JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Kutelekeza watoto hufafanuliwa kama "aina ya unyanyasaji ambao unamaanisha kutompa mtoto huduma ya malezi inayohitajika na inayostahili kulingana na umri wa mtoto ingawaje kifedha mlezi au mzazi anaweza kufanya hivyo."
Mara nyingi watu hushindwa kutofautisha kati ya umasikini na kutelekeza watoto, kwa kawaida Familia masikini hazina uwezo wa kutoa huduma ya kutosha kwa watoto wao ila wazazi na walezi waliotelekeza watoto huwa na uwezo .
Aina za Kutelekeza Mtoto
Kutelekeza Kimwili
Hii ni aina ya utelekezaji ambayo ni maarufu zaidi. Katika hali hii, mzazi au mlezi hampatii mtoto mahitaji yote ya msingi kama chakula, mavazi na malazi. Wakati mwingine, watoto wadogo huachwa bila usimamizi mzuri kwa muda mrefu.
Kutelekeza kwenye Elimu
Aina hii ya kutelekeza watoto ni pale ambapo mzazi au mlezi hatimizi mahitaji ya mtoto ya shule kama vile karo au sare za shule hali inayopelekea mtoto kushindwa kufika shuleni. Na wakati mwingine mtoto anaweza kuwa hajaandikishwa shule kabisa.
Kutekeleza Kihisia
Hii ni aina ya utelekezaji ambayo si rahisi kuitambua na kesi zake mara nyingi haziripotiwi. Hii ni pale ambapo mtoto hudharauliwa, kutishiwa na kutengwa. Mzazi au mlezi hana muda wa kumsikiliza mtoto yale yanayomsibu na pia humkataza kujumuika na wenzake.
Kutekeleza katika Matibabu
Katika visa hivi, wazazi au walezi hawawapatii huduma ya afya ya kutosha watoto wao, ingawa wanaweza kumudu. Mzazi anaweza kukataa kumpeleka mtoto hospitali hali inayoweza kupelekea mtoto kupoteza maisha.
Athari za kutekeleza watoto
Shida katika ukuzaji wa ubongo.
Kujihatarisha, kama kukimbia nyumbani.
Kutumia dawa za kulevya na pombe au kuvunja sheria.
Kuingia kwenye mahusiano hatarishi.
Ugumu katika mahusiano baadaye maishani, hata na watoto wake wenyewe.
Upvote
0