Its Pancho
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 15,966
- 26,404
Ma- dingi wengi siku hizi tunawalea watoto kimayai mayai sana ki- junior junior sana. Matokeo yake mtoto anakosa dira na kujiongoza peke yake huko mbeleni.
Sasa Fanya haya kumuokoa mtoto wako (wa kiume) Dunia imeharibika sasa.. Hakuna wa kukunyooshea mwanao zaidi ya kumtumbukiza shimoni.
1: Mtoto wako anapoanza kuongea wewe kama dingi anza kumnyoosha mapema haraka sana kwa kumkaririsha mambo mazuri na yenye kufaa kwa umri wake.
Mfano acha kutukana mbele yake kwani anakariri, na ipo atatukana mbele yako ama akiwa na wenzake.
2: Mzoeshe ajue wazi kuwa anapofanya moja ya makosa uliyomkataza kufanya basi aidha achapwe viboko kiasi kulingana na umri wake sio kumzibua na mchi sijui mpini, UTAUA.
Watu wengi siku hizi wanakariri ukimchapa mtoto anakuwa sugu, nani kasema? Unapomchapa ana- feel kwani ana hisia tena mchape mbele ya wenzake hatorudia tena kwani atajua wenzake watamcheka..
3: Mfunze kuwa na adabu hasa kunapokuwa na wageni
Hii imewatokea watu wengi kina mama Jr. Kuna wageni kutoka mbali bado mtoto anakurukia rukia na kuwadandia wageni huku kakisema "toka kwetu" umekuja kula". Nawe unachekelea, "junior bhana!"
Sababu umemzoesha azoee kila mtu na kumuona mwenzake! Hii imeanzia kwako umetengeneza gap, kwamba anakuona wewe kama rafiki na sio mzazi. Sasa kwanini asiwaone watu wengine wazima kama rafiki zake?
Na ndio maana siku hizi kesi za vitoto kulawitiwa ni nyingi. Kunapokuwa na wageni, asalimie kisha kuondoka hapo. Aje anapohitajika.
4. Mfunze kazi ndogo ndogo pale tu anapoanza shule ya msingi
Ukiachana na kuwa huko shule nyingi siku hizi za ma bus ya njano huwa hawafagii, hawamwagilii hata bustani. Basi wewe tengeneza hata bustani home awe anamwagilia jioni. Usimuache azurure sana mitaani kwani kuna matoto yameoza nayo yatamfanya aoze.
Simaanishi umuweke ndani kama mwali no! Muache aione namna dunia ilivyo kwa sura yake. Ajifunze kwa vitendo.
5:muelekeze na mzoeshe kuwa asipende kitonga (mtelezo). Na sio kila anachokuomba unampatia.
Utakuta watoto wengi wanaibiwa na kufanyiwa unyama na stranger. Kisa tu buku ya chips, kwani amezoeshwa nyumbani kila anachotaka anapata kwa wakati. Siku akikosa mtu atampa na hatokataa.
Na siku hizi mtu hatoi kitu chake Bure. Sio kila anachokuomba mwanao unampa. Ifanye akili yake iamini huwezi kupata kila kitu japo inauma ila ndo ukweli. Afurahi na kuridhika kwa anachokipata.
Funzo: Tutumie kondom tuache kufyatua watoto kama King Mswati.
Pancho boy