neemachandruok
Member
- May 28, 2024
- 8
- 12
Ninaguswa sana ninaposikia stori za watoto kubakwa au kulaitiwa na ndugu au mwalimu au jirani.
Tafiti zinaonyesha watoto wengi wanaofanyiwa vitu vibaya ni wale ambao hawana sauti yaani walinyanganywa haki zao za kuongea kwa sababu inawezekana mzazi alikuwa mkali sana au anamchapa au halikuwa asikilizwi kwa hiyo hii inapelekea mtoto kuona hana haki ya kuongea wala hana haki ya kusikilizwa. Mtoto anakosa uhuru wa kuongea chochote anakuwa mnyonge na uwezekano wa kufanyiwa vitu vibaya ni mkubwa.
Utafiti unaonyesha kuwa mbakaji au mlawiti anajua ni nani wa kufanyia hicho kitendo. Anajua huyu nikimfanyia hataongea chochote kile kwa mtu yeyote. Mtoto ambaye ni mwongeaji au anayetoa taarifa kwa haraka kwa wazazi au kwa watu wengi wenye tabia mbaya wanawaogopa na huwa hawataki kujihusisha nao kabisa maana wanajua wataumbuka mapema.
Pia Kuna maeneo tukiwa na watoto tunapaswa kuepuka kuishi. Maeneo ambayo ni atarishi mfano Kuna vibaka wengi, Kuna vilabu vya pombe vingi, kuna bar au guest pia Kuna watu ambao unaona kabisa hawaeleweki kimaadili wamekaa kihasara hasara sio sehemu sahii ya kuishi na familia. Kuna msemo unasema " akili iliyokaa kihasara hasara ni kazi ya shetani" ikimaanisha kama akili haijawekezwa kuwaza vitu endelevu inavutia kufanya mambo ambayo si mazuri kwa jamii.
Katika hili mimi napendekeza kwanza wazazi tunapaswa kutambua sisi ni walinzi wa kwanza wa watoto wetu na tuna jukumu la kuwalinda. Ninajua katika malezi kila siku kuna mambo mapya yanatukumba kutokana na sayansi na technolojia. Natamani wizara ya afya na jamii ingekuwa na kitengo maalumu au program maalumu ya kusaidia wazazi jinsi ya malezi. Naamini hata sisi wazazi Kuna mambo hatuyaelewi katika malezi lakini kama tutakuwa na program maalumu inaweza saidia watu wengi kupata uelewa na kusaidia malezi bora ya watoto.
Mlezi wa kwanza wa mtoto ni baba na mama. Lakini mtoto akiwa mdogo zaidi mama ndio mlezi mkuu na anakuwa na ukaribu sana na mtoto kwa maana ya kunyonyesha, kumbadilisha kila mara, kumuogesha n.k. Mama ana mchango mkubwa zaidi katika kulinda mtoto na mama ajengewe uwezo kuanzia akiwa na mimba
Wakati wamama tuna mimba pale tunapoenda clinic kungekuwa na darasa la malezi la kulinda mtoto na umuhimu wa ukaribu wa mama na mtoto kuanzia miaka 0 mpaka miaka 7 ya mwanzo ya utoto wake. Tunajua mtoto kuanzia mwaka 0 mpaka 7 anakuwa bado hawezi jitetea lakini mama akifundishwa jinsi ya malezi vitu gani kuepukana navyo jinsi ya kumuweka mwanawe karibu na kujua siku nzima mwanawe amefanya nini itasaidia kupunguza tatizo hilo. Lakini pia ujasiri wa mtoto unajengwa kuanzia 0 mpaka miaka 7. Ninaamini kama wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalimu ikiwekeza katika kumfunza mama jinsi ya kujali watoto wake tungepunguza kesi nyingi za ubakaji na kulawiti.
Progam maalumu iwe ina vitu vifuatavyo
1. Umuhimu wa mtoto kumjua Mungu na kujua vitu gani ni sahii ambavyo mzazi anapaswa kumwelekeza mwanawe na kumsaidia mwanawe kuwa karibu na Mungu wake.
2. Mzazi afundishwe umuhimu wa kuwa karibu na mwanawe (Bonding/attachment) inasaidia kuwa na watoto wenye afya ya akili. Na watoto watakuwa jasiri na wataweza kueleza matatizo yao kwa ufasaha.
3. Wazazi wawe na vikundi vya kusaidiana katika malezi maana mzazi moja hawezi kumlea mwanawe peke yake. Kuna msemo unasema “inachukua kijiji kizima kuweza kulea mtoto moja anayejitambua”
4. Mzazi ajue hatakiwi kuwa mkali sana mpaka mtoto akamwogopa kwa kuwa mzazi akiwa mkali sana inaweza ikasababisha mtoto akiwa ana shida hataweza mweleza mzazi wake.
5. Umuhimu wa mzazi awe na muda na mwanawe katika malezi asiwe mtu wa kuwaachia ndugu tu au majirani.
6. Wazazi waelekezwe jinsi ya kumfundisha mwanawe kuwa sehemu zipi hapaswi kuguswa na mtu mwingine. Mfano sehemu za siri na maziwa na pia waambiwe hawaruhusiwi kukaa katika sehemu zenye vificho.
7. Wazazi wafundishwe pia ubaya wa tekinolojia katika malezi ya mtoto akiwa mdogo. Wazazi wawe wanajua pia tekinolojia ikitumika vibaya watu wabaya wanaweza tumia kufundisha watoto wao mambo mabaya na kufanya watoto waharibike.
8. Serikali iwekeze kila mtaa kuwe na viwanja vya mpira na sehemu za kucheza watoto ili watoto wawe na sehemu ya kucheza.
Program iwe inafundishwa katika njia tofauti
1. Kuwe Kuna siku maalumu ya clinic ambayo watu wote walio na mimba kwa kila mwezi waweze kupata masomo ya malezi kwa mwezi iwe mara moja.
2. Kuwe na program ya malezi ambayo inaweza kuwa inarushwa mara moja au mbili kwa wiki kwenye TV AU radio.
3. Pia kuwe na short clip ambazo ziweze kuwa zinarushwa Instagram, whatup , Facebook na YouTube ambazo zinahusu malezi.
4. Pia kuwe na filamu tofauti ambazo zifanywe na wasanii zinazoelezea malezi mazuri ya watoto na filamu ziwe na ubora ambao watu wengi waweze kuvutuwa kuangalia
5. Watoto pia wa shule za msingi wajengewe uwezo wa kujikinga kwa kufundishwa kalate maana ni njia mojawapo wenzetu nje wanasaikolojia wanawafundisha watu waliopata tatizo hilo maishani ili kujikinga wasifanyiwe tena.
6. Pia watoto wawe na somo la kuwasaidia kuweza kueleza matatizo wanayopitia katika maisha yawezekana wazazi ni wakali lakini wafundishwe kujua JINSI gani wanaweza kusema matatizo yao sehemu salama inawezekana shuleni au polisi.
7. Pia kuwe na kamati maalumu ya kuratibu matatizo haya kwa haraka
8. Pia kuwe na mwanasaikolojia ambaye ana mafunzo kila shule na ikiwezekana kila serikali ya mtaa kuweza kutoa msaada wa haraka kwa matatizo kama haya na mengine ya kiafya ili kusaidia watu wawe na afya ya akili.

Upvote
10