Wewe umeamua tu kutoka nje ya hoja, hayo ni majukumu tu ambayo kwa africa yameshaonekana ni ya mwanamke tangu enzi za mababu, kama tu ambavyo kutafuta chakula lilionekana jukumu la mwanaume
Lakini leo hii tunavyoongea dunia imebadilika hakuna kazi za kike wala za kiume, ila wanaume wa kiafrika ndio bado mmeng'ang'ania hizo kazi za nyumbani ziwe majukumu ya mwanamke, ilihali kwenye suala la kutafuta pesa ndio mnajifanya kukubali kwamba dunia imebadilika ati mwanamke naye anatakiwa atafute pesa
Majukumu ya asili ya mwanamke ambayo mwanaume hawezi kufanya ni kubeba mimba, kuzaa, kunyonyesha na kulea watoto, hayo majukumu mengine ni gender roles tu ambazo zinaweza badilika kulingana na wakati sababu hazihitaji jinsia bali yeyote mwenyewe viungo vilivyokamilika aweza kuzifanya, sema wanaume wengi mmeamua kujiendekeza kuwa hamuwezi kufanya hizo kazi za nyumbani ati ni jukumu la mwanamke wakati siku hizi wanawake nao wanasaidia majukumu yenu ya kutafuta pesa
Wewe unaonekana umesoma au kushiriki sana makongamano ya mafeminists na ndio yanachangia sana kuwapotosha akili watoto wa kike wa sasa.
Sasa unasemaje hakuna gender roles wakati kiuhalisia hizo zipo tokea miaka na miaka. Gender roles si jambo la mtu kuamua bali ni matokeo ya mazingira. Nitakupa mifano.
Mfano jeshini popote duniani kuna mabomu au mizinga ambayo ikibutuka mwanamke anaweza pata hedhi hapo hapo, kama haujui hili tafuta askari wa kikosi cha mizinga atakuelekeza. Majeshi ya marekani kipindi wamekwenda misheni zao huko iraq, wale viongozi wa makundi walikiri kuwa askari wa kike walikuwa wakiwarudisha nyuma sana sababu wapo emotional eneo la vita na kuna milipuko au mashambulizi na matukio yaliwafanya waanze kuomba poo na kukataa kuendelea.
Mahoteli makubwa 90% wanakuwa na wapishi wanaume ingawa mwanamke ndie ina aminika ni mpishi mzuri. Sababu ikaja kuonekana kuwa mwanamke hawezi kuhandle mishe za majiko makubwa, kufokea wapishi na kuwapanga ma kukimbizana na order za wateja wakati akisimamia ubora wa chakula.
Maofisini huko mataifa ya magharibi ambayo ndio yanaongoza kwa kupigia chapuo la mwanamke na mwanaume ni sawa, makampuni ya wenzetu wanatumia technology kustudy uwezo na ufanisi wa employees, graph [emoji409] za waajiriwa wa kike huwa zinaanza vizuri sana siku za kwanza ila muda unavyokwenda huwa zinaanza kushuka kwa kasi na chache hurudi tena pale zilipokuwa but nyingi hufeli kurudi juu. Kilichokuja kugundulika ni kuwa mwanamke hawezi kudeal consistently na corporate stress sababu ya vitu kama maswala ya hedhi yanayoathiri ufanisi wake, wanawake wanapokuwa challeged kidogo wanatafuta utetezi badala ya kupambana wenyewe kama wenyewe, na hata wakijilazimisha hii inawagharimu upande wa akili kufocus maana mood zao huwa zipo harsh kwa staff wengine. Hii ukiingia mtandaoni utaona hizi tafiti, na ndio imepelekea kuna wage gap kati ya employees wa kiume na wakike na tafiti zimewabana feminists kutetea wanawake kwenye hili wanataka kulipwa sawa na wanaume wakati wana delivery mbovu ya matokeo.
Tazama kazi za ndani tu wewe ni shahidi hapo. Ukiwa unatafuta msaidizi wa kazi za ndani kukusaidia unapokwenda kazini asubuhi na kurejea jioni, ukiletewa binti wa miaka 22 na kijana wa miaka 22 na wote wapo vema utachagua house girl au house boy?!
Kama gender roles hazipo then kwann inapotokea hatari unategemea mwanaume akuprotect kwann wewe usichukue panga ukapambane na majambazi mwanaume akae ndani umlinde?
Kama hakuna gender roles, kwann kuna kazi huwezi kuta wanawake wanagombania na uwezekano wa kuingia ni mkubwa sana kuliko mwanaume?
Mwanamke pesa yake 9/10 times huwa haina faida kwa mwanaume so its pointless kuamini mwanamke anapambana kama team mate bali yeye huwa anatafuta kusolve matizo yake personally yaani saloon, kununua nguo za bei, kula vizuri, amnunulie mtoto zawadi(sio mahitaji ya mtoto yote),atoke out, alipe michango ya vikoba, etc.
Kimsingi, hayo uliyosema ni mawazo ya kimagharibi ambayo mabinti wengi mnayaokoteza huko mitandaoni but mnashindwa kuapply logic kuelewa kuwa si kila jambo linawezekana sababu umeliperceive kuwa linawezekana. Unaweza ukasema unataka kuja kuwa milionea kabla ya umri wa miaka 30 ila mazingira ndio yataamua. Unaweza uwe milionea ila katika mazingira yako hakunaga mamilioni so upo bound kurudi tena kuwa mtu wa kawaida sababu forces za mazingira yako zitakurudisha chini kwa nguvu. Ila ukawa kapuku ukaenda mfano japan ambapo wastani wa vijana 10 basi 8 wapo vema kiuchumi so ukienda hapo na ukajipa maono ya kuwa milionea then its very possible utakuwa milionea na hautatumia nguvu nyingi kubaki kuwa milionea.
So hizi idea zako na nyingine nyingi ambazo huwa naona watoto wa kike mnazibeba huwa nawaonea tu huruma maana in reality hazipo na unakuta mnatumia exceptions kudefine reality jambo ambalo ni ignorance of nature na mnalitumia kama bliss ya existence katika maisha hadi pale reality inapowatokea na kuwazidi nguvu.