Malezi Duni na Utandawazi ndio Chanzo cha ongezeko la mijadala ya kupinga na kukosoa ndoa na maisha ya ndoa

Malezi Duni na Utandawazi ndio Chanzo cha ongezeko la mijadala ya kupinga na kukosoa ndoa na maisha ya ndoa

Mkuu Mimi naona Maisha ya Mtu kukaa single bila Attachment na Mwanamke ni mazuri Sana

Kula vizuri
Lala vizuri
Sali Sana
Kataa ndoa
Tafuta pesa kwa ajili yako na wazazi na wasiojiweza huu mradi wa Ndoa unawafaidisha wanawake tu.
Huu ni ubinafsi wa hali ya juu
 
Na weng inaelekea ni watoto waliozaliwa nje ya ndoa hawajui umuhimu wa familia na ndoa jazia nyamanyama kwenye kukosa malezi hapo
Mimi naona hawana nguvu za kiume [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] ndo maana wameamua kujificha kwenye kichaka cha kataa ndoa.
 
Mkuu unapokuja na personal attacks onesha tatizo liko wapi kwenye hoja yangu, wewe ulitakaje ulitaka mwanamke akusaidie kutafuta pesa halafu na majukumu yake afanye peke yake ipasavyo huku wewe ukitafuta pesa tu, au wewe ulitaka iwe vipi
Kweli hapo sasa ndipo SIJALI anakutana na POTELEA MBALI.
 
Ndoa inaweza kukufanyia mambo haya...

1. Ndoa inaweza kubadilisha Maisha yako
2. Ndoa inampa mtu heshima kwa jamii
3. Ndoa inakuweka karibu na MUNGU
4. Ndoa inakukomaza kiakili

Pia ndoa inaweza kukufanyia haya
1.ndoa itakuchanganya uonekane kituko
2. Ndoa itakuua kwa mawazo
3. Ndoa itakufilisi ubaki masikini kabisa
4. Ndoa itakuweka karibu na shetani


Mimi naona ni vinzuri sana kutokurupuka kwenye swala kubwa kama hilo,ni vyema kuchukua mda mrefu kuamua kuishi na mtu
 
Mkuu Mimi naona Maisha ya Mtu kukaa single bila Attachment na Mwanamke ni mazuri Sana

Kula vizuri
Lala vizuri
Sali Sana
Kataa ndoa
Tafuta pesa kwa ajili yako na wazazi na wasiojiweza huu mradi wa Ndoa unawafaidisha wanawake tu.
Unalijua lengo la ndoa? Mwishoni umemaliza vizuri sana kwamba unatafuta kwa ajili ya wazazi wako je kama ndivyo unafikiria wewe utakuwa kijana daima au unakumbuka kwamba kuna siku pia wanao watatakiwa kukulea tana waliotokana na familia bora ya mke na mume walioishi pamoja na mkawapa malezi bora? Tujitafakari na tuache ubinafisi.
 
Actually ninyi ndio mnaotumia mihemko badala ya logic, nikikuuliza wewe mwanamke aliyeajiriwa anayetoka saa kumi na mbili asubuhi na kurudi saa kumi na mbili jioni amechoka kama mumewe anawezaje kuhandle majukumu ya nyumbani ipasavyo sidhani kama utanijibu bila kutumia mihemko, zaidi sana utaishia kuniuliza anachokaje wakati hayo ni majukumu yake nami nitajua tu kwamba ndio wale wale
Hahaha na hapo ndo tunakuja anachangia kiasi gani kwenye pato la familia??

Simple tu..

Mwanamke ana fanya kazi, mwanaume anafanya kazi.Hela yake inachangia kiasi gani kwenye pato la familia..

Kama ana changia well & Good..

Maana hapo tunazungumzia kuwa na wafanyakazi hata wawili, tunazungumzia washing machine, tunazungumzia vitu vingi hapo costs zitagawanywa kwa utaratibu flani...

Au ndo tunarudi kule kule hela ya mwanamke haiguswi[emoji1787][emoji1787][emoji125][emoji125]

Kama unaweza kukaa mezani uka prove mchango wako bila kuanzia ku blame mtu,Yes you are fine...[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Mtu anayekataa ndoa unakuta mama yake na baba yake wanaishi kwenye ndoa ila akija huku kataa ndoa kataa ndoa.Raha sana kuishi bila ndoa mpk pale utakapofika uzeeni.Utarudi hapa enzi hizo na kusoma hizi mada utajilaumu.Maisha bila ndoa watoto unawalea kiholela holela unatia mimba hapa unaacha unampa mimba yule unaacha.Kadri watoto wanavyokuwa na sumu watakazomezeshwa na hao akina mama utagundua ulikuwa unajaza maji kwenye gunia
 
Ndio design ya wanaume tulionao hivi sasa kwenye jamii yetu, wabinafsi na wasiotaka kusikia ukweli na wakikosa hoja ndio huja na personal attacks kama hizi, wanawake tuna kazi na safari ndefu sana
Nimekuattack wapi?
 
Ndio mkuu hapa naongelea mwanamke ambaye anatafuta pesa na anachangia pato la familia, kama nilivyosema kwamba ukiona mwanamke pesa yake haiguswi basi ujue majukumu yake ya nyumbani anayafanya hivyo haoni haja ya kusaidia majukumu ya mwanaume wakati ya kwake hasaidiwi, sasa shida inakuja kuna wanaume wanataka mke atafute pesa achangie pato la familia na bado afanye majukumu ya nyumbani huu ndio ubinafsi ninaozungumzia hapa
Kama tumekubaliana hapo basi ni sawa kabisa.Mume kuwa na uelewa na kukubali baadhi ya vitu havitawezekana..

Na shida sio mke bali ni mfumo mzima ambao mmechagua kuuapply kwenye ndoa yenu...

Sasa mwanaume akitaka mwanamke afanye kazi,achangie pato la familia bado afanye kazi zote za nyumbani nadhani huyo anataka kuoa mtumwa sio mke...
 
Wengi hawajitambui Wana stress za maisha instead ya kutafuta wanawake wenye heshima wanagombana haww wavaa nusu uchi ..Nina rafiki zangu wengi wameoa wale wanawake wa dini haswa wako kweny ndoa zaidi ya miaka 5 wanafurahi .

Sio unaona mwanamke alishawahi kuwa na majamaa kibao huko nyuma unafikria atatulia kwani we ni Nan? ..wenzenu wanaoa wanawake wanajielewa wao ni hao wanapokutana nao bar sijui coco beach wakidanga
Hata kanisani Kuna malaya wengi Sana

We ukimpata anayejielewa shukuru lakini ni probably 3 ya 10 kupata aliyetulia kabisa
Dunia imebadilika Sana
 
Tatizo liko hapa
Kukimbilia kuoa
Kuoa kwasababu ya umbo, sura
Kuoa bila kuvhukua muda wa kujiridhirisha kama anakufaa ama la na kama unamfaa
Kuoa bila kujua, kupeleleza background yake, marafiki zake ndugu zake ukoo wake na hata kabila sometimes

Kuna baadhi ya tabia zitajifunua huko mbeleni baada ya ndoa hapo sasa ndio itabidi kutumia akili uzoefu ukomavu na hekima
Binti unayemchumbia atakuwa si chini ya miaka 20, imagine kapitia mangapi mpaka mnaonana?
Mkuu mshana apo kwenye sura na umbo hicho ni kigezo cha kwanza kam wanawake mwenye sura na umbo hawana tabia zuri bora nikate ndoa kuliko kuoa kiumbe cha Mungu chenye sura ya kiume ,hii itakujengea hisia ya kuona waupinde wapo sahii kama unaishi na mdada mwenye sura ya baba.
 
Mkuu mshana apo kwenye sura na umbo hicho ni kigezo cha kwanza kam wanawake mwenye sura na umbo hawana tabia zuri bora nikate ndoa kuliko kuoa kiumbe cha Mungu chenye sura ya kiume ,hii itakujengea hisia ya kuona waupinde wapo sahii kama unaishi na mdada mwenye sura ya baba.
Usioe mwanamke mzuri sana .. Hao huwa ni mapambo tu ya kufurahisha macho.. Oa wife material
 
Back
Top Bottom