Malengo yangu nitakayoyatimiza nikifikisha miaka 40

Malengo yangu nitakayoyatimiza nikifikisha miaka 40

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Posts
11,837
Reaction score
17,412
Ndoa stable kabisa ambayo iliyopitia magomvi kadhaa lakini haijawahi kuwa na tishio lolote la kuachana.

Watoto wa 4 huku wa kwanza wao akiwa na miaka 18,yaani wawili wa kike na wawili wa kiume.

Nyumba yangu iliyozungukwa na eneo lenye ukubwa wa hekari 1 na humo ndani nitakuwa nifanya maendeleo kama yafuatayo..

  • Mihogo ambayo. ni dawa ya kansa na inapunguza risk ya tezi dum
  • Mibaazi kwani ni dawa moja mujarrabu ya kifua.
  • Matembele yanayoongeza damu.
  • Mbuzi wenye kuleta maziwa safi
  • Migomba yenye ndizi ambazo huomgeza nguvu za misuli ya miwli.
-Mipapai ya kutosha inayosaidia kujenga miwli.
  • Minazi ambayo tutakula nazi na madafu.
  • Miembe yenye kuzaliana sana.
  • Miparachichi isiyopungua mitano.
  • Kuku wengi saana wasiopungua 100 hao ni kwa ajili ya nyama na mayai.
  • Kilimo cha nyanya na mchicha bustani.

Kisha nitakuwa na gari yangu ya usafiri kwa ajili ya safari za mjini na kurudi.

Majirani wema ambao tutaishi nao kama ndugu,huku tukibadilishana mawazo.

Eneo hili litakuwa maeneo ya shamba kidogo ambako ni mbali na mji Kwa KM kadhaa.

Haya maisha tunahitaji mambo machache sana ili tuyafurahi na sio mambo makubwa ambayo tunalishana katika zama zetu.
 
40-18 = 22

Kwahiyo sahivi upo under 22?
Ahahahaha..mkuu wewe ni mkali wa logical maths.
Nilikua nawaza nachomokea pande gani kujua umri wake kamil wa sasa?? Hapa nilikua najiuliza sana hatimae nikakutana na hii concept.. bravoo bro.
Wadogo zetu hawa bwana

Ila what if kwasasa ana miaka 35 na mwanae ana miaka 13 already na 40 years kwake ni justb5 year ahead??
 
Ahahahaha..mkuu wewe ni mkali wa logical maths.
Nilikua nawaza nachomokea pande gani kujua umri wake kamil wa sasa?? Hapa nilikua najiuliza sana hatimae nikakutana na hii concept.. bravoo bro.
Wadogo zetu hawa bwana

Ila what if kwasasa ana miaka 35 na mwanae ana miaka 13 already na 40 years kwake ni justb5 year ahead??
Jamaa angepata code ya umri wangu kama tu ningesema mwanangu ana miaka mingapi kwa sasa..

Ila hesabu zake haziwezi kumpa umri wangu wa sasa hivi😀😀.

Jambo la msingi ni kwamba bado sijafikia miaka 40
 
Nakuombea
Mkuu naomba na mimi niombee sio badae nataka uniombee now h
kama una mda..

Mimi nataka nipate mwenza ambaye atakua anaendana na hali yangu ya upambanaji ili tufike malengo...

Asiwe wa kunizidi umri awe wa kawaida ila awe ametoka sehemu ambayo sio hali ya chini kama mimi kwa maana kipofu hawezi mwendesha kipofu mwenzake
 
Sikukatishi tamaa ila hata mimi mwenyewe nilikuwa na ndoto kama hizo, sasa hivi naishi ghetto ambalo ni kama stoo bora hata enzi za ujana nilikuwa ninamuelekeo
1000012625.jpg
 
Back
Top Bottom