na ku-bet

MICHAEL SON

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2020
Posts
458
Reaction score
536
Wakuu salaam!

Mwaka 2020 Nimeamua na nimedhamiria kuacha mambo haya:

1. Pombe
2. Umalaya
3. Ku-bet

Hii combination inafanya natumia zaidi ya laki 6 kwa mwezi wakati kipato changu ni chini ya 500k, najikuta katika madeni ya kijinga kijinga.

Nimedhamiria kumrejea Muumba, yaani kwa dhambi nilizotenda na nilizonazo natamani hata nisali Dini zote!

MARRY X MASS & HAPPY NEW YEAR IN ADVANCE

NB: MNIWEKE KATIKA MAOMBI
 
Kwa malengo haya makini ujue malaika wa nuru Paradiso wanapongezana na kushangilia kwa machozi ya furaha kwa kuongeza idadi ya raia wa Ufalme. But, resolutions are just as strong as nothing kama hakuna corresponding, intelligent action steps on a daily basis.

Lastly, to every action there is an equal and opposite reaction. You have simply declared a terrible war against the forces of darkness, the worst of which is the Devil & Satan himself -- the most wicked, gullible & the bitterest of all formidable foes. This is to say the journey upwards will never be easy for you, but fortunately God has promised abundant and constant grace and power to carry you through to the very end triumphantly.
 
Shetani nae hapendezwi na mipango yako, Maana wafuasi wake watapungua. Atakuletea pisi kali zinazokunywa pombe badala ya kuacha pombe utaongezewa zaidi wanywaji na kampani kama hizo usingetangaza maana umetangaza vita na shetani.
 
Mkuu kwa nini:-
1) Unakunywa pombe?
2) Unafanya umalaya?
3) Una-bet?

Unakusudia kufanya nini ili kushinda huo unywaji pombe (ulevi), Umalaya na ku-bet?
Pombe SABABU ya marafiki ambao nimekusudia kuwaepuka na nikilewa lazima nihangaike na madanga and kubet ni tu kutaka pesa za chap chap ili nikanywe nipate malaya! Its like a circle!.. Am going through on line counselling pia
 
Back
Top Bottom